Hadithi ya Leo, Jumatano, tarehe 28, Rajab, 1446, H, sawa na tarehe 29, JANUARI, 2025
KUHUSU KUCHINJA MNYAMA WA UDH-HIYA
SEHEMU YA PILI
1346 – عَنْ أَنَسِ بنِ مَالِكٍ رضي الله عنه{أَنَّ اَلنَّبِيَّ كَانَ يُضَحِّي بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ، أَقْرَنَيْنِ، وَيُسَمِّي، وَيُكَبِّرُ، وَيَضَعُ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا، وَفِي لَفْظٍ: ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ . وَفِي لَفْظِ: { سَمِينَيْنِ} وَلِأَبِي عَوَانَةَ فِي “صَحِيحِهِ” : { ثَمِينَيْنِ . بِالْمُثَلَّثَةِ بَدَلَ اَلسِّين ِ وَفِي لَفْظٍ لِمُسْلِمٍ، وَيَقُولُ: { بِسْمِ اَللَّهِ. وَاَللَّهُ أَكْبَرُ }.
- Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه akisema: “Mtume alikuwa na kawaida ya kuchinja kondoo wawili wa Udh-hiya, ambao walikuwa wa rangi nyeupe, wenye pembe. Hupiga Bismillahi kisha hupiga Takbir na kuweka mguu wake kwenye bega mnyama huyo, halafu humchunja kwa mkono wake, mwenyewea.” Muttafaq alayhi, Riwaya nyengine inasema: “Walikuwa wanene.” Riwaya ya Abi Awana, kutoka kwenye Kitabu chake Swahihi, inasema: “Wenye thamani kubwa.” Riwaya ya Muslim inasema inasema: “Na husema Bismillahi Wallahu Akbar!”
UFAFANUZI
Hadithi hii inatusimulia kitendo cha Mtume ﷺ inapoingia asubuhi ya siku ya Idi Al-Adh-ha, alikuwa na kawaida ya kuchinja kondoo wawili, weupe, wenye pembe, wanene na wenye thamani kubwa, kwa kupiga _Bismillahi_ na Takbiri, baada ya kuweka mguu wake mgongoni mwa mnyama husika, karibu ma shingo ya mnyama husika, na kuwachinja kwa mkono wake mwenyere. Kitendo hicho cha kuchijna wanyama wawili wa Udh-Hiya asubuhi ya Siku ya Idi kubwa, baada ya Swala ya Idi, kilikuwa hakimpiti Mtume ﷺ, na hivyo ni Sunna kwa Wafuasi wake, wenye uwezo na wasaa wa kufanya hivyo wafanye; kama tutavyo kuja kuona hapo chini, kwenye Hadithi na,bari 1348, Mtume ﷺ akiamrisha wafuasi wake wachinje wanayama ya Udh-hiya..
1347 – وَلَهُ: مِنْ حَدِيثِ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا; { أَمَرَ بِكَبْشٍ أَقْرَنَ، يَطَأُ فِي سَوَادٍ، وَيَبْرُكُ فِي سَوَادٍ، وَيَنْظُرُ فِي سَوَادٍ; لِيُضَحِّيَ بِهِ، فَقَالَ: “اِشْحَذِي اَلْمُدْيَةَ”، ثُمَّ أَخَذَهَا، فَأَضْجَعَهُ، ثُمَّ ذَبَحَهُ، وَقَالَ: “بِسْمِ اَللَّهِ، اَللَّهُمَّ تَقَبَّلْ مِنْ مُحَمَّدٍ وَآلِ مُحَمَّدٍ، وَمِنْ أُمّةِ مُحَمَّدٍ” }.
- Imepokewa na Anas bin Malik, kutoka kwa ‘Aisha رضي الله عنها akisema: “Aliamrisha aletewe kondoo wawili Weupe, wenye pembe ambao miguu yao ni meusi na matumbo yao ni meusi na macho yao ni meusi ili awachinje kuwa ni wanyama wa Udh-hiya. Walipo letwa aliniambia: “Noa kisu!” Kisha akakichukua, akamlaza chini kondoo na kumchinja na kusema: “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu kubali kichinjwa hiki kutoka kwa Muhammad na ukoo wa Muhammad na kwa niaba ya umma wa Muhammad!”
UFAFANUZI
Hadithi hii, kutoka kwa Mama Aisha رضي الله عنها inatusimulia kuwa Mtume ﷺ, alikuwa na kawaida ya kuchinja mnyama wa Udh-hiya, mwenye rangi nyeupe, lakini miguu yake na tumbo lake na macho yake huwa ya rangi nyeusi; ambaye alikuwa akizingatiwa kuwa ni miongoni mwa kondoo au mbuzi wanao thaminiwa sana, kutokana na unadra wa rangi zake. Na alimuamuru Mama Aisha ameletee kisu na akinowe, sawa sawa. Mtume ﷺ baada ya kuletewa hicho kisu na kunolewa, alikipokea na kumlaza chini kichinjwa husika, kisha akasema: “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu! Ewe Mwenyezi Mungu kubali kichinjwa hiki kutoka kwa Muhammad na ukoo wa Muhammad na kwa niaba ya umma wa Muhammad!”
Hivyo, Hadithi zote mbili hizi, kutoka kwa watu waliokuwa karibu sana na Mtume ﷺ, mmoja akiwa mtumishi wake wa kujitolea, na wa pili akiwa mkewe, zinatusimulia kwa kirefu aina ya wanayama aliokuwa akipendelea Mtume ﷺ kuwachinja asubuhi ya Sikukuu ya Idi Kubwa, na ambao alikuwa akiwachinja kwa mkono wake mwenyewe. Alikuwa akipendelea kuchinja kondoo au mbuzi weupe, wenye rangi nyeusi miguuni mwao na tumboni mwao na kandokando ya macho yao. Walikuwa ni wanyama wenye pembe, na ambao kutokana na kuwa na sifa adimu kama hizo, walikuwa wenye thamani kubwa na kupendwa sana na watu.
Wanazuoni wamesema:
أنَّ اختيار الأضحية كريمة وطيبة هو من تعظيم شعائر الله؛ قال تعالى: {ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ (32)} [الحج: 32]؛ فهي من أعلام دين الإِسلام، قال ابن عباس: تعظيمها: استسمانها واستحسانها.
Kuchagua mbuzi au kondoo wa Udh-hiya wawe miongoni mwa wanyana wenye sifa nzuri, wenye kupendeza na kupendwa sana na watu, kwani kufanya hivyo ni dalili ya kutukuza Ishara za Mwenyezi Mungu, kama Alilvyosema: Ndiyo hivyo! Na atayetukuza Ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.! (Al-Hajj, 25:32) Amesema Ibn Abbas: “Na kufanya hivyo, ni kuonesha utukufu wa Ishara kubwa za Dini ya Uwislamu, kuzifanya ziwe kubwa, nono, na zenye kuvutia kutendwa!” Hivyo, kuchinja mnyama asubuhi ya Sikukuu kubwa, baada ya kuswaliwa Swala ya Idi, ndiyo amali kubwa na bora ya kujitolea siku hiyo, kwa wakati wake na kwa Sunna zake, kama alivyo sema na kuusia Mtume ﷺ kupitia kwa Mama Aisha:
عن عائشة -رَضِيَ اللهُ عَنْهَا- أنَّ النَّبي -صلى الله عليه وسلم- قال: “ما عمل ابن آدم يوم النَّحر عملًا أحب إلى الله من هراقة دم؛ فطيبوا بها نفسًا “.
Imepokewa kutoka kwa Aisha رَضِيَ اللهُ عَنْهَا akisema: “Amesema Mtume ﷺ: Hakuna amali bora, atayo weza kuifanya mwanadamu, Siku ya Idil Al-Adhha, kwa kujitolea na ambayo inapendwa, zaidi, na Mwenyezi Mungu, kuliko kuchinja mnyama na kumwaga damu yake; hivyo fanyeni amali hiyo kwa ridhaa yenu!”
YALIYOMO NA YATOKANAYO (kweye Hadithi mbili hizi)
- Hadithi hizi mbili na nyingi nyenginezo ni dalili ya Uhalali wa Asasi ya Kuchinja mnyama asubuhi ya Sikukuu ya Idi ya Mfungo tatu.
- Hakuna Amali bora ya kujitolea asubuhi ya Sikukuu ya Mfungo tatu, kama kuchinja mnyama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kuigawa nyama yake nyumbani na kwa ndugu, jamaa, majirani na maskini.
- Kuchinja mnyama wa Udh-hiya asubuhi ya Sikukuu ya Mfungo tatu, ndiyo amali inayopendwa, zaidi, na Mwenyezi Mungu, kuliko hata kutoa sadaka.
- Inapendekezwa kutafuta mnyama mzuri, mwenye afya, aliye nona, na anaye thaminiwa na kupendwa sana na jamii husika.
- Sunna ni kumchinja mwenyewe, kwa mkono wake, na kama hawezi basi awepo anapochinjwa kwa niaba yake.
- Miongoni mwa wanayama wanaopendekezwa, zaidi, ni wenye rangi nyeupe, miguu na tumbo yenye rangi nyeusi, na kandokado ya macho meusi; ila itategemea sifa zinazopendwa sana na watu wa jamii husika.
- Inasuniwa kupiga Bismillahi, wakati wa kuchinja, na kuongezea kusema: Allahu Akbar.
- Sunna kuhakikisha kuwa ala inayotumiwa kumchinja mnyama wa Udh-hiya, iwe ni kali yenye kuweza kukata mishipa ya kooni, kwa haraka, pasi na kumtesa na kumuadhibu mnyama husika.
- Hakuna jinsia maalamu katika kuchinja mnyama wa Udh-hiya, ilimradi ni Mwislamu, aliye kwisha balighi, na mwenye akili timamu.
- Ni makuruhu kuchinja mnyama wa Udh-hiya, mbele ya mnyama mwengine anaye ona na kushuhudia kuchinjwa mnayama mwenzake: huko ni kutesa na kuadibu; haramu.
- Inamjuzia mtu kuchinja mnyama mmoja, kwa niaba yake na kwa niaba ya watu wa nyumbani kwake anaowajibika kuwatunza na kuwaangalia.
- Hakuna Dua maalumu ya kuomba kwa lugha yoyote, ila ni bora kuomba kupitia mojawapo wa Dua alizokuwa akiomba Mtume ﷺ wakati wa kuchinja mnyama wa Udh-hiya.
- Miongoni mwa Dua mbali mbali alizokuwa akiomba Mtume ﷺ wakati wa lichinja ni:
- “اللهم هذا منك ولك وحدك، لا إلى سواك، فلا رياء، ولا سمعة.
- “باسم الله، الله أكبر، اللهم هذا منك ولك”.
- “اللهم تقبَّل عني، وعن أهل بيتى، وعن أقاربى “.
والله أعلم
وبالله التوفيق
HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!
IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
*Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *
من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية
KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO*
JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA
UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.
NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, na kuweka kwenye FB yako, WhatsApp, na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com
Leave a Reply