DARSA YA BM.13\13 KUHUSU KITABU CHA VYAKULA

Hadithi ya Leo, Jumatatu, tarehe 5, Rajab, 1446, sawa na tarehe 6, JANUARI, 2025

KUHUSU VYAKULA

SEHEMU YA KUMI NA TATU

1331 – وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عُثْمَانَ اَلْقُرَشِيُّ رضي الله عنه { أَنَّ طَبِيباً سَأَلَ رَسُولَ اَللَّهِ  عَنْ اَلضِّفْدَعِ يَجْعَلُهَا فِي دَوَاءٍ، فَنَهَى عَنْ قَتْلِهَا }أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ.

  1. Imepokewa kutoka kwa Abdulrahman bin Uthman Al Kurashiy رضي الله عنه akisema: “Daktari mmoja alimuuliza Mtume  kuhusu chura ambaye yeye humuua akamuingiza katika dawa za matibabu. Mtume  akamkataza kuua chura.” Ameipokea Ahmad na ameisahihisha Al Hakim.

UFAFANUZI

Hadithi hii, inayotufungia mlago huu wa VYAKULA, inatufundisha kuwa Mtume ﷺ alikataza kuuliwa Chura, baada ya kuulizwa na Daktari mmoja, uhalali wa kumtumia Chura katika matibabu yake anayoyatoa kwa wagonjwa wake, na hivyo kutibu watu . Mtume ﷺ akakataza kimuua Chura. Ila haikuelezewa hutumiwa kutibu maradhi gani, wala aina ya chura husika. Maana kuna vyuura wa aina nyingi sana, wengine wana sumu; hivyo si kila chura. Ila chunguzi za kitabibu zilizofanywa na Taasisi mbali mbali , miongoni mwake wataalamu wa kitengo cha Matibabu, kutoka vyuo Vikuu mbali mbali, khasa Chuo Kikuu cha Queens  cha Belgast, Uiingereza, kilichotunukiwa Tunzo kuu ya Utafiti wake, na Chuo Kikuu cha Panama, Chup Kiku chaAustralia na kwengineko, zimethibitisha kuwa ngozi ya chura ina udenda wa vimeleya mahasusi ambavuo vinasaidia kutibu zaidi ya maradhi 70. Ni chura wa aina ya CANE TOAD na aina nyengine ya BUFONIDAE mwenye ngozi nene, mbaye ni vigumu sana kumtambua isipokuwa kama wewe ni bingwa wa tiba mbali mbali. Hivyo, usirukie kula chura kwa kuamini kuwa ni dawa. Na kwa vile Mtume ﷺ ameharamisha kumuua chura, basi ni hramu kula chura katika Uwislamu. Na kama HAIJUZU kumuua, basi haijuzu kumla vile vile. 

أخبار الطبي.
TAARIFA ZA KITABIBU

*اكتشف علماء إيرلنديون بالصدفه ان افرازات الضفدع يمكن استخدامها في علاج اكثر من سبعين مرضا” من ضمنها السرطان والسكري *!
Wataalamu wa Ireland ya Kaskazini Uiingereza, wamevumbua, kwa kusadifu tu, kuwa udenda wa baadhi ya Vyura, una vimelea, vinavyo toka kwenye ngozi yake, vinaweza kutumiwa kutibu zaidi ya maradhi 70 kwenye mwili wa mwanadamu, miongoni mwake ni maradhi ya Saratani na Kisukari.

وقد وجد العلماء في جامعه كوين في ايرلندا خلال ابحاثهم على نوع من الضفادع الذي ينتشر في امريكا الجنوبيه وأفريقيا وتستخدم مواد تفرزها على الجلد كوسيله دفاعيه حال تعرضها الى الحيوانات المفترسه الى وجود بروتين من نوع خاص في هذه الافرازات له القدره على التحكم في تصنيع اوعيه دمويه جديده من خلال اما تكوين اوعيه جديده او تثبيط نموها

Madaktari bingwa wa Kitivo cha MATIBABU kutoka Cuo Kikuu cha Queens nchini ya Irlend ya kusini, kupitia chunguzi zao mbali mbali za kawaida, wamegundua kuwa kuna aina ya Vyura vilivyo zagaa Amerika ya Kusini na Afrika, ambvyo vina vimeleya mahasusi kwenye ngozi zao, ambavyo vyura hao huvitumia kujilinda na mashambulizi yoyote kutoka kwa wanyama wengine wanaotaka kuwashambulia na kuwala. Vimelea hivyo huwafukuza na kuwadhuru wanyama mwitu hao wanaotaka kuwala vyura hao. Matabibu hao wamesema wamegundua kuwa vimelea hiyo vinaweza kutumiwa katika kutengeneza madawa mbali mbali yenye kuweza kutibu matatizo kwenye damu mwilini, ama kwa kutengeneza dawa mpya, au kuimarisha dawa zilizopo za zamani kutibu magonjwa ya damu mwilini.

ما يجدر ذكره هنا هو أن الخلايا السرطانيه تنمو الى حجم معين في المراحل المرضيه الاولى قبل ان تبدأ لاحقا” في تكوين اوعيه دمويه خاصه بها تساعد على استمراريه بقائها وانتشارها في الجسم وبإستخدام هذا البروتين قد يتمكن العلماء من السيطره على المرض من خلال قتل الخلايا السرطانيه اضافه الى منع تكوين المزيد منها وبالتالي الحد من انتشار المرض وتفشيه في الجسم

Jambo lilio muhimu kulikumbusha hapa ni kuwa vidudu vya Saratani hukua ndani ya damu, kupitia awamu mbali mbali, kabla ya kufikia kiwango cha mwisho cha kusababisha maradhi ya Saratani ndani ya damu ya mtu husika, na kusambaa sehemu nyengine za mwili wa mwanadamu. Ila inawezekana sana kudhibiti kukua kwa vimelea hivyo, katika awamu zake, tokea awamu ya mwanzo, kuvizuwia kukua, hadi kuviua vimeleya vilivyo vikifikia mwisho, na hivyo kutibu mwanzo wa maradhi ya saratani, hadi kuzuwia kuzuka maradhi ya saratani na kisukari mwilini.

وفقا للبروفيسور شو، فإن العلماء وشركات الأدوية في مختلف أنحاء العالم، على الرغم من انفاقها ما بين 4 إلى 5 مليارات دولار على الأبحاث إلا أنهم لم يتوصلوا حتى الآن إلى دواء التي يمكن أن يتحكم ويراقب نمو الأوعية الدموية.

Kufuatia Profesa Shaw Kiongozi wa Jopo la watafiti hao, “Wanazuoni na Mashirika mbali mbali ya madawa Duniani, licha ya kutumia mabilioni kwa mabilioni, kila mwaka, baina ya Dola bilioni 4 hadi 5, katika kuendeleza tafiti, ukweli usiopingika ni kuwa hadi hii leo, bado hakujapatikana suluhu ya kudhibiti na kuzuwia ukuaji wa vemilea vya maradhi mbali mbali ndani ya damu mwilini.

وأضاف شو “إن الهدف من عملنا في جامعة كوينز هو اطلاق طاقات الطبيعة وهناك مثل على ذلك وهو الافرازات التي تم العثور عليها من في جلود الضفادع لتخفيف معاناة البشر.

Na akaongeza kusema, Profesa Shaw: “Lengo la kazi zetu kwenye Chuo kikuu cha Qweens, ni kuachia nguvu za kimaumbile zifaye kazi zake, na kuna mifano mingi ya kweza kufikia lengo hilo, nayo ni kuengeza juhudi na jitihada kwene vimelea vilivyo kwisha tambuliwa, kutokana na vimelea vya ngozi ya Chura, ili kupunguza na kukomesha maumivu ya wanaadamu kwenye damu zao.

وقال أيضا ” نحن مقتنعون تماما بأن الطبيعة تحمل حلولا لكثير من مشاكلنا الحقيقية ونحن بحاجة فقط لطرح الأسئلة الصحيحة للعثورعليها”.

Na akamalizia kwa kusema: “Sisi tumetosheka, kikamilifu, kuwa TABIA-MAUMBILE iana majibu mengi sana yanyohusiana na matatizo yetu halisi, na hivyo tunawajibika kuzusha na kujadili masuala mabali mbali ili tuishie kupata majibu sahihi ya matatizo yetu.”

YALIYOMO NA YATOKANAYO

  1. Haramu kuua Chura, pasi na sababu yoyote ya msingi; hasa vyura vinavyo tumiwa na matabibu wa dawa za miti-shamba, kutibu maradhi mbali mbali.
  2. Kilicho haramishwa kuuliwa ni haramu kukila, vile vile; hivyo ni haramu kula mnyama ya chura katika Uwislamu.
  3. Kuna aina nyingi sana za Vuura, wengine wana sumu, hivyo si suala la kila chura, wala si suala la kujiamulia kutokana na mawazo binafsi, bali ni suala la kusomea na uzoefu na kulifanya tafiti mbali mbali, kutoka kwa wataalamu mahasusi wa kufanya tafiti.
  4. Kiumbe chochote chenye sumu, kama nyoka, tandu, nge na kadhalika ni haramu kuliwa; na inajuzu kuviua ikibainika hatari yao kwa wahusika.
  5. “Mwenyezi Mungu Ameumba kila gonjwa na kila gonjwa Ameliumbia dawa yake; hivyo ikisibu dawa itatibu gonjwa husika,” Amesema Mtume ﷺ.
  6. Miujiza ya Mtume ﷺ kuhusu upatikanaji wa dawa ya Saratani na Kisukari kutokana na vimelea vya ngozi ya baadhi ya Chura.

والله أعلم

وبالله التوفيق

HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
*Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية

KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
kcwajawema@gmail.com

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *