Category: Vitabu

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Alkhamis, tarehe 16, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 19, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    31- بَاب: مَنْ صَلَّى بِالنَّاسِ وَهُوَ لَا يُرِيدُ إِلَّا أَنْ يُعَلِّمَهُمْ صَلَاةَ النَّبِيِّ ﷺ وَسُنَّتَهُ

    1. Mlango: Kuhusu mtu anayewaswalisha watu na lengo lake lilikuwa ni kutaka kuwafundisha tu swala ya mtume ﷺ na sunna zake

    405- عَنْ مَالِكُ بْنُ الْحُوَيْرِثِ رضي الله عنه قَالَ: إِنِّي لأصَلِّي بِكُمْ وَمَا أُرِيدُ الصَّلاَةَ، أُصَلِّي كَيْفَ رَأَيْتُ النَّبِيَّ ﷺ يُصَلِّي. [رواه البخاري: 677].

    1. Imepokewa kutoka kwa Malik bin Huwayrith رضي الله عنه akisema: “Mimi ninakuswalisheni na lengo langu siyo mimi kuswali lakini nakuswalisheni nikuonyesheni vipi nimemuona Mtume ﷺ anaswali.” [Bukhari: 677]

    32- بَاب: أَهْلُ الْعِلْمِ وَالْفَضْلِ أَحَقُّ بِالْإِمَامَةِ

    1. Mlango: Wanawazuoni na wenye fadhila wanastahiki zaidi kuongoza swala

    406- عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا حَدِيثُ: «مُرُوا أَبَا بَكْرٍ يُصَلِّي بِالنَّاسِ»تَقَدَّمَ،( ) وَفِي هذِهِ الرِّوايَةِ قَالَتْ: قُلْتُ: إِنَّ أَبَا بَكْرٍ إِذَا قَامَ فِي مَقَامِكَ، لَمْ يُسْمِعْ النَّاسَ مِنْ الْبُكَاءِ، فَمُرْ عُمَرَ فَلْيُصَلِّ لِلنَّاسِ. فَقَالَتْ عَائِشَةُ: فَقُلْتُ لِحَفْصَةَ: قُولِي لَهُ: إِنَّ أَبَا بَكْرٍ إِذَا قَامَ فِي مَقَامِكَ، لَمْ يُسْمِعْ النَّاسَ مِنْ الْبُكَاءِ، فَمُرْ عُمَرَ فَلْيُصَلِّ لِلنَّاسِ، فَفَعَلَتْ حَفْصَةُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «مَهْ، إِنَّكُنَّ لاَنْتُنَّ صَوَاحِبُ يُوسُفَ، مُرُوا أَبَا بَكْرٍ فَلْيُصَلِّ لِلنَّاسِ» فَقَالَتْ حَفْصَةُ لِعَائِشَةَ: مَا كُنْتُ لِأُصِيبَ مِنْكِ خَيْرًا. [رواه البخاري: 679].

    1. Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها na hii ni hadithi ndefu ambayo Mtume ﷺ anaripotiwa kusema: “Muamrisheni Abu Bakr akawaswalishe watu” imeshatangulia. Katika riwaya hii ya hapa anasema Aisha رضي الله عنها : “Nikamwambia Mtume ﷺ : Kama Abu Bakr atakuqaimu kuswalisha basi watu hawatomsikia kitu kutokana na kulia kwake bora umuamrishe Umar awaswalishe watu” anasema Aishaرضي الله عنها : Nikamnong’oneza Hafswa رضي الله عنها amwambie mtume ﷺ maneno hayo hayo kwamba Abu Bakr akikuqaimu katika swala watu hawataweza kumsikia kitu kutokana na kulia kwake kwa hivyo Muamrishe Umar awaswalishe watu, Hafswa akafanya akaenda kumwambia mtume ﷺ , Mtume ﷺ alipoambiwa maneno hayo ambayo keshayasikia kutoka kwa Aisha alimuambia Hafswa: “Nyamaza! Acha nyinyi mmekuwa kama wanawake wa Nabii Yusuf, nimesema muamrisheni Abu Bakr awaswalishe watu” anasema Hafswa: akamrudia Aisha na kumwambia: “Sijapata jambo lolote kutoka kwako wewe lenye khayr.” [Bukhari: 679]

    407- عَنْ أَنَسُ رضي الله عنه : أَنَّ أَبَا بَكْرٍ كَانَ يُصَلِّي لَهُمْ فِي وَجَعِ النَّبِيِّ ﷺ الَّذِي تُوُفِّيَ فِيهِ، حَتَّى إِذَا كَانَ يَوْمُ الِإثْنَيْنِ، وَهُمْ صُفُوفٌ فِي الصَّلاَةِ، فَكَشَفَ النَّبِيُّ ﷺ سِتْرَ الْحُجْرَةِ، يَنْظُرُ إِلَيْنَا وَهُوَ قَائِمٌ، كَأَنَّ وَجْهَهُ وَرَقَةُ مُصْحَفٍ، ثُمَّ تَبَسَّمَ يَضْحَكُ، فَهَمَمْنَا أَنْ نَفْتَتِنَ مِنْ الْفَرَحِ بِرُؤْيَةِ النَّبِيِّ ﷺ ، فَنَكَصَ أَبُو بَكْرٍ عَلَى عَقِبَيْهِ لِيَصِلَ الصَّفَّ، وَظَنَّ أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ خَارِجٌ إِلَى الصَّلاَةِ، فَأَشَارَ إِلَيْنَا النَّبِيُّ ﷺ أَنْ أَتِمُّوا صَلاَتَكُمْ وَأَرْخَى السِّتْرَ، فَتُوُفِّيَ مِنْ يَوْمِهِ. [رواه البخاري: 680].

    1. Imepokewa kutoka kwa Anas رضي الله عنه akisema: “Pale Abu Bakr alipokuwa anawaswalisha watu kutokana na maradhi aliyokuwa nayo mtume ﷺ ambayo ndiyo yaliyompelekea mpaka akafariki, ilipofika siku ya Jumatatu na watu wamejipanga swafu msikitini wanaswali Mtume ﷺ alifunhua pazia kutoka chumbani kwake akaangalia msikitini akatuangalia msikiti na yeye amesimama chumbani kwake, uso wake una ng’ara utafikiri karatasi ya Mus’haf kisha akatabasamu na kucheka, tukataka kufitinika kutoka na furaha ya kumuona mtume ﷺ , Abu Bakr akarudi kinyume nyuma ili akajiunge na swafu alidhani kwamba mtume ﷺ atatoka kuja kuswalisha lakini mtume ﷺ akaashiria kwa mkono wake kwetu sisi kwamba timizeni swala kisha akalifunga pazia lake na siku hiyo ndiyo aliyofariki.” [Bukhari: 680]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumatano, tarehe 14, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 18, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    27- بَاب: حَدِّ الْمَرِيضِ أَنْ يَشْهَدَ الْجَمَاعَةَ

    1. Mlango: Mgonjwa kutohudhuria jamaa

    399- عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: لَمَّا مَرِضَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ مَرَضَهُ الَّذِي مَاتَ فِيهِ، فَحَضَرَتْ الصَّلاَةُ، فَأُذِّنَ، فَقَالَ: «مُرُوا أَبَا بَكْرٍ فَلْيُصَلِّ بِالنَّاسِ» فَقِيلَ لَهُ: إِنَّ أَبَا بَكْرٍ رَجُلٌ أَسِيفٌ،( ) إِذَا قَامَ فِي مَقَامِكَ لَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يُصَلِّيَ بِالنَّاسِ، وَأَعَادَ فَأَعَادُوا لَهُ، فَأَعَادَ الثَّالِثَةَ فَقَالَ: «إِنَّكُنَّ صَوَاحِبُ يُوسُفَ، مُرُوا أَبَا بَكْرٍ فَلْيُصَلِّ بِالنَّاسِ» فَخَرَجَ أَبُو بَكْرٍ فَصَلَّى، فَوَجَدَ النَّبِيُّ ﷺ مِنْ نَفْسِهِ خِفَّةً، فَخَرَجَ يُهَادَى( )بَيْنَ رَجُلَيْنِ، كَأَنِّي أَنْظُرُ رِجْلَيْهِ يَخُطَّانِ مِنْ الْوَجَعِ، فَأَرَادَ أَبُو بَكْرٍ أَنْ يَتَأَخَّرَ، فَأَوْمَأَ إِلَيْهِ النَّبِيُّ ﷺ أَنْ مَكَانَكَ، ثُمَّ أُتِيَ بِهِ حَتَّى جَلَسَ إِلَى جَنْبِهِ. وَكَانَ النَّبِيُّ ﷺ يُصَلِّي، وَأَبُو بَكْرٍ يُصَلِّي بِصَلاَتِهِ، وَالنَّاسُ يُصَلُّونَ بِصَلاَةِ أَبِي بَكْرٍ رضي الله عنه.
    وَفِي رِوايَةٍ: جَلَسَ عَنْ يَسَارِ أَبِي بَكْرٍ، فَكَانَ أَبُو بَكْرٍ يُصَلِّي قَائِمًا.( )[رواه البخاري: 664].

    1. Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها akisema: “Pale Mtume ﷺ alipoumwa katika maradhi ambayo alifariki na swala ikawadia pakaadhiniwa, mtume ﷺ akasema: “Muamrisheni Abu Bakr aswalishe watu” watu wakamwambia: “Abu Bakr ni mtu mwenye moyo wa upole sana akisimama mahala pako hatoweza kuwaswalisha watu na ataanza kulia” Mtume ﷺ akawaambia: “Muamrisheni Abu Bakr aswalishe” wakamwambia tena maneno hayohayo, Mtume ﷺ akawaambia wakeze: “Nyinyi ni mfano wa wale watu wa Nabii Yusuf, nimekwambieni muamrisheni Abu Bakr awaswalishe watu” basi Abu Bakr akatoka kuwaswalisha watu. Mtume ﷺ akapata unafuu kidogo akatoka akiwa amekamata mabega ya watu wawili ilhali mpaka sasa hivi ninaona miguu yake inagusa kidogo tu ardhi kutokana na maumivu aliyokuwa nayo, alipofika pale nyuma ya Abu Bakr, Abu Bakr akataka kurudi nyuma ampishe mtume ﷺ aswalishe lakini mtume ﷺ akampa ishara kwamba aendelee kuswalisha hapohapo alipo, basi mtume ﷺ akapelekwa mpaka akakaa kitako ubavuni mwa Abu Bakr na mtume akawa anaswali na Abu Bakr anafuata swala ya mtume ﷺ na watu wanaswali kumfuata Abu Bakr katika swala yake.”

    Riwaya nyengine inasema: “Alikaa kushotoni mwa Abu Bakr a Abu Bakr akawa anawaswalisha watu akiwa amesimama.” [Bukhari: 664]

    400- وعَنْها رَضِيَ اللهُ عَنْهَا فِي رِوَايةٍ: قالت: لَمَّا ثَقُلَ النَّبِيُّ ﷺ ، وَاشْتَدَّ وَجَعُهُ، اسْتَأْذَنَ أَزْوَاجَهُ أَنْ يُمَرَّضَ فِي بَيْتِي، فَأَذِنَّ لَهُ. وَبَاقِي الحَدِيثِ تَقَدَّمَ آنِفًا.( )[رواه البخاري: 665].

    1. Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها akisema: “Pale Mtume ﷺ maradhi yalipo mzidi aliwaomba ruhusa wake zale wamruhusu kuja kuuguzwa katika nyumba yangu, wakamruhusu” mpaka mwisho wa hadithi hii ambayo imeshapita huko nyuma. [Bukhari: 665]

    28- بَاب: هَلْ يُصَلِّي الْإِمَامُ بِمَنْ حَضَرَ؟ وَهَلْ يَخْطُبُ يَوْمَ الْجُمُعَةِ فِي الْمَطَرِ؟

    1. Mlango: Je anaswalisha Imam watu waliokuwepo na je inajuzu kwa Imamu kutoa hotuba ya Ijumaa huku mvua inanyesha

    401- عَنِ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّهُ خَطَبَ النَّاسَ فِي يَوْمٍ ذِي رَدْغٍ،( ) فَأَمَرَ الْمُؤَذِّنَ لَمَّا بَلَغَ حَيَّ عَلَى الصَّلاَةِ قَالَ: قُلْ: الصَّلاَةُ فِي الرِّحَالِ، فَنَظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ، كَأَنَّهُمْ أَنْكَرُوا، فَقَالَ: كَأَنَّكُمْ أَنْكَرْتُمْ هَذَا، إِنَّ هَذَا فَعَلَهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ مِنِّي – يَعْنِي النَّبِيَّ ﷺ- إِنَّهَا عَزْمَةٌ،( ) وَإِنِّي كَرِهْتُ أَنْ أُحْرِجَكُمْ. [رواه البخاري: 668].

    1. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنهما kwamba: Aliwahutubia watu siku moja katika siku ya joto kali sana akamuamrisha muadhini alipofika pale kusema: Haiyya ‘alal swalaa aseme: Swalini katika kambi zenu” Watu walivyosikia muadhini anasema hivyo hawakupendezwa. Ibn Abbas akawaambia: “Nakuoneni kama mmechukizwa au hamkupendezwa na kauli yangu hii, jambo kama hili alilifanya aliyekuwa bora zaidi kuliko mimi -anakusudia Mtume ﷺ – na hiyo ni Amri na mimi sikupenda kukutoeni kwenye kambi zenu na majumba yenu ilhali kuna joto kali sana.” [Bukhari: 668]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumanne, tarehe 13, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 17, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    25- بَاب: فَضْلِ مَنْ غَدَا إِلَى الْمَسْجِدِ وَمَنْ رَاحَ

    1. Mlango: Fadhila za Mtu mwenye kwenda msikitini mapema na kudumu kufanya hivyo

    397- وعَنْهُ رضي الله عنه، عَنْ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «مَنْ غَدَا إِلَى الْمَسْجِدِ وَرَاحَ، أَعَدَّ اللَّهُ لَهُ نُزُلَهُ مِنْ الْجَنَّةِ، كُلَّمَا غَدَا أَوْ رَاحَ».[رواه البخاري: 662].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Atakaye kwenda msikitini na kurudi Mwenyezi Mungu atamtayarishia nyumba yake peponi kwa kila anapokwenda au kurudi kutoka msikitini.” [Bukhari: 662]

    26- بَاب: إِذَا أُقِيمَتْ الصَّلاَةُ فَلاَ صَلاَةَ إِلاَّ الْمَكْتُوبَةَ

    1. Mlango: Inapoqimiwa swala haijuzu kuswali swala yeyote isipokuwa swala ya faradhi

    398- عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَالِكٍ ابْنِ بُحَيْنَةَ، رجلًا مِنْ الأَزْدِ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ رَأَى رجلًا وَقَدْ أُقِيمَتْ الصَّلاَةُ يُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ لاَثَ بِهِ النَّاسُ، وَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «الصُّبْحَ أَرْبَعًا؟! الصُّبْحَ أَرْبَعًا؟!». [رواه البخاري: 663].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Malik Ibn Buhaynah ambaye ni wa kabila la Azad رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ alimuona mtu mmoja anataka kuswali rakaa mbili ilhali swala ya fardhi imeshaqimiwa, alipomaliza swala Mtume ﷺ aliwageukia watu na kumuonesha mtu huyo akimwambia: “Kuna Swala ya Alfajiri ya rakaa nne!? Wala ya Alfajiri rakaa nne!? (Yaani alimkataza kwanini baada ya kuqimiwa swala ya Alfajiri anainuka kuswali rakaa mbili za sunna).” [Bukhari: 663]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumatatu, tarehe 12, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 16, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    22- بَاب: احْتِسَابِ الْآثَارِ

    1. Mlango: Thawabu za kutembea kutoka mbali kwenda kuswali jamaa

    394- عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه : أَنَّ بَنِي سَلِمَةَ أَرَادُوا أَنْ يَتَحَوَّلُوا عَنْ مَنَازِلِهِمْ، فَيَنْزِلُوا قَرِيبًا مِنْ النَّبِيِّ ﷺ ، قَالَ: فَكَرِهَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ أَنْ يُعْرُوا الْمَدِينَةَ،( ) فَقَالَ: «أَلاَ تَحْتَسِبُونَ آثَارَكُمْ».[رواه البخاري: 656].

    1. Imepokewa kutoka kwa Anas رضي الله عنه akisema: “Watu wa ukoo wa Bani Salama walitaka wahame kutoka kwenye majumba yao na vijiji vyao waje kuhamia karibu na msikiti wa Mtume ﷺ ili wawe wanaswali msikitini kwa haraka, Mtume ﷺ alivyosikia hivyo hakupendezwa akawaamrisha wasalie huko huko wanapoishi na akawaambia: “Hamtaki kupata thawabu nyingi zaidi za hatua mnazotembea kutoka kwenu kuja msikitini.” [Bukhari: 656]

    23- بَاب: فَضْلِ صَلاَةِ الْعِشَاءِ فِي الْجَمَاعَةِ

    1. Mlango: Fadhila ya swala ya Ishaa kuswali jamaa

    395- عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «لَيْسَ صَلاَةٌ أَثْقَلَ عَلَى الْمُنَافِقِينَ مِنْ الْفَجْرِ وَالْعِشَاءِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لاَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا». [رواه البخاري: 657].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Hakuna swala ambayo wanafiki wanaiona ni nzito kabisa kwao wao kuliko swala ya Alfajiri na Ishaa na lau kama wangelijua fadhila zinazopatikana katika swala mbili hizo basi wangezijia na kukimbilia hata kwa kusota.” [Bukhari: 657]
      24- بَاب: مَنْ جَلَسَ فِي الْمَسْجِدِ يَنْتَظِرُ الصَّلاَةَ، وَفَضْلِ الْمَسَاجِدِ
    2. Mlango: Fadhila za mwenye kukaa msikitini anasubiri swala na fadhila za msikiti

    396- وعَنْهُ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمْ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ، يَوْمَ لاَ ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ: الْإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأَ فِي عِبَادَةِ رَبِّهِ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرجلان تَحَابَّا فِي اللَّهِ، اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ طَلَبَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ( )وَجَمَالٍ، فَقَالَ: إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ، أَخْفَى حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللَّهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ».[رواه البخاري: 660].

    396.Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Watu saba Mwenyezi Mungu atawafunika chini ya kimvuli chake siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli cha Mwenyezi Mungu: (1) Kiongozi mkuu muadilifu (2) na kijana aliyekulia katika kumuabudu Mola wake (3) na mtu ambaye moyo wake umeshikamana sana na misikiti (4) na watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wamekutana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mpaka wakafa wakiwa bado wameshikamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (5) Na mwanaume aliyetakiwa na mwanamke mzuri mwenye cheo na mali lakini akakataa na kumwambia: Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu (6) na Mtu aliyetoa sadaqa akaificha kiasi kwamba mkono wa kushoto haujui kilichotolewa na mkono wake wa kulia (7) Na mtu mwengine aliyemtaja Mwenyezi Mungu faraghani peke yake mpaka akabubujikwa na machozi kutoka machoni mwake.” [Bukhari: 660]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumapili, tarehe 11, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 15, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    20- بَاب: فَضْلِ صَلاَةِ الْفَجْرِ فِي جَمَاعَةٍ

    1. Mlango: Fadhila ya swala ya Alfajiri katika jamaa

    391- عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهقَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ يَقُولُ: «تَفْضُلُ صَلاَةُ الْجَمِيعِ صَلاَةَ أَحَدِكُمْ وَحْدَهُ بِخَمْسٍ وَعِشْرِينَ جُزْءًا، وَتَجْتَمِعُ مَلاَئِكَةُ اللَّيْلِ وَمَلاَئِكَةُ النَّهَارِ فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ» ثُمَّ قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: فَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ ]إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا[[الإسراء: 78]. [رواه البخاري: 648].

    391.Imepokewa kutoka kwa Abu Huraya رضي الله عنه akisema: “Nimemsikia Mtume ﷺ akisema: “Swala ya jamaa na swala anayoswali mmoja wenu peke yake inazidi kwa thawabu kwa daraja ishirini na tano na malaika wa usiku wa zamu na wale malaika wengine wa zamu mchana wanakutana katika swala ya Alfajiri.” Anasema Abu Hurayra: “Na mktaka kujua fadhila hizo someni Aya inayosema: Hakika Qur’an ya Alfajiri inahudhuriwa na Malaika (Al-Israa:78).” [Bukhari: 648]

    392- عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنهقَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «أَعْظَمُ النَّاسِ أَجْرًا فِي الصَّلاَةِ أَبْعَدُهُمْ فَأَبْعَدُهُمْ مَمْشًى، وَالَّذِي يَنْتَظِرُ الصَّلاَةَ حَتَّى يُصَلِّيَهَا مَعَ الْإِمَامِ، أَعْظَمُ أَجْرًا مِنْ الَّذِي يُصَلِّي ثُمَّ يَنَامُ». [رواه البخاري: 651].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa Al Ash’ariyy رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Watu wenye fadhila na ujira mwingi mkubwa katika swala ya jamaa ni wale wanaotoka mbali na wale wanaokuja kwa kutembea kwa miguu, na yule anayesubiri swala mpaka aiswali swala hiyo na Imamu anapata thawabu nyingi zaidi kuliko yule ambaye anaswali nyumbani kwake kisha analala.” [Bukhari: 651]

    21- بَاب: فَضْلِ التَّهْجِيرِ إِلَى الظُّهْرِ

    1. Mlango: Fadhila za kuswali Adhuhuri mapema

    393- عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه : أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِطَرِيقٍ، وَجَدَ غُصْنَ شَوْكٍ عَلَى الطَّرِيقِ فَأَخَّرَهُ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ( )فَغَفَرَ لَهُ». [رواه البخاري: 652].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Wakati mmoja mtu alikuwa njiani alikuta mwiba njiani akautenga akauweka mbali watu wakashukuru kwa kitendo chake hicho na Mwenyezi Mungu akamfutia madhambi yake.” [Bukhari: 652]

    ثُمَّ قَالَ: «الشُّهَدَاءُ خَمْسَةٌ: الْمَطْعُونُ، وَالْمَبْطُونُ، وَالْغَرِيقُ، وَصَاحِبُ الْهَدْمِ، وَالشَّهِيدُ( )فِي سَبِيلِ اللَّهِ». وَبَاقِي الحَدِيثِ تَقَدَّمَ.( )[رواه البخاري: 653].

    Baada ya maneno hayo Mtume ﷺ akasema: “Mashahidi ni watano: kwanza anayeuwawa kwa mkuki au mshale, na anayefariki kutokana na maradhi ya kipindupindu na anayezama ilhali anajua kuogelea na aliyeangukiwa na nyumba akafa na vilevile aliyeuwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu.” Na iliyosalia katika hadithi hii imeshatangulia [Bukhari: 653]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Ijumaa, tarehe 08, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 13, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    12- بَاب: كَمْ بَيْنَ الْأَذَانِ وَالْإِقَامَةِ؟

    1. Mlango: Muda gani uwepo baina ya adhana na Iqama

    382- عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ المُزَنِيِّ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاَةٌ – ثلاثًا – لِمَنْ شَاءَ». [رواه البخاري: 624].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Mughaffal Al-Muzziyy رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Baina ya kila adhana mbili kuna swala ya sunna-alisema maneno hayo mara tatu- kwa anayetaka.” [Bukhari:624]

    وَفِي رِوايَةٍ: «بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاَةٌ، بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاَةٌ» ثُمَّ قَالَ فِي الثَّالِثَةِ: «لِمَنْ شَاءَ».[رواه البخاري: 627].

    Riwaya nyengine inasema: “Baina ya kila adhana mbili (yaani baina ya dhana na iqama) kuna swala” aliyakariri maneno hayo mara tatulakini mara ya mwisho akasema: “Swala hiyo kwa anayetaka.” [Bukhari:627]

    (12) [عن أنسِ بنِ مالكٍ رضي الله عنه قال: كان المؤذِّنُ إذا أَذَّنَ، قام ناسٌ من أصحابِ النبيِّ ﷺ يبتدِرونَ السَّواريَ، حتى يَخرُجَ النبيُّ ﷺ وهم كذلكَ، يُصَلُّونَ الرَّكعتينِ قبلَ المغرِبِ،ولم يكنْ بينَ الأذانِ والإِقامةِ شيء.
    قال الراوي:( ) لم يَكنْ بَينَهما إلا قليل].( ) [رواه البخاري: 625].

    (12)Nyongeza. kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه akisema: “Ilikuwa muadhini anapoadhini baadhi ya maswahaba wa Mtume ﷺ husimama kukimbilia nguzo za msikitini wakimsubiri mtume ﷺ aje msikitini na wana swali rakaa mbili kabla ya magharibi lakini hawakuwa wanafanya chochote baina ya adhana na iqama.”

    Mpokezi anasema: “Haijakuwa muda mrefu baina ya adhana na iqama kwa swala ya magharibi.” [Bukhari:625]

    13- بَاب: مَنْ قَالَ: لِيُؤَذِّنْ فِي السَّفَرِ مُؤَذِّنٌ وَاحِدٌ

    1. Mlango: Kuadhini mtu mmoja tu katika safari

    383- عَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رضي الله عنه قَالَ: أَتَيْتُ النَّبِيَّ ﷺ فِي نَفَرٍ مِنْ قَوْمِي، فَأَقَمْنَا عِنْدَهُ عِشْرِينَ لَيْلَةً، وَكَانَ رَحِيمًا رَفِيقًا، فَلَمَّا رَأَى شَوْقَنَا إِلَى أَهَالِينَا، قَالَ: «ارْجِعُوا فَكُونُوا فِيهِمْ، وَعَلِّمُوهُمْ، وَصَلُّوا، فَإِذَا حَضَرَتْ الصَّلاَةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أَحَدُكُمْ، وَلْيَؤُمَّكُمْ أَكْبَرُكُمْ».[رواه البخاري: 628].

    1. Imepokewa kutoka kwa Malik bin Al Huwayrith رضي الله عنه akisema: “Nilimuendea Mtume ﷺ nikiwa nimefuatana na baadhi ya watu wangu, tukakaa kwake kwa muda wa siku ishirini kama wageni wake, tukamkuta kwamba ni mtu Rahimu sana mpole alipokuja kutuona kwamba tunashauku ya kurudi kwetu kwa watu wetu alituambia: ‘Rudini nendeni na kaeni na watu wenu waelimisheni ilimu na swalini, na inapowadia wakati wa swala mmoja wenu aadhini na aliyekuwa na umri mkubwa kati yenu ndiyo akuswalisheni kama Imam wenu.” [Bukhari:628]

    14- بَاب: الْأَذَانِ لِلْمُسَافِرِ إِذَا كَانُوا جَمَاعَةً وَالْإِقَامَةِ

    1. Mlango: Adhana ya msafiri wakiwa jamaa pamoja na vipi kuqimu

    384- وعَنْهُ رضي الله عنه فِي رِوايَةٍ: أَتَى رجلان النَّبِيَّ ﷺ يُرِيدَانِ السَّفَرَ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «إِذَا أَنْتُمَا خَرَجْتُمَا، فَأَذِّنَا، ثُمَّ أَقِيمَا، ثُمَّ لِيَؤُمَّكُمَا أَكْبَرُكُمَا».[رواه البخاري: 630].

    1. Imepokewa kutoka kwa Malik bin Huwayrith رضي الله عنه katika riwaya nyengine akisema: “Watu wawili walimjia Mtume ﷺ wanataka kusafiri wamekuja kumuaga, akamwambia: “Mtapotoka mkasafiri basi muadhini na mqimu na aliyekuwa na umri zaidi kati yenu ndiyo awe Imam.” [Bukhari:630]

    (13) [وَعَنْهُ رضي الله عنه فِي رِوايَةٍ أُخْرَى: «وَصَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي»]. [رواه البخاري: 631].

    (13). Kutoka kwa Malk bin Huwayrith رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ amesema: “Na swalini kama mnavyoniona mimi ninaswali.” [Bukhari:630]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • عند دخول الإمام المسجد يوم الجمعة يقول المؤذن:

    1. يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُمْ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُقِيمٌ. خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ
    2. اللهم يا حنان يا منان! اللهم أعز الإسلام والمسلمين، وأذل الشرك والمشركين، وأعل كلمتك إلى يوم الدين، واختم لنا بفضل منك يا أرحم الراحمين!
    3. إمام يسلم على الحاضرين قى المسجد، ويجلس.
    4. المؤذن يؤذن ثم يختم بحديث الآتى:
    5. عن أبى هريرة رضي الله عنه قال: “قال رسول الله ﷺ: إِذَا قُلْتَ لِصَاحِبِكَ يَومَ الجُمُعَةِ: أنْصِتْ، والإِمَامُ يَخْطُبُ، فقَدْ لَغَوْتَ. ومن لغا فلا جمعة له!” أنصتوا، واستمعوا، واعتبروا: يرحمكم الله!
  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Alkhamis, tarehe 08, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 13, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    385- عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ كَانَ يَأْمُرُ مُؤَذِّنًا يُؤَذِّنُ، ثُمَّ يَقُولُ عَلَى إِثْرِهِ: «أَلاَ صَلُّوا فِي الرِّحَالِ» فِي اللَّيْلَةِ الْبَارِدَةِ، أَوْ الْمَطِيرَةِ فِي السَّفَرِ. [رواه البخاري: 632].

    1. Imepokewa kutoka kwa Ibn Umar رضي الله عنهما akisema: “Mtume ﷺ alikuwa akimuamrisha muadhini aadhini kisha anamwambia aseme katika mwisho wa adhana yake: “Enyi watu! Swalini katika kambi zenu” alikuwa akimuamrisha muadhini aseme maneno hayo katika usiku wa baridi kali au siku ya mvua kubwa safarini.” [Bukhari:632]

    15- بَاب: قَوْلِ الرَّجُلِ فَاتَتْنَا الصَّلاَةُ

    1. Mlango: Mtu anaposema: Swala imetupita nini hukumu yake

    386- عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنهقَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ نُصَلِّي مَعَ النَّبِيِّ ﷺ ، إِذْ سَمِعَ جَلَبَةَ الرِجَالٍ، فَلَمَّا صَلَّى قَالَ: «مَا شَأْنُكُمْ؟( )» قَالُوا: اسْتَعْجَلْنَا إِلَى الصَّلاَةِ. قَالَ: «فَلاَ تَفْعَلُوا، إِذَا أَتَيْتُمْ الصَّلاَةَ فَعَلَيْكُمْ بِالسَّكِينَةِ، فَمَا أَدْرَكْتُمْ فَصَلُّوا، وَمَا فَاتَكُمْ فَأَتِمُّوا».[رواه البخاري: 635].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah رضي الله عنه akisema: “Wakati mmoja tulikuwa tukiswali na Mtume ﷺ mara akasikia makelele ya watu wanaume, alipomaliza swala akawauliza: “Kelele za nini zile nimezisikia?” wakamwambia: “Tulikuwa tunakimbilia kuswali isitufutu” Mtume ﷺ akawaambia: “Msifanye tena, mkija kuiswali tembeeni kwa utulivu na unyenyekevu mtachodiriki swalini na kitachokupiteni kamilisheni.” [Bukhari:635]

    (14) [وَفِي رِوَايَةٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه ،عَنِ النَّبِيِّﷺ قَالَ:«إِذَا سَمِعْتُمُ الإِقَامَةَ فَامْشُوا إِلَى الصَّلاَةِ، وَعَلَيْكُمْ بِالسَّكِينَةِ وَالْوَقَارِ وَلاَ تُسْرِعُوا، فَمَا أَدْرَكْتُمْ فَصَلُّوا وَمَا فَاتَكُمْ فَأَتِمُّوا»]. [رواه البخاري: 636].( )
    (14) Nyongeza. Riwaya nyengine ya Abu Hurayra inasema: “Amesema Mtume ﷺ : “Mkisikia iqama inaadhiniwa basi jongeeni kwenye swala kwa utulivu na unyenyekevu na vilevile kwa heshima wala msifanye pupa kukimbili mtachodiriki swalini na kitachokupiteni kikamilisheni.” [Bukhari: 636]

    16- بَاب: مَتَى يَقُومُ النَّاسُ إِذَا رَأَوْا الْإِمَامَ عِنْدَ الْإِقَامَةِ؟

    1. Mlango: Wakati gani watu wanatakiwa kusimama wanapomuona Imam amesimama baada ya kuqimiwa swala

    387- وعَنْهُ رضي الله عنه، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «إِذَا أُقِيمَتْ الصَّلاَةُ، فَلاَ تَقُومُوا حَتَّى تَرَوْنِي».[رواه البخاري: 637].

    387.Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Ikiqimiwa swala msisimame mpaka mnione mimi nimeingia.” [Bukhari: 637]

    (15) [زَادَ فِي رِوَايَةٍ: «وَعَلَيْكُمْ بِالسَّكِينَةِ»]. [رواه البخاري: 638]( )

    (15) Nyongeza. Riwaya nyengine inasema: “Na mnaposimama simameni kwa utulivu na mqimu.” [Bukhari:638 ]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumatano, tarehe 07, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 11, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    12- بَاب: كَمْ بَيْنَ الْأَذَانِ وَالْإِقَامَةِ؟

    1. Mlango: Muda gani uwepo baina ya adhana na Iqama

    382- عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ المُزَنِيِّ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاَةٌ – ثلاثًا – لِمَنْ شَاءَ». [رواه البخاري: 624].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Mughaffal Al-Muzziyy رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Baina ya kila adhana mbili kuna swala ya sunna-alisema maneno hayo mara tatu- kwa anayetaka.” [Bukhari:624]

    وَفِي رِوايَةٍ: «بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاَةٌ، بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلاَةٌ» ثُمَّ قَالَ فِي الثَّالِثَةِ: «لِمَنْ شَاءَ».[رواه البخاري: 627].

    Riwaya nyengine inasema: “Baina ya kila adhana mbili (yaani baina ya dhana na iqama) kuna swala” aliyakariri maneno hayo mara tatulakini mara ya mwisho akasema: “Swala hiyo kwa anayetaka.” [Bukhari:627]

    (12) [عن أنسِ بنِ مالكٍ رضي الله عنه قال: كان المؤذِّنُ إذا أَذَّنَ، قام ناسٌ من أصحابِ النبيِّ ﷺ يبتدِرونَ السَّواريَ، حتى يَخرُجَ النبيُّ ﷺ وهم كذلكَ، يُصَلُّونَ الرَّكعتينِ قبلَ المغرِبِ،ولم يكنْ بينَ الأذانِ والإِقامةِ شيء.
    قال الراوي:( ) لم يَكنْ بَينَهما إلا قليل].( ) [رواه البخاري: 625].

    (12)Nyongeza. kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه akisema: “Ilikuwa muadhini anapoadhini baadhi ya maswahaba wa Mtume ﷺ husimama kukimbilia nguzo za msikitini wakimsubiri mtume ﷺ aje msikitini na wana swali rakaa mbili kabla ya magharibi lakini hawakuwa wanafanya chochote baina ya adhana na iqama.”

    Mpokezi anasema: “Haijakuwa muda mrefu baina ya adhana na iqama kwa swala ya magharibi.” [Bukhari:625]

    13- بَاب: مَنْ قَالَ: لِيُؤَذِّنْ فِي السَّفَرِ مُؤَذِّنٌ وَاحِدٌ

    1. Mlango: Kuadhini mtu mmoja tu katika safari

    383- عَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رضي الله عنه قَالَ: أَتَيْتُ النَّبِيَّ ﷺ فِي نَفَرٍ مِنْ قَوْمِي، فَأَقَمْنَا عِنْدَهُ عِشْرِينَ لَيْلَةً، وَكَانَ رَحِيمًا رَفِيقًا، فَلَمَّا رَأَى شَوْقَنَا إِلَى أَهَالِينَا، قَالَ: «ارْجِعُوا فَكُونُوا فِيهِمْ، وَعَلِّمُوهُمْ، وَصَلُّوا، فَإِذَا حَضَرَتْ الصَّلاَةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أَحَدُكُمْ، وَلْيَؤُمَّكُمْ أَكْبَرُكُمْ».[رواه البخاري: 628].

    1. Imepokewa kutoka kwa Malik bin Al Huwayrith رضي الله عنه akisema: “Nilimuendea Mtume ﷺ nikiwa nimefuatana na baadhi ya watu wangu, tukakaa kwake kwa muda wa siku ishirini kama wageni wake, tukamkuta kwamba ni mtu Rahimu sana mpole alipokuja kutuona kwamba tunashauku ya kurudi kwetu kwa watu wetu alituambia: ‘Rudini nendeni na kaeni na watu wenu waelimisheni ilimu na swalini, na inapowadia wakati wa swala mmoja wenu aadhini na aliyekuwa na umri mkubwa kati yenu ndiyo akuswalisheni kama Imam wenu.” [Bukhari:628]

    14- بَاب: الْأَذَانِ لِلْمُسَافِرِ إِذَا كَانُوا جَمَاعَةً وَالْإِقَامَةِ

    1. Mlango: Adhana ya msafiri wakiwa jamaa pamoja na vipi kuqimu

    384- وعَنْهُ رضي الله عنه فِي رِوايَةٍ: أَتَى رجلان النَّبِيَّ ﷺ يُرِيدَانِ السَّفَرَ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «إِذَا أَنْتُمَا خَرَجْتُمَا، فَأَذِّنَا، ثُمَّ أَقِيمَا، ثُمَّ لِيَؤُمَّكُمَا أَكْبَرُكُمَا».[رواه البخاري: 630].

    1. Imepokewa kutoka kwa Malik bin Huwayrith رضي الله عنه katika riwaya nyengine akisema: “Watu wawili walimjia Mtume ﷺ wanataka kusafiri wamekuja kumuaga, akamwambia: “Mtapotoka mkasafiri basi muadhini na mqimu na aliyekuwa na umri zaidi kati yenu ndiyo awe Imam.” [Bukhari:630]

    (13) [وَعَنْهُ رضي الله عنه فِي رِوايَةٍ أُخْرَى: «وَصَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي»]. [رواه البخاري: 631].

    (13). Kutoka kwa Malk bin Huwayrith رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ amesema: “Na swalini kama mnavyoniona mimi ninaswali.” [Bukhari:630]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumanne, tarehe 06, Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 10, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    9- بَاب: أَذَانِ الأَعْمَى إِذَا كَانَ لَهُ مَنْ يُخْبِرُهُ

    1. Mlango: Adhana ya kipofu ambaye haadhini mpaka aambiwe na watu kwamba wakati wa kuadhini umefika

    379- عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «إِنَّ بِلاَلًا يُؤَذِّنُ بِلَيْلٍ، فَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يُنَادِيَ ابْنُ أُمِّ مَكْتُومٍ» قَالَ: وَكَانَ رجلًا أَعْمَى، لاَ يُنَادِي حَتَّى يُقَالَ لَهُ: أَصْبَحْتَ أَصْبَحْتَ. [رواه البخاري: 617].

    1. Imepokewa kutoka kwa Ibn Umar رضي الله عنهما akisema: “Mtume ﷺ amesema: “Bilal anaadhini usiku kwa hivyo anapoadhini nyie kuleni na kunyweni mpaka atapoadhini Ibn Ummi Maktuum.” Anasema: “Na Ibn Maktum alikuwa kipofu, haebdi kuadhini mpaka watu wamzindue kumwambia: “Asubuhi imeshaungia.” [Bukhari:617]

    10- بَاب: الأَذَانِ بَعْدَ الْفَجْرِ

    1. Mlango:Kuadhini baada ya kuingia Alfajiri

    380- عَنْ حَفْصَةُ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ كَانَ إِذَا اعْتَكَفَ الْمُؤَذِّنُ لِلصُّبْحِ،( ) وَبَدَا الصُّبْحُ، صَلَّى رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ تُقَامَ الصَّلاَةُ. [رواه البخاري: 618].

    1. Imepokewa kutoka kwa Hafswa رضي الله عنها akisema: “Mtume ﷺ alikuwa akikaa ‘itikafu na muadhini akafika akaadhini kwa swala ya Alfajiri basi Mtume ﷺ huanza kwa kuswali rakaa mbili nyepesi za sunna kabla ya kuswaliwa swala ya Alfajiri.” [Bukhari:618]

    11- بَاب: الأَذَانِ قَبْلَ الْفَجْرِ

    1. Mlango: Kuadhini kabla ya Alfajiri

    381- عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه ، عَنْ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «لاَ يَمْنَعَنَّ أَحَدَكُمْ، أَوْ أحدًا مِنْكُمْ، أَذَانُ بِلاَلٍ مِنْ سَحُورِهِ، فَإِنَّهُ يُؤَذِّنُ – أَوْ يُنَادِي– بِلَيْلٍ، لِيَرْجِعَ قَائِمَكُمْ، وَلِيُنَبِّهَ نَائِمَكُمْ، وَلَيْسَ أَنْ يَقُولَ الْفَجْرُ، أَوْ الصُّبْحُ»وَقَالَ بِأَصَابِعِهِ، وَرَفَعَهَا إِلَى فَوْقُ، وَطَأْطَأَ إِلَى أَسْفَلُ، حَتَّى يَقُولَ هَكَذَا، يُشِيرُ بِسَبَّابَتَيْهِ،( ) إِحْدَاهُمَا فَوْقَ الْأُخْرَى، ثُمَّ مَدَّهَا عَنْ يَمِينِهِ وَشِمَالِهِ. [رواه البخاري: 621].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Asizuiliwe mmoja wenu kula daku lake kwa kusikia adhana ya Bilal kwa sababu Bilal anaadhini usiku kwa hivyo yeyote aliyezindukana arudi katika hema lake na amuamshe aliyelala wala akamuamsha asimwambie kwamba imeingia Alfajiri au asubuhi imeingia” na mtume ﷺ aliposema maneno hayo aliinua vidole vyake kwenda juu kisha akaviinamisha chini akiashiria kwa kidole chake cha shahada kimoja juu ya chengine kisha akanyoosha mkono wake upande wa kushoto na kulia (yaani asiseme kwamba Alfajiri imeingia kutoka upande huu au upande huu au juu au chini bali kuleni kutokana na adhana ya Bilal).” [Bukhari:621]