مختصر صحيح البخاري للزبيدي
رتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقات
السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسيني
خادم السنة النبوية
*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.
*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *
Sayyid Abdulqadir Shareef
MTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME
*Leo Siku ya Jumatano, tarehe 30, Saffar, 1446, H., sawa na tarehe 04, Septemba, 2024. *
(9)
كِتَاب مَوَاقِيتِ الصَّلاَةِ
KITABU CHA NYAKATI ZA SWALA
363- وعَنْهَا رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: رَكْعَتَانِ، لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَدَعُهُمَا، سِرًّا وَلاَ عَلاَنِيَةً: رَكْعَتَانِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَرَكْعَتَانِ بَعْدَ الْعَصْرِ. [رواه البخاري: 592].
- Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها akisema: “Rakaa mbili Mtume ﷺ hakuwa anaziacha si kisiri siri wala waziwazi nazo ni rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri na rakaa mbili baada ya laasiri.” [Bukhari:592]
UFAFANUZI
Mtume ﷺ alikuwa anaswali rakaa mbili laasiri lakini hii ilikuwa khususwia yake, ndiyo maana alikuwa anaziswali peke yake nyumbani lakini zimekatwaza.
25- بَاب: الأَذَانِ بَعْدَ ذَهَابِ الْوَقْتِ
- Mlango: Kuhusu kuadhini baada ya wakati wa swala husika kupita
364- عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: سِرْنَا مَعَ النَّبِيِّ ﷺ لَيْلَةً، فَقَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ: لَوْ عَرَّسْتَ بِنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: «أَخَافُ أَنْ تَنَامُوا عَنْ الصَّلاَةِ». قَالَ بِلاَلٌ: أَنَا أُوقِظُكُمْ. فَاضْطَجَعُوا، وَأَسْنَدَ بِلاَلٌ ظَهْرَهُ إِلَى رَاحِلَتِهِ، فَغَلَبَتْهُ عَيْنَاهُ فَنَامَ، فَاسْتَيْقَظَ النَّبِيُّ ﷺ وَقَدْ طَلَعَ حَاجِبُ الشَّمْسِ، فَقَالَ: «يَا بِلاَلُ! أَيْنَ مَا قُلْتَ؟» قَالَ: مَا أُلْقِيَتْ عَلَيَّ نَوْمَةٌ مِثْلُهَا قَطُّ. قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ قَبَضَ أَرْوَاحَكُمْ حِينَ شَاءَ، وَرَدَّهَا عَلَيْكُمْ حِينَ شَاءَ، يَا بِلاَلُ، قُمْ فَأَذِّنْ بِالنَّاسِ بِالصَّلاَةِ» فَتَوَضَّأَ، فَلَمَّا ارْتَفَعَتْ الشَّمْسُ وَابْيَاضَّتْ،( ) قَامَ فَصَلَّى. [رواه البخاري: 595].
- Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah رضي الله عنه akisema: “Tulisafiri usiku mmoja na mtume ﷺ Tulivyofika njiani baadhi ya watu wakasema: “Lau tungesimama hapa njiani tukapiga kambi” Mtume ﷺ akawaambia: “Nachelea msije mkapitiwa na usingizi” Bilal alivyosikia maneno hayo akasema: “Mimi nit akuamsheni jionyoosheni tu” na Bilal akakaa na kuegemea masoji au mizingo ya mnyama wake lakini akapitiwa na usingizi. Mtu wa mwanzo kuzindukana alikuwa mtume ﷺ na wakati huo mwangaza wa jua ushachomoza, mtume ﷺ akasema: “Bilal yako wapi maneno yako uliyoyasema?” Bila akasema: “Sijapata kupitiwa na usingizi kama nilivyopitiwa jana usiku” Mtume ﷺ akasema: “Mwenyezi Mungu anazichukua roho zenu wkaati wowote anaotaka na anakurudishieni roho zenu wakati wowote anaotaka ewe Bilal, haya nasi simama uadhini” Bilal akaondoka akaenda akatawadha na jua lilikuwa limeshachomoza limeinuka juu kidogo ndiyo akaadhini na mtume ﷺ akasimama kuswali.” [Bukhari:595]
26- بَاب: مَنْ صَلَّى بِالنَّاسِ جَمَاعَةً بَعْدَ ذَهَابِ الْوَقْتِ
- Mlango: Kuswalisha jamaa baada ya kupita wakati wa swala husika
365- عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رضي الله عنه جَاءَ يَوْمَ الْخَنْدَقِ بَعْدَ مَا غَرَبَتْ الشَّمْسُ، فَجَعَلَ يَسُبُّ كُفَّارَ قُرَيْشٍ، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! مَا كِدْتُ أُصَلِّي الْعَصْرَ حَتَّى كَادَتْ الشَّمْسُ تَغْرُبُ، قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «وَاللَّهِ مَا صَلَّيْتُهَا» فَقُمْنَا إِلَى بُطْحَانَ فَتَوَضَّأَ لِلصَّلاَةِ، وَتَوَضَّأْنَا لَهَا، فَصَلَّى الْعَصْرَ بَعْدَ مَا غَرَبَتْ الشَّمْسُ، ثُمَّ صَلَّى بَعْدَهَا الْمَغْرِبَ. [رواه البخاري: 596].
- Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdullah رضي الله عنهما akisema: “Umar bin Khattwab رضي الله عنه alifika kwenye vita vya Khandaq baada ya jua kuchwa, akawa anawashambulia na kuwatukana makafiri wa Kiqureshi akisema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu sijapata wasaa wa kuswali laasiri mpaka jua limekuchwa” Mtume ﷺ akasema: “Hata mimi sijaiswali” kwa hiyo wote tukasimama kwenda katika bonde la maji Mtume ﷺ akatawadha na sisi pia tukatawadha akatuswalisha swala ya laasiri baada ya kuwa jua limeshakuchwa kisha akaswali magharibi baada yake.” [Bukhari:596]
KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية
Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
Leave a Reply