Category: Maswali

  • Nimeulizwa kuhusu Talaka ya mume kwa mkewe, aliyoitundika, NANUKUU:-

    Assalama alaikum al habbi naomba kujua huku au majibu ya hili jambo

    kuna wanandoa wamegombana baada ya kukutwa na hatia mume ndo mkosa akabidi aombe msamah mwanamke akamuambia ili nikusameh niahidi kutorudia tena hilo
    tena uniahid vzur mume aliahid hivi endapo nitafanya kosa hilo bas ndo talaka yako akimuahakikishia mke ili tu amsamhe(akajitundilkia yye talaka)mwanamke akamsameh sasa nafs ya mume kila mda inamsuta n kumuambia umeahid vby sana tengua ahid kingine ssa nini akifanye ili talaka alotundika itenguke na mkewe ameongea nae yuko Radhi kwa hilo ila hawajui nni kifanyike naomb muongoz maalim

    JIBU

    BISMILLAH*

    Msimamo wa wanazuoni wengi ni kuwa Talaka iliyotundikwa na mtoaji Talaka, yaani Mume mwenyewe, kwa hiari yake, kuhusu kutenda jambo linaloweza kutendwa NAYE, na jambo hilo akalitenda, BASI TALAKA IMETOKEA, PAPO HAPO, NA MKE AMEACHIKA, BILA YA KUJALI KAMA ALITOA TALAKA HIYO KWA UKWELI AU KWA KITISHO TU, AU KUMDANGANYA MKEWE TU. TALAKA ITATOKEA KISHARIA.
    MTUME صلى الله عليه وسلم AMESEMA:
    ثلاث جدهن جد، وهزلهن جد. الطلاق، والعتاق والدين.
    “Mambo matatu, ukweli wake ni kweli na mzaha wake ni kweli. 1.Talaka 2.Kuacha mtumwa huru na 3.Kuungama Deni!”

    Ameipokea Abu Daud na Ibn Majah.

    Hivyo TALAKA NI JAMBO ZITO SANA KATIKA SHARIA ZA UWISLAMU: SI MFANO WA KADI YA REFA KWENYE UWANJA WA MCHEZO WA MPIRA.
    TALAKA NI TAMKO LA KUVUNJA AHADI ILIYOTOLEWA WAKATI WA KUOA. UMEOA KWA TAMKO LA AHADI KWA MWENYEZI MUNGU, NA UNAIVUNJA AHADI HIYO NA MOLA WAKO, KWA TAMKO LA KUACHANA NA MWANAMKE ULIYEOZESHWA KIHALALI!
    MUNKARI ULIOKUBUHU!

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎

    من السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم

    Imejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    Kutoka Masuali na Majibu: Nimeulizwa, NANUKUU:– yanayo jibiwa kila siku kwenye kumbi za Darasa za Mitandaoni, za Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aalish- Shaykh Abi Bakr bin Salim.‎

    JIUNGE KWENYE MOJAWAPO WA KUMBI ZA SAYYID ABDULQADIR KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, NA MAHALI ULIPO, KWENDA NAMBA 0786887887 KUPITIA WHATSAP TU!

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • Je, majini wataingia peponi?

    Je, majini wataingia peponi?

    Nimeulizwa NANUKUU:-

    Al Habib Assalamu alaykum Mimi Nina swali dogo shareef Allah katuumba sisi na majini ili tumuabudu na akatuahidi sisi wanaadamu malipo ya pepo siku ya kiyama lakini pia Allah s,w kasema atawajaza motoni majini na watu lakini kuhusu peponi haijaelezwa je majini tutaingia nao peponi pamoja?

    JIBU

    BISMILLAH

    Kwa ufupi, kote kuwili kutajazwa wastahikifu wake tu, kutoka katika viumbve hivyo viwili; majini na wanaadamu. Acha nifafanue: Neno HAQQ maana yake USTAHIKIFU, au kwa maneno mengine, USTAHIKI, USTAHILI, USTAHILIVU na kadhalika. Kwa mfano, mtu akifanya jambo baya, akapatwa na madhara, huambiwa Astahili yako! Na mtu akifanya jambo jema akatunzwa huambiwa: Hongera unastahiki zawadi.

    Hibyo, pale watu wa Peponi watapomaliza kungia Peponi, na watu wa Motoni wakamaliza kuingia Motoni, basi majaaliwa hayo ndiyo USTAHILIVU wa kila kundi la viumbe vya Mwenyezi Mungu kutokana na AMALI ZAO walizozintanguliza kabla ya kufa na kuhesabiwa. Huko ndii kukamilisha USTAHILIVU wa kila mmoja, Wema kwa Wema na Uovu kwa Uovu. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema kwenye Kitabu Chake:

    وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ. إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ

    Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana, Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja.

    قال الشوكاني في تفسير هذه الآية: وإنما قضى عليهم بهذا لأنه سبحانه قد علم أنهم من أهل الشقاوة، وأنهم ممن يختار الضلالة على الهدى. اهـ.

    Mwenyezi Mungu amepitisha uamuzi Wake wa kuwahukumu watu hawa, kwa sababu AMEJUA kuwa ni miongoni mwa waja Wake waliojichagulia wenyewe UPOTOVU kwa vitendo vyao, wataishia wapi, baada ya kujichagulia Uongofu.

    Na kwa maana hiyo, mwenye kutenda mema atalipwa mema, na mwenye kutenda maovu atalipwa uovu. Na Mwenyezi Mungu ametubainishia wazi wazi kuwa Hakuna Usawa wa malipo, baina ya makundi mawili yenye kutofautiana: kundi la Mafasiki V Muumini. Hakuna malipo sawa kwa makundi hayo mawili tofauti. Amesema katika Sura mbali mbali, nani ya Qur’ani, kama ifuatavyo:

    وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ

    Na Mola wako, lau angelitaka, angeli wafanya watu wote wakawa umma mmoja; lakii hawaachi kutofautiana na kuhitalafiana. I_sipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja. (Huud, 11:118-9)

    Na Amesema:

    أَفَمَنْ كَانَ مُؤْمِنًا كَمَنْ كَانَ فَاسِقًا ۚ لَا يَسْتَوُونَ! أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ؟

    Je. aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa! Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu? (Swaad 38:28)

    أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ؟ مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ؟

    Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? Mna nini? Mnahukumu vipi? (Al-Qalam, 68:35-36)

    وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَلَا الْمُسِيءُ ۚ قَلِيلًا مَا تَتَذَكَّرُونَ

    Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na walio amini na watendao mema hawalingani na muovu. Ni machache mnayo yakumbuka. (Ghafir, 48:58)

    Katika Aya zote hizo, Mwenyezi Mungu ametubainishia wazi wazi, kuwa viumbe Vyake vimegawika katika makundi mawili makuu, Kundi la Wapotofu ambao majaaliwa yao ni kuishia kuingizwa Motoni, na Kundi la Watiifu, ambao majaaliwa yao ni kuishia kuingizwa Peponi. Ndiyo maana Akasema kuwaambia watu wa kila kundi husika: ndani ya Aya hiyo hiyo

    فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ ۖ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ

    Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. (As-Sajdah, 32: 14)

    فعلم من هذا أن امتلاء جهنم بهؤلاء لاستحقاقهم العذاب؛ وإلا فإن الله تعالى غني عن أن يعذب عباده، فقد صرح سبحانه أنه لا ينفعه ذلك، ولا يريده شرعا لكن الناس أنفسهم يظلمون؛ كما قال تعالى: ما يفعل الله بعذابكم إن شكرتم وآمنتم {النساء: 147}.

    Ndiyo maana ikatangazwa na kujulikana kuwa Kujazwa kwa Moto kwa watu waovu ni kutokana na USTAHIKIFU wao wa kuwepo huko; pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu hana haja ya kuwaadhibu Waja Wake, wala hapati manufaa yoyote kwa kuwaadhibu; bali wao wenyewe ndio waliotenda uovu, wakastahiki kuingizwa Wote Motoni kutokana na vitendo vyao wenyewe viovu. Mwenyezi Mungu hana haja ya kuwaadhibu waje Wake, kama alivyofafanua hivyo Mwenyewe, ila ni Viumbe Vyake venyewe, ndivyo vinavyo jiamulia waende wapi kutokana na dhuluma zao. Ndio maana Mwenyezi Mungu Akasema: Hafanyi kitu Mola wenu kwa kukuadhibisheni; ila mkinishuruku nitakuzidishieni malipo mema, na mkinikufuru basi juweni kuwa Adhabu Zangu ni kali mno (An-Nisaa,4:147) na Akasema:

    وقال: إن تكفروا فإن الله غني عنكم ولا يرضى لعباده الكفر وإن تشكروا يرضه لكم ولا تزر وازرة وزر أخرى ثم إلى ربكم مرجعكم فينبئكم بما كنتم تعملون إنه عليم بذات الصدور {الزمر: 7}.

    Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani._ (Az-Zumar, 39:7)

    Na Mwenyezi Mungu amekariri USTAHIKIFU huo wa kila kundi mahali mbali mbali ndani ya Kitabu Chake Kitukufu. Tunukuu Aua chache kuhusu Maudhui hiyo:

    كقوله عز وجل: لقد حق القول على أكثرهم فهم لا يؤمنون {يس: 7}.

    Bila ya Shaka, Kauli (ya Ustahikifu) imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo haaamini. (Yasin,36:7)

    قال السعدي: إنما حق عليهم القول بعد أن عرض عليهم الحق فرفضوه، فحينئذ عوقبوا بالطبع على قلوبهم. اهـ.

    Amesema As-Sa’diy akifasiri Aya hiyo: Kauli au Ahadi ya Mwenyezi Mungu imewastahiki, baada ya kuwaeleza wajibu wao, lakini wakakataa maelzo hayo, hivyo basi wakaadhibiwa kutokana na tabia ya ukaidi na ukanushi ndani ya nyoyo zao.

    وقوله تعالى: وتمت كلمت ربك صدقا وعدلا لا مبدل لكلماته وهو السميع العليم {الأنعام: 115}

    Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. (Al-An’am 6:116)

    Ndiyo maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu, yasemayo:

    إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ

    Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja (HUUD,11:119)

    قال ابن كثير: يخبر تعالى أنه قد سبق في قضائه وقدره، لعلمه التام وحكمته النافذة، أن ممن خلقه من يستحق الجنة، ومنهم من يستحق النار، وأنه لا بد أن يملأ جهنم من هذين الثقلين الجن والإنس، وله الحجة البالغة والحكمة التامة. اهـ.

    Ibn Kathiir akifasiri Aya hizi, amesema: “Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba: Kutokana na Ujuzi wke wa Utangu, Ameshaamua kupitia Hukumu Zake na Maaaliwa yake, kupitia Ujuzi wake kamilikfu, uliotimia na kutokana na Hekima zake, kuwa wapo waja Wake ambao Wanastahiki kuingia Peponi, na wapo Wanaostahiki kuingia Motoni. Na kwamba ni uhakika kuwa Moto wa Jahannam utajazwa na Viumbe Vyake hivyo, viwili: Majini na Wanaadamu; na hivyo Mweniezi Mungu Ana Hoja kamili na timilifu, na Hekima iliyokamilika.”

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    Limejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

  • Ufafanuzi wa Aya Zenye Msamaha na Adhabu

    Ufafanuzi wa Aya Zenye Msamaha na Adhabu

    NIMEULIZWA NANUKUU:-

    Swali langu Al Habib Allah Katika quran katupa nafasi ya kuomba msamaha tunapokosea turejee kwake, na pia katuambia anasamehe madhambi yote, Aya nyengine anasema Allah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo duni ya hayo kwa amtakaye Na aya nyengine anasema mwenye kumuua muumini kwa kukusudia malipo yake jahanam milele na laana ya Allah juu yake. Sasa suala langu msingi nataka kujua hizi aya ipi mansuh

    JIBU
    BISMILLAH

    Umeshapata MAJIBU katika Aya hizo zote. Hakuna zaidi.

    Acha nifafanue!

    1.Atayekufa bila ya kutubu hatia ya ushirikina HANA MSAMAHA.

    2.HAKI YOYOTE ILIYOPO BAINA YA MJA NA MOLA WAKE, INAWEZA KUSAMEHEWA NA MOLA WAKE, AKITUBU TOBA YA KWELI NA KURUDI KWA MOLA WAKE, KABLA YA KUFA KWAKE.

    3.HAKI YOYOTE ILIYOPO BAINA YA MWANADAMU NA MWANADAMU MWENZIWE, HAIWEZI KUSAMEHEWA ISIPOKUWA ALIYE DHULUMIWA ASAMEHE, VENGINEVYO ITALIPISHWA KWENYE MAHAKAMA YA MBINGUNI.

    4.HUKUMU YA KUMUUA MWISLAMU, PASI NA HAKI, NI KUUAWA ALIYEMUUA. AKIKIMBIA KUULIWA DUNIANI, AKAFA BILA YA KUTUBU, ATAISHIA KUINGIZWA MOTONI MILELE.

    FULL STOP.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق