DARSA YA BM.14.4\1 MLANGO WA UDH-HIYA

Hadithi ya Leo, Jumaane, tarehe 27, Rajab, 1446, sawa na tarehe 28, JANUARI, 2025

KUHUSU KUCHINJA MNYAMA WA UDH-HIYA

SEHEMU YA KWANZA

بَاب اَلْأَضَاحِيِّ

  1. Mlango kuhusu Mbuzi wa Udh-hiya
    مقدمة
    UTANGULIZI Neno الأضاحي ni wingi wa أُضحيَّة likimaanisha KICHINJWA cha siku ya Idi ya Mfungo Tatu, عيد الأضحى baada ya Swala ya Idi.

وهي مشروعةٌ بالكتاب، والسنَّة، والإجماع: قال تعالى: {فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ (2)} [الكوثر].
Na ni Asasi iliyothibiti kupitia Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na Sunna ya Mtume ﷺ tokea ya Kauli hadi ya Vitendo, na pia imethibiti kwa Ijma’ ya wanazuoni wote wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu Ameamrisha ndani ya Kitabu Chake kwa kusema: “Swali kwa ajili ya Mola wako na Chinja mnyama wa Udh-hiya.” Surat Al-Kawthar, 108, Aya ya pili, isemayo: Swali swala ya Idi na kisha chinja mnyama wa Udh-hiya. (Surat Al-Kawthar, 109:2)

وفي السنَّة كثير؛ ففي البخاري (5564) ومسلم (1966) أنَّه -صلى الله عليه وسلم-: “كان يضحِّي بكبشين أملحين أقرنين”.
Kwa upande wa Sunna, kuna Hadithi nyingi sana, miongoni mwake ni Hadithi iliyopokewa na Bukhari na Muslim, isemayo: “Mtume ﷺ alichinja kondoo wawili, weupe na wenye pembe, kwa ajili ya Udh-hiya.” Bukhari, H.5564, na Muslim, H.1966.
Nyengine:
وفي المسند (8074) أنَّه -صلى الله عليه وسلم- قال: “من كان له سعةٌ ولم يضح، فلا يقربنَّ مصلاَّنَا”.
Hadithi nyengine kutoka kwa Mtume ﷺ ni iliyopokewa na Imam Ahmad, katika Kitabu chake Al-Musnad, ikisema: “Mwenye uwezo na wasaa wa kuchinja mnyama wa Udh-hiya, na papo akaacha kuchinja, basi asisogelee mahali tunaposwali swala ya Idi ya Udh-hiya.” Musnad, H. 8074.
وأجمع العلماء على مشروعيتها، واختلفوا في وجوبها:
Wanazuoni wote wamekubaliana kuhusu Uhalali wa kuthibiti Asasi ya kuchinja mnyama wa Udh-hiya, ila wametofautiana kuhusu kuwa ni Wajibu au Si Wajibu.
فذهب أبو حنيفة: إلى وجوبها، ويروى ذلك عن مالك.
Abu Hanifa amechukua msimamo kuwa kuchinja mnyama wa Udh-hiya ni Wajibu, na imeelezwa, kuwa Imam Malik amechukua msimamo huo huo.
وذهب جمهور العلماء -ومنهم الشَّافعي وأحمد-: إلى أنَّها سنَّةٌ مؤكدة على كلِّ قادرٍ عليها من المسلمين.
Jumhur ya wanazuoni wengi, miongoni mwao Imam Shafi’i na Imam Ahmad, wamechukua msimamo wa kuwa kuchinja mnyama wa Udh-hiya ni Sunna iliyotiliwa mkazo, juu ya kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuchinja mnyama ya Udh-hiya.

والمشهور عن مالك: أنَّها لا تجب على الحجاج اكتفاء بالهدى، واختاره شيخ الإِسلام. وأفضل الأضحية إنْ ضحَّى كاملًا: إبل، ثُمَّ بقر، ثمَّ غنم.
Msimamo mash-huri, kutoka kwa Imam Malik ni kuwa Hakuna Uwajibikaji wa kuchinja mnayama wa Udh-hiya, kwa mahujjaji, inatosheleza kwa Mahujjai, kuchinja mnayama wa kujitolea siku ya Idi, kuanzi Ngamia, akifuatiwa na Ng’ombe na kisha Mbuzi au Kondoo.
Baada ya Utangulizi huo, sasa tusome Hadithi alizotuwekea Imam Ibn Hajar.

والله أعلم

وبالله التوفيق

HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
*Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية

KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO*

JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.

NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *