Hadithi ya Leo, Ijumaa, tarehe MOSI, SHAABANI, 1446, sawa na tarehe 31, JANUARI, 2025
KUHUSU KUCHINJA MNYAMA WA UDH-HIYA
SEHEMU YA NNE
1349 -* وَعَنْ جُنْدُبِ بْنِ سُفْيَانَ رضي الله عنه قَالَ: {شَهِدْتُ اَلْأَضْحَى مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ فَلَمَّا قَضَى صَلَاتَهُ بِالنَّاسِ، نَظَرَ إِلَى غَنَمٍ قَدْ ذُبِحَتْ، فَقَالَ: “مَنْ ذَبَحَ قَبْلَ اَلصَّلَاةِ فَلْيَذْبَحْ شَاةً مَكَانَهَا، وَمَنْ لَمْ يَكُنْ ذَبَحَ فَلْيَذْبَحْ عَلَى اسْمِ اَللَّهِ”} مُتَّفَقٌ عَلَيْه*.
- Imepokewa kutoka kwa Jundub bin Sufyan رضي الله عنه akisema: “Nilihudhuria Swala ya Idd na Mtume . Alipomaliza kuwaongoza watu katika swala aliangalia akamuona mbuzi mdogo ameshachinjwa. Akasema: “Nani kachinja mbuzi huyu kabla ya Swala ya Idd? Kama ni hivyo, achinje mbuzi mwingine mbadala wa mbuzi wa Udh-hiya. Na yule ambaye bado hajachinja, akichinja aseme Bismillahi.” Muttaq alayhi.
UFAFANUZI
Hadithi hii, inatufundisha kuwa wakati wa kuchinja mnyama wa Udh-hiya ni kuanzia asubuhi Baada ya kuswaliwa Swala ya Idil Adh-ha, na kuendelea mchana kutwa hadi baada ya kuswaliwa Swala ya Laasiri. Na kwa maana hiyo, atayechinja ndani ya wakati huo, atakuwa ametekeleza Ibada husika, ndani ya wakati wake. Lakini akichinja KABLA ya kuswaliwa Swala ya Idi Al-Adh-ha, basi mnyama wake hawezi kuwa ni mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya Al-Adh-ha. Huyo atakuwa ni Sadaka kama sadka yoyote nyengine. Na mtu ambaye hajawahi kuchinja mnyama wa Udh-Hiya, basi akichinja, ndani ya wakati wa kuchinja mnyama wa Udh-hiya, basi achinje mbuzi au kondoo, na apige _Bismillahi._ Kwa maana hiyo, wakati wa kuanza kuchinja mnyama wa Udh-iya ni baada ya Kuswaliwa swala ya Idi, iliyo ongozwa na Kiongozi Mkuu wa Waislamu. Sawa sawa, mchinjaji awe ameshaswali swala ya Idi, au hajaswali. Kigezo ni kumalizika Swala ya Idi ya watu wote, iliyoongozwa na Kiongozi Mkuu wa Waislamu. Ni vyema mchinjaji awe na yeye ameshaswali swala ya Idi, ila siyo lazima awe ameshaswali swala ya Idi, maana wakati wa kuanza kuchinja ni Baada ya Kiongozi mkiuu kumaliza kuswalisha Swala ya Idi, na kwa maana hiyo mchinjaji aliyeswali au hajaswali swala ya Idi, inamjuzia kuchinja mnyama wa Udh-hiya, ilimradi amchinge Baada ya kumalizika kuswaliwa swala ya Idi, na kiongozi mkuu wa Umma. Na wakati wa kuswali Swala ya Idi, ni baada ya kuchomoza Jua, na kuinuka juu urefu wa mkuki. Kabla ya hapo haijuzu kuswali swala yoyote ile.
WANAZUONI WAMETOFAUTIANA KUHUSU WAKATI WA KUCHINJA MNYAMA WA UDH-HIYA.
Kwanza, Imamu Abu Hanifa ni kuanzia kuingia alfajiri ya siku ya mwanzo ya Sikukuu ya Idi al-Adh-ha, hadi kumalizika kuswaliwa Swala ya Idi husika.
PILI: Imam Malik ni kuanzia anapoingia Imamu kuswalisha Swala ya Idi na kuendelea mchana kutwa.
TATU: Imam Shafi ni kuanzia kumalizika Swala ya Idi, hadi kuingia magharibi ya Sikukuu ya Tatu ya mfungo tatu. Dalili yake ni Hadithi kutoka kwa Mtume ﷺ isemayo: “كل يوم التشريق ذبح” [رواه أحمد (16309)]. “Siku zote za kukausha nyama ni siku za kujuzu kuchinja mnyama wa Udh-hiya.” Ameipokea Ahmad, H.16309.
Dalili yake nyengine ni Aya ya Qur’ani isemayo:
لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ
Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri. (Surat, Al-Hajj, 22:28)
YALIYOMO NA YATOKANAYO
- Wakati wa Ibada ya kuchinja mnyama wa Udh-hiya, ni BAADA ya kumalizika kuswaliwa Swala ya Idi, chini ya Uimamu wa Kiongozi mkuu wa Waislamu.
- Mara baada ya kumalizika kuswaliwa Swala ya Idi, chini ya Uimamu wa Kiogozi mkuu wa Waislamu, basi wakati wa kuchija mnyama wa Udh-hiya unaanza, na kuendelea mchana kutwa wa Siku ya Mwanzo ya Idi husika.
- Inavyo onesha Hadithi hii ni kuwa ataye chinja mnyama wa Udh-hiya, Kabla ya kuswaliwa Swala ya Idi, basi kichinjwa chake ni sadaka tu.
- Ataye pitiwa kuchinja mnyama wake wa Udh-hiya, kwa kusahau, au kupitiwa na usingizi, au kwa kutokujuwa wakati wa kuchinja mnyama wa Udh-hoya, basi anaweza kumchinja ndani ya siku tatu za mwanzo za Sikukuu ya Idi Al-Adh-ha.
- Mwenye kupitiwa na wakati wote wa kuchinja mnyama wa Udh-hiya, hawezi kukubaliwa kichinjwa chake kuwa ni mnyama wa Udh-hiya; bali ni sadaka tu, kama sadaka yoyote nyengine,
- Mnyama wa Udh-hiya ndio Ibada kubwa kabisa ya kujitolea, inayopendwa na Mwenyezi Mungu katika Idil Udh-hiya.
والله أعلم
وبالله التوفيق
HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!
IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
*Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *
من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية
KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO*
JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA
UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.
NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, na kuweka kwenye FB yako, WhatsApp, na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com
Leave a Reply