Category: Vitabu

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*

    TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*

    مختصر صحيح البخاري للزبيدي
    رتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقات
    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسيني
    خادم السنة النبوية
    *MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.
    *Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *
    Sayyid Abdulqadir Shareef
    MTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME
    *Leo Siku ya Jumatano, tarehe 30, Saffar, 1446, H., sawa na tarehe 04, Septemba, 2024. *
    (9)
    كِتَاب مَوَاقِيتِ الصَّلاَةِ
    KITABU CHA NYAKATI ZA SWALA

    363- وعَنْهَا رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: رَكْعَتَانِ، لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَدَعُهُمَا، سِرًّا وَلاَ عَلاَنِيَةً: رَكْعَتَانِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَرَكْعَتَانِ بَعْدَ الْعَصْرِ. [رواه البخاري: 592].

    1. Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها akisema: “Rakaa mbili Mtume ﷺ hakuwa anaziacha si kisiri siri wala waziwazi nazo ni rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri na rakaa mbili baada ya laasiri.” [Bukhari:592]

    UFAFANUZI

    Mtume ﷺ alikuwa anaswali rakaa mbili laasiri lakini hii ilikuwa khususwia yake, ndiyo maana alikuwa anaziswali peke yake nyumbani lakini zimekatwaza.

    25- بَاب: الأَذَانِ بَعْدَ ذَهَابِ الْوَقْتِ

    1. Mlango: Kuhusu kuadhini baada ya wakati wa swala husika kupita

    364- عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: سِرْنَا مَعَ النَّبِيِّ ﷺ لَيْلَةً، فَقَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ: لَوْ عَرَّسْتَ بِنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: «أَخَافُ أَنْ تَنَامُوا عَنْ الصَّلاَةِ». قَالَ بِلاَلٌ: أَنَا أُوقِظُكُمْ. فَاضْطَجَعُوا، وَأَسْنَدَ بِلاَلٌ ظَهْرَهُ إِلَى رَاحِلَتِهِ، فَغَلَبَتْهُ عَيْنَاهُ فَنَامَ، فَاسْتَيْقَظَ النَّبِيُّ ﷺ وَقَدْ طَلَعَ حَاجِبُ الشَّمْسِ، فَقَالَ: «يَا بِلاَلُ! أَيْنَ مَا قُلْتَ؟» قَالَ: مَا أُلْقِيَتْ عَلَيَّ نَوْمَةٌ مِثْلُهَا قَطُّ. قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ قَبَضَ أَرْوَاحَكُمْ حِينَ شَاءَ، وَرَدَّهَا عَلَيْكُمْ حِينَ شَاءَ، يَا بِلاَلُ، قُمْ فَأَذِّنْ بِالنَّاسِ بِالصَّلاَةِ» فَتَوَضَّأَ، فَلَمَّا ارْتَفَعَتْ الشَّمْسُ وَابْيَاضَّتْ،( ) قَامَ فَصَلَّى. [رواه البخاري: 595].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah رضي الله عنه akisema: “Tulisafiri usiku mmoja na mtume ﷺ Tulivyofika njiani baadhi ya watu wakasema: “Lau tungesimama hapa njiani tukapiga kambi” Mtume ﷺ akawaambia: “Nachelea msije mkapitiwa na usingizi” Bilal alivyosikia maneno hayo akasema: “Mimi nit akuamsheni jionyoosheni tu” na Bilal akakaa na kuegemea masoji au mizingo ya mnyama wake lakini akapitiwa na usingizi. Mtu wa mwanzo kuzindukana alikuwa mtume ﷺ na wakati huo mwangaza wa jua ushachomoza, mtume ﷺ akasema: “Bilal yako wapi maneno yako uliyoyasema?” Bila akasema: “Sijapata kupitiwa na usingizi kama nilivyopitiwa jana usiku” Mtume ﷺ akasema: “Mwenyezi Mungu anazichukua roho zenu wkaati wowote anaotaka na anakurudishieni roho zenu wakati wowote anaotaka ewe Bilal, haya nasi simama uadhini” Bilal akaondoka akaenda akatawadha na jua lilikuwa limeshachomoza limeinuka juu kidogo ndiyo akaadhini na mtume ﷺ akasimama kuswali.” [Bukhari:595]

    26- بَاب: مَنْ صَلَّى بِالنَّاسِ جَمَاعَةً بَعْدَ ذَهَابِ الْوَقْتِ

    1. Mlango: Kuswalisha jamaa baada ya kupita wakati wa swala husika

    365- عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رضي الله عنه جَاءَ يَوْمَ الْخَنْدَقِ بَعْدَ مَا غَرَبَتْ الشَّمْسُ، فَجَعَلَ يَسُبُّ كُفَّارَ قُرَيْشٍ، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! مَا كِدْتُ أُصَلِّي الْعَصْرَ حَتَّى كَادَتْ الشَّمْسُ تَغْرُبُ، قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «وَاللَّهِ مَا صَلَّيْتُهَا» فَقُمْنَا إِلَى بُطْحَانَ فَتَوَضَّأَ لِلصَّلاَةِ، وَتَوَضَّأْنَا لَهَا، فَصَلَّى الْعَصْرَ بَعْدَ مَا غَرَبَتْ الشَّمْسُ، ثُمَّ صَلَّى بَعْدَهَا الْمَغْرِبَ. [رواه البخاري: 596].

    1. Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdullah رضي الله عنهما akisema: “Umar bin Khattwab رضي الله عنه alifika kwenye vita vya Khandaq baada ya jua kuchwa, akawa anawashambulia na kuwatukana makafiri wa Kiqureshi akisema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu sijapata wasaa wa kuswali laasiri mpaka jua limekuchwa” Mtume ﷺ akasema: “Hata mimi sijaiswali” kwa hiyo wote tukasimama kwenda katika bonde la maji Mtume ﷺ akatawadha na sisi pia tukatawadha akatuswalisha swala ya laasiri baada ya kuwa jua limeshakuchwa kisha akaswali magharibi baada yake.” [Bukhari:596]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*

  • BM.14.11.\3.6 MLANGO KUHUSU ADHABU YA WIZI

    BM.14.11.\3.6 MLANGO KUHUSU ADHABU YA WIZI

    Hadithi ya Leo, Jumaane, tarehe 29, Mfungo Tano, 1446, H. sawa na tarehe 03, Ogasti, 2024

    SEHEMU YA SITA

    KUHUSU ADHABU YA WIZI

    1236* وَعَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ؛ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ  قَالَ: لَا يَغْرَمُ السَّارِقُ إِذَا أُقِيمَ عَلَيْهِ الْحَدُّ. رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَبَيَّنَ أَنَّهُ مُنْقَطِعٌ. وَقَالَ أَبُو حَاتِمٍ: هُوَ مُنْكَرٌ*.

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdulrahman bin Awf **رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Halipishwi mwizi fidia ya kitu alichokiiba, baada ya kupitishiwa hukumu ya kukatwa mkono.” Ameipokea Nasai ila amebainisha kuwa Riwaya yake haikufika kwa Mtume . Abu Hakim anasema: Riwaya hii ni Munkari.

    UFAFANUZI

    Haidithi hii, pamoja na kwamba maana yake ni sahihi kuwa mwizi akithibitika kuwa ameiba na akakatwa mkono wake, haijuzu kumtaka alipe fidia ya kitu alichoiba, ila Isnadi yake ni pungufu, haijakamilika, maana mpokezi mmoja aitwaye Al-Miswar bin Ibrahim bin Abdurrahman bin Awf, hajakutana na Babu yake Abdurrahman bin Awf, lakini katika Hadithi amesema kuwa ameipokea kutoka kwa Abdurrahman bin Awf, ambaye ni babu yake. Hata Abu Hatim ameipokea hivyo hivyo, na kuishia kusema kuwa Hadithi hiyo ni Munkari; yaani haiwezi kukubaliwa kuwa ni maneno yametoka kwa Mtume ﷺ ; maana mtu yeyote akithibitika kutenda hatia na akatiwa adhabu ya Mwenyezi Mungu, hawezi kutakiwa alipe fidia ya kitu alichokiiba, wala kutakiwa arudishe alichokiiba, baada ya kutiwa adabu ya Mwenyezi Mungu. Hivyo, mafunzo yake ni kweli, lakini matamshi yake kunasibishwa kwa Mtume ﷺ siyo kweli.

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Mwizi aliyeiba kitu cha mtu mwengine, ana haki mbili:
      a) Haki mahasusi, nayo ni kitu alichokiiba iwapo kipo; au kutozwa fidia iwapo alichokiiba hakipo, au kutozwa thamani ya alichokiiba, iwapo alichokiiba kimepotea au kimeharibika.
      b) Haki ya Jamii ya Waislamu, juu yake, na hiyo ndiyo Haki ya Mwenyezi Mungu, ya kukatwa mkono baada ya kukamilika masharti na nguzo za kukatwa mkono, au kuaziriwa iwapo hayajakamilika masharti ya kukatwa mkono.
    2. Iwapo kitu alichokiiba kipo salama, kama kilivyokuwa kabla ya kuibiwa, basi wanazuoni wa Kiislamu wameafikiana kuwa ni wajibu kurudishwa kwa mmiliki wa kitu hicho, na hakuna adhabu ya mwizi aliyekiiba kukatwa mkono, bali atatiwa adhabu ya kuaziriwa na kufedheheshwa hadharani.
    3. Haki ya Mwenyezi Mungu, ikithibitika hatia, lazima ipitishwe, ambayo ama ni Adhabu kubwa iliyowekwa juu ya aliyetenda Hatia, au adhabu ndogo, nayo ni kufedheheshwa hadharani, ili ajulikane kuwa ni mtu aliyewahi kuvuka mpaka ya Mwenyezi Mungu, makusudi.
    4. Adhabu za Mwenyezi Mungu kwa Hatia mbali mbali, hazikuwekwa kuwa ni ndiyo lengo lenuyewe, bali ni Onyo na Tahadhari kwa wengine, wasitende hatia husika; hivyo ni wajibu wa kukamilisha lengo hilo la kuzuwia wengine wasitende hatia hiyo.
    5. Haki ya Mwenyezi Mungu haiepukikji baada ya kufikishwa aliyetenda Hatia ya Adhabu, akishafikishwa mbele ya Mwenye mamlaka rasmi ya kupitisha Sharia za Mwenyezi Mungu.
    6. Hakuna junaha kwa aliyetenda hatia ya Adhabu ya Mwenyezi Mungu, kutopitishwa Adhabu ya Mwenuyezi Mungu, KABLA ya kufikishwa mbele ya Mwenye Mamlaka ya kusimamia Sharia, kwa kusamehewa na aliyedhulumiwa au aliye dhuriwa na mtenda hatia.
    7. Inajuzu kwa mtu aliyedhulumiwa au kudhuriwa, kumsamehe aliyemdhulumu au kumdhuru, kama alivyosema Mtume ﷺ : “لا يحل مال امرىء مسلم، إلاَّ بطيبة من نفسه” Haimjuzii mtu kujihalalishia mali ya mtu Mwislamu mwengine, isipokuwa akiridhia kumhalalishia.”

    والله أعلم

    وبالله التوفيق