DARSA YA BM.14.3\2 MLANGO WA KUCHINJA

Hadithi ya Leo, Jumaane, tarehe 13, Rajab, 1446, sawa na tarehe 14, JANUARI, 2025

KUHUSU wa KUCHINJA

SEHEMU YA PILI

1336 -* وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا; { أَنَّ قَوْمًا قَالُوا لِلنَّبِيِّ  إِنَّ قَوْماً يَأْتُونَنَا بِاللَّحْمِ، لَا نَدْرِي أَذُكِرَ اِسْمُ اَللَّهِ عَلَيْهِ أَمْ لَا! فَقَالَ: ” سَمُّوا اَللَّهَ عَلَيْهِ أَنْتُمْ، وَكُلُوهُ” } رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ* .

  1. Imepokewa kutoka kwa ‘Aisha رضي الله عنها akisema: “Watu walimuuliza Mtume : “Tufanye nini ikiwa watu wametuletea nyama na hatujui mnyama yule alipochinjwa kama alitajwa Mwenyezi Mungu au hakutajwa?” Mtume  akasema: “Nyinyi mkipokea nyama hiyo mtajeni Mwenyezi Mungu na kuleni.” Ameipokea Bukhari.

UFAFANUZI

Hadithi hii, inayotufungulia mlango wa Vichinjwa, inatusimulia tukio moja ambapo watu waliosilimu karibuni walimuendea Mtume ﷺ na kumwambia kuwa, huwa wanatembelewa na baadhi ya watu ambao huwatunukia nyama, ila wao hawajuwi kama mnyama husika alipigiwa _Bismillahi_ au hakupigiwa, na hivyo hawajuwi wafanya nini. Mtume ﷺ akawajibu kwa kuwaambia: “Kama nyinyi hamjuwi kuwa mnyama wa nyama hiyo alichinjwa kwa kuigiwa _Bisimillahi_ au la, basi nyini pigeni _Bismillahi_ wakati wa kutaka kula nyama hiyo, na kuleni, itakuwa halali kwenu nyinyi.  

Kigezo cha Sharia kinasema:
القاعدة الشرعية: أنَّه متى وُجِدَ مبيح وحاظر، غُلِّبَ جانب الحظر؛ لحديث: “دع ما يريبك إلى ما لا يريبك” [رواه الترمذي (2518)].

Panapotokea mgongano wa Kisharia katika jambo moja, kama uhalali upande mmoja na uharamu upande wa pili, basi uzito wa Uharamu unapewa kipambele, na njia ya kuondoka uzito huo ni kutenda wewe mwenyewe jambo la kuhalalisha, kama inavyosema Hadithi ya Mtume ﷺ “Acha linalokutia wasi wasi na tenda lisilokuwa na wasi wasi.” Ameipokea Tirmdhi, H. 2518.

Kwa maneno mengine, unapo kuwa na shaka au wasi wasi kuhusu uhalali wa kitu fulani, ambacho huna uhakika kimetengenezwa vipi, kufuatia Sharia za Kiislamu, basi ondoa wasi wasi wako, kwa kufanya lisilokuwa na wasiwasi, kama alivye sema Mtume ﷺ : دع ما يريبك إلى مالا يريبك “Acha linalokkutia wasi wasi na tenda lisilokutia wasiwasi.”

Hivyo, ilimradi aliyekutunukieni kitu kama nyama ni Mwislamu au ni miongoni mwa Ahlul-Kitabu, lakini ukawa na wasi wasi kama pamefuatwa sharia za Kiislamu katika kukiandaa kitu hicho, basi jihalalishieni nyingi wenyewe kwa kutimiza sharia za Kiislamu. Na hii inamaanisha kuwa iwe unaamini kuw kupiga _Bismillahi_ ni Faradhi au si Faradhi, basi anayetaka kula nyama hiyio apige *Bismillahi* yeye mwenyewe. 

YALIYOMO NA YATOKANAYO

  1. Vichinjwa vya watu wa Ahlul-Kitab ni halali kuliwa na kila mfuasi wa mojawapo wa Vitabu vya Mwenyezi Mugu vilivyo teremshwa.
  2. Panapo tokea wasi wasi kuhusu uhalali au uharamu wa kitu fulani, pasi na kujuwa msimamo wa Sharia, basi ni kuachana na linalokutia wasiwasi na kufanya lisilokutia wasi wasi.
  3. Vichinjwa vya Wenye kuabudu moto, kama Majusi, au wenye kuabudu ng’ombe, kama mabaniani, ambao SIi miongoni mwa Ahlul-Kitab, ni haramu kuliwa na Mwislamu.
  4. Nguruwe, na wanyama wote walio haramishwa, kama Kipanga, Chui na Simba, ni haramu kumla, bila ya kujali amechinjwa na nani.

والله أعلم

وبالله التوفيق

HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
*Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية

KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *