Hadithi ya Leo, Jumatatu, tarehe 12, Rajab, 1446, sawa na tarehe 13, JANUARI, 2025
KUHUSU wa KUCHINJA
SEHEMU YA KWANZA
باب الذبائح14.3
مقدمة
UTANGULZI
Neno *الذبح* kwa upande wa Lugha ya Kiarabu, maana yake ni mnyama aliyechinjwa, au atayechinjwa *الذبيحة*, na kwa maana hiyo ni kukatwa mishipa ya shingoni mwa mnyama anayetakiwa kuchinjwa.
وشرعًا: ذبح حيوان مقدور عليه مباح أكله، يعيش في البر غير جراد، بقطع حلقوم ومريء، أو عَقْر ما لم يقدر عليه منه.
Kwa upande wa Sharia, hata hivyo, maana yake ni kuchinjwa mnyama halali, aliyedhibitiwa, na ambaye anaishi nchi kavu (isipokuwa nzige) kwa kukata mishipa yake rohoni, au kwa kumwindwa kisharia.
وحكمه ثابت، بالكتاب، والسنَّة، والإجماع.
Na Asasi ya Kuchinja mnayama halali, imethibiti kupitia Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Sunna ya Mtume ﷺ tokea Sunna ya kauli hadi ya vitendo, na imethibiti vile vile kupitia Ijma’a ya wanazuoni wote.
Kwa upande wa Qur’ani, Mwenyezi Mugu Amesema:
حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنْزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ
Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama,ILA MKIMDIRI KUMCHINGA. .(Al-Maida 5:3)
ومن السنة ما رواه الدارقطني أنَّ النَّبي -صلى الله عليه وسلم- بعث ببديل ابن ورقاء يصيح في فِجَاج مني: “ألا إنَّ الذكاة في الحلق واللبة”.
Kwa upande wa Hadithi, Mtume ﷺ alimtuma Budayl bin Warqa’, aende kwa mahujjaji, mini Mina, kuwatangazia “Juweni kuwa kuchinja ni kukata mishipa ya kooni kwenye kupitia chakula!” Ameipokea Dara-Qutny.
وما جاء في البخاري (5509)، ومسلم (1968) من حديث رافع بن خديج قال: كنا مع رسول الله -صلى الله عليه وسلم- في سفر، فندَّ بعير من إبل القوم، ولم يكن معنا خيل، فرماه رجل بسهم، فحبسه، فقال -صلى الله عليه وسلم-: “إنَّ لهذه البهائم أوابد كأوابد الوحش، فما فعل منها هذا، فافعلوا به هكذا”.
Hadithi nyengine imepokewa na Bukhari na Muslim, kutoka kwa Rafi’ bin Khudayj akisema: “Tulikiwa safarini na Mtume !ﷺ Ikatokea ngamia mmoja kutokana na ngami wa jamaa wasafiri, akakimbia, na hapakuwepo mtu yeyote mwenye farasi wa kumkimbilia kumkamata. Basi mtu mmoja akamdunga ngamia huyo kwa mshare wake, akaanguka.” Mtume ﷺ akasema: “Juweni kuwa mifugo hii, ni viumbe kama viumbe mwitu; hivyo huyu aliyemdunga kwa mshare wake amemuwinda, na nyingi mnapokuwa hamna njia nyengine ya kumkamata mnyama wenu aliyekimbia, basi mdungeni kwa mishare yenu.”
Wanazuoni wakazidi kufafanua kwa kusema:
“أجمعوا على أنَّ المرء إذا ذبح ما يجوز ذبحه، وسمَّى الله، وقطع الحلقوم والودجين، وأسَالَ الدَّمَ، فإنَّ الشاة مباح أكلها”.
“Wanazuoni wote wamekubaliana kuwa mchinjaji akichinga mnyama anayejuzu kujichinwa, akapiga Bismillahi, na akakata mishipa mwili mikuu ya damu rohoni, damu ikachururika, basi ni halali kula mnyama huyo.”
وأجمعوا على أنَّ ما أبيح أكله لا يباح إلاَّ بالذكاة، كما أجمعوا على أنَّ الميتة حرام.
Na wamekubalina, kwa kauli moja, kuhusu wanyama wa nchi kavu, kuwa haijuzu kumla isipokuwa baada ya kuchinjwa, kama walivyo kubaliana kuwa nyamafu ni haramu kuliwa.
وصفة الذبح، والنحر، والعقر: واحدة في جميع الشرائع السماوية من حيث وجوب إسالة الدم، ومن حيث وجوب إجراء عملية الذبح أو النحر في الموضع الَّذي حدَّده الشرع في جسم المذبوح أو المنحور.
Na kuchinha mnyama halali, ni kukata mishipa ya rohoni, au kujeruhi kichinjwa, kwa mujibu wa Sharia zote za Vitabu vilivyoteremshwa kutoka Mbinguni, ambapo ni wajibu wa kutumia ala ya kuchururisha damu, kwa kujeruhi mwili wa mnyama aliyechinjwa.
ولولا توحد الشرائع السماوية في أصول الذكاة، لما أحل الله للمسلمين ذبائح أهل الكتاب، كما أحل ذبائح المسلمين.
Na pasi na kuwepo Sharia za kuchinja ndani ya Vitabu vvyote vilivyo teremshwa kutoka Mbinguni, wasingeruhusiwa Waialamu kula wanyama waliochinjwa na Ahlul-Kitab, kupitia shaia hizo hizo walioteremshiwa Waislamu, ndani ya Qur’ani.
ويشترط للذكاة ذبحًا أو نحرًا أربعة شروط:
Kuna Masharti mane kuhalalisha kichinjwa halali kuliwa.
أحدها: أهلية الذابح، أو النَّاحر، أو العاقر، وهو أنْ يكون عاقلاً، قاصدًا التذكية، فلا تحل ذكاة مجنون، وسكران، وطفلٍ دون التمييز؛ لأنَّه لا قصد لهم.
SHARTI LA KWANZA: Linamnhusu mchinjaji, au muwindaji, ambaye anapaswa awe mwenye akili timamu, aliyekusudia kuchinja. Na kwa maana hiyo, haijuzu kula mnyama aliyechinjwa na mwenda wazimu, au mlevi, au mtoto mdogo chini ya umri wa Tamyiiz, kwa sababu wote hao hawna mamlaka ya kukusudia kuchinja.
الثاني: الآلة: وهو أنْ يذبح بآلة محدَّدة تقطع، أو تخرق بحدها، لا بثقلها سواءٌ من حديد، أو حجر، أو خشب، أو غيرها، غير عظم وظفر؛ فلا تحل الذبيحة بهما.
SHARTI LA PILI: Linahusu ala iliyotumiwa; yaani lazima patumiwe ala yenye makali, yenye uwezo wa kukata mishipa kooni, au kuchoma mwilini kwa ncha na makli yake; siyo kumuua kwa kumpiga mtarimbo wa chuma, au kumpiga jiwe, au kumpiga gongo, au kumpiga kitu chochote chengine, kama kumpiga kwa pembe, au kwa fupa kubwa. Mnyama yoyote ataye uliwa kwa kupigwa kupitia vitu kama hivyo, haijuzu kumla.
الثالث: أنْ يقطع الحلقوم: وهو مجرى النفس، والمريء: وهو مجرى الطعام والشراب، ولا يشترط قطع الودجين، بل يستحب، والودجان: عرقان بجانب الرقبة.
SHARTI LA TATU: Wajibu wa kukata mishipa ya damu shingoni na rohoni, panapo pita chakula na kinywaji. Siyo lazima kukata shingo nzima, bali koo na mishipa ya damu kooni tu. Bali Sunna ni kukata mishipa ya sehemu hiyo tu, shingoni.
الرَّابع: التسمية عند حركة يده بالذبح بقوله “باسم الله”، ولا يجزئ غيرها، ووجوبها إذا ذكرها، ويسقط مع السهو، وهو مذهب الجمهور.
SHARTI LA NNE: Kupiga Bismillahi wakati wa kuanza kuchinja, kwa kusema Bismillahi. Na haijuzu kutumia maneno mengine, isipokuwa Bismillahi. Akisahau kupiga Bismillahi hapana junaha. Huo ndio msimamo wa Wanazuoni wote wa Kiislamu.
Baada ya Utangulizi huo, sasa tusome Hadithi alizotuwekea Imam Ibn Hajar katika Mlango huu wa Vichinjwa.
والله أعلم
وبالله التوفيق
HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!
IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
*Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *
من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية
KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO
JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA
UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA
NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, na kuweka kwenye FB yako, WhatsApp, na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com
Leave a Reply