Category: Maswali

  • Nimeulizwa NANUKUU-:

    Shekhe Nina swali kama ifuatavyo-

    Mke nilienae alizaa mtoto WA kike Kwa mume mwengine na Mimi nilizaa mtoto WA kiume Kwa mke mwengine je Hawa watoto inafaa kuoana?

    JIBU

    BISMILLAH!

    Inajuzu mtoto wako wa kiume uliyezaa na mke mwengine, kumuoa binti wa mkeo, aliyezaa na mume mwengine, ambaye huitwa ربيبة yaani binti wako wa kulea, kwa vile umemuoa mama yake.

    Rabibah ni haramu kwako kumuoa, lakini si haramu kuolewa na mtoto wako wa kiume uliyezaa na mke mwengine.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎

    من السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم

    Imejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    Kutoka Masuali na Majibu: Nimeulizwa, NANUKUU:– yanayo jibiwa kila siku kwenye kumbi za Darasa za Mitandaoni, za Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aalish- Shaykh Abi Bakr bin Salim.‎

    JIUNGE KWENYE MOJAWAPO WA KUMBI ZA SAYYID ABDULQADIR KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, NA MAHALI ULIPO, KWENDA NAMBA 0786887887 KUPITIA WHATSAP TU!

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • Nimeulizwa kuhusu Waqfu, NANUKUU:-

    SHEIKH NAOMBA KUULIZA. WAKFU NI NINI? AINA ZA WAKFU? FAIDA ZA WAKFU

    JIBU

    BISMILLAH

    Waqfu (kwa upande wa Lugha ya Kiarabu: الوقف Ni mkataba maalum ambapo mali hukabidhiwa au huwasilishwa ili watu wa kikundi au tabaka fulani waweze kunufaika nayo.

    Kwa upande wa Sharia, hata hivyo, Waqfu

    حبس العين عن تمليكها لأحد من العباد والتصدق بالمنفعة على مصرف مباح. والعين إما أن تكون دارا أو بستانا أو نقدا
    Kuzuwiya kitu fulani, kisiweze kumilikiwa na mtu yeyot, miongoni mwa watu, na badala yake kukifanya kitu husika kuwa manufaa yake ni sadaka kwa matumizihalali. Na kitu cha Waqfu ni ama Nyumba, Shamba au Pesa taslimu.

    Katika waqfu hakuna hata mmoja mwenye haki ya kuuza au kutoa mali ya waqf na kuihamishia kwa watu wengine, si mweka waqfu wala si waliokusudiwa kunufaika na mali hiyo ya waqfu. Qur’an haikuzugumzia suala la waqfu kwa uwazi Katika Hadithi, mali ya waqfu imezingatiwa kama ni “sadaka endelevu (sadaqatu al-Jaria)”. Historia ya waqfu inarudi kwenye zama za kabla ya Uislamu. Hata hivyo, suala la watu kuweka waqfu lilikuwa ni maarufu kati ya masahaba tokea wakati wa maisha ya Mtume ﷺ.

    Hivyo, Waqfu katika istilahi za wanazuoni ni aina ya mkataba ambao kupitia mkataba huo, mali fulani hutolewa ili tu watu wanufaike na faida yake. Kwa mfano, mahali fulani huwekwa kwa ajili ya maskini, ili maskini hao wapate wanufaike na faida ya mahali hapo, huku hati ya kuweza kuuza au kununua mahali hapo ikiwa imefutwa moja kwa moja (yaani hapauziki wala kununulika kisheria). katika mkataba wa waqfu, mali hutoka katika umiliki wa mwekaji waqfu, kwa hiyo sio yeye wala wale waliowekewa waqfu, anaweza kuwa na mamlaka ya kuuza au kutoa mali hiyo. MALI HUSIKA IMEFUNGWA KABISA.

    Kwa maneno mengine, Waqfu ni mojawapo ya aina za mikataba katika Uislamu. Mkataba huu umejadiliwa na kufafanuliwa, sana, katika vitabu vya fiqh, ambapo masharti na nguzo za uhalali na hukumu zake yamefafanuliwa ndani yake. Kwa ufupi, hata hivyo, Waqfu imegawanywa katika aina mbili: Waqfu maalumu na Waqfu wa kiujumla (waqfu huria).

    Katika vitabu vya fiqh, waqfu umegawanywa katika aina mbili: waqfu wa umma (waqfu huria) na waqfu makhususi (waqfu kwa walengwa maalumu). Waqfu ulio wekwa kwa lengo la umma au kwa ajili ya umma huitwa waqfu wa umma, kama vile waqfu wa shule au hospitali au nyumba ya mayatiima, kwa ajili ya maskini au wanazuoni. Waqfu unaowekwa kwa lengo la walengwa makhususi, au kwa ajili ya kikundi maalum huitwa wakqu makhususi, kama vile waqfu wa mahali fulani kwa mtu au watu na walengwa maalumu.

    Katika Qur’an, neno WAQFU halikutajwa kabisa ndani yake, lakini katika vitabu vyenye kujadili Aya zinazozungumzia sheria za kifiqhi, suala la waqfu limeorodheshwa katika orodha sawa na masuala ya sukna (سُکنیٰ) (matumizi ya faida ya mali kwa muda maalum), sadaka, na zawadi, na imeainishwa chini jumla ya masuala yanayo husiana na misaada inayo tolewa bila ya malipo (mali ambayo hupewa watu bila yakutakiwa watowe ujira wowote kutoka kwa watu hao).

    Nafasi ya waqfu katika vitabu hivyo imefanana na baadhi ya dhana za misaada mingine ilioko kwenye Aya za Qur’ani, kama vile infaq (kutoa sadaka) na kutoa zawadi ya mali هبة . Kulingana na Hadithi, sadaka inayoendelea (waqfu وقف) ni mojawapo ya mambo ambayo hueendelea faida zake hata baada ya kifo cha mtoaji wa sadaka hiyo. Bila shaka, katika Hadithi hizi, neno waqfu limetumika mara chache tu, ila neno sadaka ndilo neno liliokoza rangi zaidi katika uwanja wa Hadithi. Hata hivyo, katika Hadithi zinazohusiana na sheria za waqfu, neno waqfu limeonekana kumetumika ndani yake. Mwenye kutaka, zaidi, kuhusu Waqfu, Sharia zake, Masharti yake, Nguzo zake, na kadhalika AKATAFUTE VITABU VYA VINAVYO ZUNGUMZIA, KWA KINA, SUALA LA WAQFU.

    Mada ya waqfu ni mojawapo ya mada zinazojadiliwa sana miongoni mwa Waislamu. Mbali na maandishi ya kifiqhi juu ya mada hii, pia kuna vitabu na makala nyingi zilizo JIKITA katika kujadili suala la waqfu.

    Kuna maoni tofauti kuhusu asili ya waqfu na inaaminika kwamba; amali ya waqfu ina historia ndefu na kwamba iliibuka kabla ya Uislamu. Hata hivyo, baada ya Uislamu, amali ya waqfu ilianza kuenea haraka miongoni mwa Waislamu. Mtume Muhammad ﷺ mwenyewe aliwahi kumiliki mali na kuitoa waqfu. Mara ya kwanza bwana Mtume ﷺ , alitoa ardhi ya kwa ajili kutumiwa na wasafiri waliokwama katika safari zao (ibnu sabiil). Pia, kuna Hadithi iliyo nukuliwa kutoka kwa Sayyidina Jabir bin Abdullah Ansari, رضي الله عنه inayosema kwamba; “Hakuna mtu miongoni mwa Maswahaba ambaye alikuwa na uwezo wa kifedha akawa hakuwahi kutoa kitu chochote kwa ajili ya waqfu.”

    Katika baadhi ya maandishi yanayo husiana na waqfu, pia kuna mazungumzo juu ya athari za waqfu katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Kulingana na maelezo mbali mbali ya kihistoria, baadhi ya masuala ambayo mali za waqfu huweza kutumika ni: Ujenzi wa misikiti, masshule, maktaba na hospitali, jela za wendawazimu, visima, misingi ya maji na huduma kwa maskini, yatima, walemavu na wafungwa, na utoaji wa gharama za maisha kwa wanazuoni. Kwa hivyo wanazuoni wamesema kuwa; waqfu ilikuwa na jukumu la kuhudumiu maeneo ya utoaji wa huduma za kijamii, afya na matibabu na kueneza kwa elimu na teknolojia.

    Wengine, kwa msingi wa tafiti za kihistoria, wamegawanya kazi za waqfu katika maeneo manne yafuatayo:

    1. Masuala ya kitamaduni: kama vile kuanzisha shulei, vitabu na maktaba.
    2. Masuala ya afya: kama vile kuanzisha hospitali, jela za wendawazimu na mabwawa ya maji.
    3. Masuala ya kijamii na ustawi: kama vile ujenzi wa karakana, daraja, ngome, visima, misingi ya maji na viwanda.
    4. Masuala ya kidini: kama vile kujenga misikiti na viwanya vya kuzikia watu wema. [27]

    Kutokana na ukweli wa Ulafi, Ulanguzi, Wizi na Unyang’anyi, nchi nyingi za Kiislamu huwa na Wizara maalumu zinazoitwa Wizara ya Mali za Waqfu, kudhibiti Ulafi, Ulanguzi, Ufujaji wa Mali za Waqfu, na hata vitendo haramu vya kuuza mali za Waqfu. Kwa nchi ambazo hazifuati Sharia za Kiislamu, basi kwa uchache kutakuwepo IDARA maalumu ya mali za Waqfu, ambayo aghalabu huwekwa chini ya Uwongozi wa Kiongozi Mkuu wa Waislamu, kama Kadhi mkuu na wasaidizi wake.

    Wanazuoni wametaja masharti manne kuhusiana na uhalali wa waqifu ambayo ni: kuwepo kwa mali inayowekwa waqfu, mweka waqfu, wanao wekewa wakfu na tendo la kuweka waqfu.

    Mali inayowekwa waqfu ni lazima iwe na masharti manne yafuatayo:

    1. Iwe na uwepo unaohisiwa ambayo imehusishwa na kuonekana kimwili. Kwa mujibu wa sharti hii, hatuwezi kuweka waqfu mali ambayo iko kwa mtu mwingine, au nyumba ambayo haipo, au bado kujengwa. Lakini inazungumziwa katika waqfu huo.
    2. Iwe ina uwezo wa kumilikika kisheria (iwe inahisabiwa ni mali kisheria). Kwa mujibu wa sharti hii, kwa mfano, hatuwezi kuweka waqfu danguro, au nyumba ya pombe, au shamba la mizabidu kwa kutengeneza pombe.
    3. Iweze inawezekana kutumiwa manufaa yake bila mali hiyo kutalifika. Kwa mujibu wa sharti hii, hatuwezi kuweka wakfu pesa; kwani kutumia manufaa yake kunamaanisha kutalifika na kumaliszika kwa mali yenyewe.
    4. Iwezekane mali hiyo kuchukuliwa kutoka kwa mweka waqfu. Kwa hivyo, mwekaji waqfu hawezi kuweka waqfu mali ya mtu mwingine; kwani kuchukua mali hiyo ni haramu.

    MUWEKA WAQFU

    Muweka waqfu awe amebaleghe, awe amepevuka kiakili; si hamnazo, na pia awe na mamlaka ya kutumia mali yake.

    WANAO WEKEWA WAQFU

    Anaye wekewa waqfu lazima awepo, awe mtu au watu mahususi, na kuwekewa waqfu kwake isiwe haramu. Kwa mujibu wa masharti haya, haiwezekani kuweka waqfu kwa mtu ambaye hajazaliwa. Pia haiwezekani kuweka wakfu kwa majambazi na makafiri wapinzani; kwani kuwawekea waqfu kama hao ni haramu.

    TENDO LA KUWEKA WAQFU

    Tendo la kuweka waqfu ni halali iwapo lina masharti yafuatayo:

    1. Kudumu; yaani, waqfu haupaswi kuwa na muda maalumu. Kwa hivyo, kuweka wakqfu kwa muda maalumu, si sahihi. Pia kuweka waqfu kwa mtu maalum si sahihi; kwani kwa kifo chake, wakfu huisha na kusimama.
    2. Nia amilifu shikamanifu itendekayo bila ya kuchelewa; yaani, haiwezekani kupitisha maneno ya kuweka wakfu (nia) kwa ajili ya kuweka waqfu mali katika siku zijazo (kwa mfano, mwanzoni mwa mwezi iingie kwenye waqfu).
    3. Kuchukua mali; Yaani mpaka pale ambapo kitu kilichowekewa waqfu kitakuwa bado hakijachukuliwa kutoka kwa mwakifi, wakfu huo utakuwa bado haujafanyika, kitu hicho kinahisabiwa kuwa bado ni mali yake.
    4. Kutoka nje ya umiliki wa mweka waqfu; Kwa mujibu wa sharti hii, mtu hawezi kuweka waqfu mali yake kwa ajili yake mwenyewe.

    VITABU VYA KUSOMA ZAIDI KUHUSU MAUDHUI YA WAQFU**

    1. بداية المجتهد ونهاية المقتصد
      لإبن رشد الأندلسي
    2. مداد الحرف في احكام الوقف
      تأليف د عاصم محمد الغامدي‎
    3. فقه السنة
      السيد سابق (المجلد الثالث)
    4. مصادر الوقف في القديم والحديث
      سليمان بن عبد الكريم الجاسر
    5. الوقف العقاري في الشريعة ألإسلامية
      سليمان بن عبد الكريم الجاسر
    6. الجامع لأحكام الوقف والهبات والوصايا الجزء الأول
      الدكتور خالد بن علي بن محمد المشيقح
    7. المبدع في شرح المقنع
      ابن مفلح – أبو إسحاق برهان الدين بن محمد بن عبد الله الحنبلي
    8. من مصادر أحكام الوقف
    9. أبو سليمان، عبد الوهاب إبراهيم محمد
    10. مدونة أحكام الوقف الفقهية
      الأمانة العامة للأوقاف – الكويت

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    Limejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAMBO YAKO MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887, KUPITIA WHATSAP TAJA MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA
    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • Nimeulizwa NANUKUU:-

    Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh Sheikh. Samahani, naomba ufafanuzi kuhusu STOCKS, BONDS & MUTUAL FUND katika uislamu. Je, inaswihi kuwekeza kwa njia hizo? Natanguliza shukran

    Nimeshajibu Suala hilo , hili hapa jibu langu!

    NINI HUKUMU YA BIASHARA YA HISA KATIKA UWISLAMU

    Nimeulizwa, NANUKUU:-
    Eti shekh vipui masuala ya hisa katika Uwislamu. Ni halali?

    JIBU
    BISMILLAH!

    Naam inajuzu kununua hisa halali katika jambo halali lenye faida halali, na ununuzi wa namna hiyo unaitwa شركة العنان Sharikat al-‘Inan: Yaani ushirika wa mtaji, ambapo watu wawili au zaidi ya wawili wanatoa mtaji wa kununua mali maalum na halali, ambayo inaweza kugawika katika mfumo wa hisa: ama mali yenyewe inaweza kugawika, au faida\pato la mali hiyo- ambalo linaitwa مرابحة =Murabaha\mrabaha, linaweza kugawika, na lazima kinachonunuliwa kiwepo au kijulikane aina yake (haijuzu kununua hisa ya mali isiyojulikana na wala haipo); mfano kununua hisa za umiliki wa nyumba, gari fulani au ya aina fulani, bidhaaa maalum za biashaara, kama duka la kuuza bidhaa maalum, au hoteli ya wageni, ect., ect. Ilimradi pato lake au faida yake itokane na biashara halali, na igawiwe kwa utaratibu halali. Inajuzu, na hakuna junah.

    Na kila mshirika au kila mwanahisa atalipwa hisa maalum=mrabaha maalum, kila baada ya muda fulani wa kukusanya mapato, na yeye atakuwa na umillki wa hisa inayowiana na mchango wake katika mtaji wa kununua mali hiyo, na awe na uhuru wa kuuza hisa yake wakati wowote.
    Na iwapo patatokea hasara, basi washirika wote watapata hasara, vile vile kulingana na mchango wao katika raslimali ya biashara hiyo. Hivyo, siyo kugawana faida tu, bali watabeba hasara vile vile, kila mmoja kwa mujibu wa kima cha mchango wake katika raslimali. Hakuna junaha kufanya biashara ya aina hiyo, kwa mtindo huo na kwa masharti hayo.
    Na asili ya yote haya ni kuwa sura zote hizo ni biashara na biashara ni halali katika Uwislamu: أحل الله البيع وحرم الربا

    Hivyo, huwezi kununua hisa za kuunda gari lisilojulikana hata michoro yake; wala hisa za kujenga danguro, wala jumba la kuchezea kamari, au mtaji wa mashindano ya kamari au bahati nasibu, wala ukulima wa zabibu za kutengezea mvinyo, wala ukuwadi wa kutunza au kuchuuza malaya, ect., ect., wala mtaji wa kukopesha kwa riba, ect. ect. Yaani hakuna ubiya katika haramu.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم

    Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • Nimeulizwa, NANUKUU:-

    Masheikh naomba mwongozo katika Hili:-

    Kumeibuka kadhia ya kupima vinasaba vya damu kwa mwanamme Na mwanamke wanaotarajia kufunga ndoa. Ni kwa lengo la kuthibitisha kama wanaweza kupata watoto, au kupata watoto wenye afya njema kupitia sampuli Za dam zao. Iwapo dam zao hazitaendana, basi hapo ndoa haitakuepo. Je Jambo hili linajuzu kisheria?’

    Wengine wameongongeza Na kipengele Chu kuangalia kama mmoja Wapo WA wanaotarajia kufunga ndoa,ana magonjwa ya kurithi au laa
    Haya yote Ni kupitia vipimo. Je sheria ya kiislam inasemaje?’

    JIBU
    BISMILLAH!

    Hakuna Junaha. Ni hiyari ya watu wawili husika.

    Mtume صلى الله عليه وسلم
    amesema:
    تزوجوا الودود المولود…
    “Oweni wanawake watiifu, wapole wenye huruma na wazalifu: kwani mimi nitajivunia wingi wenu, mbele wa watu wengine, SIKU YA KIYAMA.”

    Yaani CHAGUWENI MNAO TAKA KUWAOWA, KWA KUCHUNGUZA ASILI ZAO TOKEA TABIA ZA MAMA ZAO, DADA ZAO, NA NDUGU ZAO WA FUKO LA UZAZI, KWA UPANDE MMOJA, NA KUANGALIA HULKA ZAO, KWENYE NDOA ILIYO TANGULIA.

    HIYO NDIYO TUNAYOITA HII LEO DNA

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎

    من السيد عبدالقادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم

    Imejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    Kutoka Masuali na Majibu: Nimeulizwa, NANUKUU:– yanayo jibiwa kila siku kwenye kumbi za Darasa za Mitandaoni, za Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aalish- Shaykh Abi Bakr bin Salim.‎

    JIUNGE KWENYE MOJAWAPO WA KUMBI ZA SAYYID ABDULQADIR KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, NA MAHALI ULIPO, KWENDA NAMBA 0786887887 KUPITIA WHATSAP TU!

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • JE INAJUZU KUFUNGA NDOA KWA NJIA YA SIMU

    Nimeulizwa, NANUKUU:-‎

    ‎“Jaman naombeni mnisaidie kitu.CLeo ninafura napia ninahuzuni.Cku yaleo ‎ninafuraha kwasababu nimeingia ktk ibada ya ndoa ‎
    Ninahuzuni kwasababu watu wanaipingia ndoa yangu wanasema haiswihi ‎Kisa mm nipo oman alienioa yupo America. Ndoa imefungwa Tanzania ‎naombeni ufafanuz juu yahili nikweli cna ndoa ?”‎
    NB. Muulizaji ametoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala lake hilo, ambao ‎umenisaidia kuelewa siyo tu mazingira ya ndoa yenyewe, bali pia utaratibu ‎uliotumiwa kufungisha ndoa hiyo. Maelezo yako yote, hata hivyo, ‎yanaelekea kuuliza kwa ufupi: Je nini hukumu ya kufunga ndoa kupitia ‎mawasiliano ya simu?‎

    JIBU

    BISMILLAH

    Hili ni suala la enzi zetu hizi, si suala la hata nusu karne iliyopita. Hivyo, ‎tunazungumzia wanazuoni wa zama zetu za mawasiliano ya simu na intaneti, ‎na mawasiliano ya papo kwa papo, iwe ya sauti, ya sura au ya sura na sauti.‎
    Kabla ya kujibu hitimisho la Suala lenyewe, hata hivyo, napenda kutoa ‎maelezo yafuatayo.‎

    Ndoa ni chanzo cha fungamanisho takatifu baina ya wanandoa wao kwa wao ‎na baina yao na jamii yao, kwa mujibu wa Sharia za Ndoa katika Uwislamu.‎
    Hivyo, ndoa ina nguzo zake, masharti yake, na maadili yake. Ikikosekana ‎nguzo moja tu, basi hakuna ndoa. Ndoa ni batili. ‎
    Ikikosekana sharti moja tu, basi ndoa ni fasidi=imeharibika, imeingia dosari; ‎lazima dosari hilo liondolewe ili ndoa iweze kusihi. ‎

    Na ndoa ina maadili ambayo yakikosekana ndoa imesihi ila ina walakini, au ‎haikufuata Sunna. Ila ndoa ni sahihi.‎

    Nguzo za ndoa ni TANO: 1. KUWEPO Bwana harusi Mwislamu au ‎Mwakilishi wake halali, kwa mujibu wa sharia za uwakala; 2. Kuwpo Bibi ‎Harusi (siyo binti atayezaliwa, au akishazaliwa, au binti yangu anayeishi nchi ‎fulani – bwana harusi hamjuwi, mashahidi hawamjui, au hajulikani yupo ‎wapi ) 3.Kuwepo Walii wa mke kwa mujibu wa Sharia za uwalii; 4. Kuwepo ‎Mashahidi wawili, Waislamu, waadilifu, watu wazima, wenye akili zao ‎timamu, si viziwi, si vipofu, si mabubu, a wenye kuelewa lugha inayotumiwa ‎kufungisha ndoa, na wanao wajua au kuwatambua wanandoa, au familia za ‎wanandoa (sio watu waliookotwa njiani ti. au kupatikana msikitini tu, na ‎kuombwa washuhudie kufungwa ndoa, ilhali hawawjuwi wenye kuoana), 5. ‎الصيغة‎ Tamko wazi wazi la kuozeshwa mtu fulani na kukubali kumuoa ‎mwanamke huyo. Yaani :‎‏ زوجتك فلانة بنت فلان … قبلت نكاحها وتزويجها‎ ‎
    Dosari lolote lenye kuvuruga sifa za mojawapo ya nguzo hizo, linabatilisha ‎ndoa; hakuna ndoa, kabisa.‎

    Masharti ya ndoa ni saba: ‎
    ‎1. Kujulikana wanandoa, kwa majina yao, koo zao, na sifa zao. Haijuzu ‎kusema: “Nimekuozesha binti yangu”, ilhali ana zaidi ya binti mmoja. Hivyo, ‎lazima aainishwe kinaganaga binti gani, na binti mwenyewe awepo, kwa ‎maana yuhai na anajulikana kupindukia kujulikana na baba yake na mama ‎yake. Siyo mwenye kujulikana kwa mama na baba wazazi tu; watu wengine ‎hawamjui. Hivyo, awepo na ajulikane, hasa kwa mashahidi.‎
    ‎2. Papatikane, hasa kwa mashahidi, ridhaa ya wanandoa, khasa mwenye ‎kuolewa, hata kama ni mwanamwari. Akikataa au akipinga hakuna ndoa. ‎Inaingia hapa, vile vile, ‎كفاءة‎ uwiano au ulingano wa wanandoa, isipokuwa ‎wakiridhiana wenyewe kwa wenyewe kuoana au kuozeshwa kama walivyo.‎

    ‎3. Pawepo na Walii wa upande wa mwanamke; akiwa mwanamwari, basi ‎Baba yake mzazi, na kwenda juu. ‎
    Mtume ‎ﷺ‎ amesema: ‎‏”لا نكاح إلا بولي” [رواه أحمد وأبو داود] ‏‎ “Hakuna ndoa pasi na ‎kuwepo walii.” Ameipokea Abu Daud na Ahmad.‎
    Na amesema: ‎
    ‏أيما امرأة نكحت بغير إذن وليها فنكاحها باطل. فنكاحها باطل. فنكاحها باطل” رواه أحمد وأبو داؤد ‏
    ‎“Mwanamke yeyote atayejiozesha pasi na kupitia kwa walii wake basi ndoa ‎yake ni batili, ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili.” Ameipokea Abu Daud. ‎‎[Hivyo, hii ni mojawapo wa dalili ya kutosihi ndoa ya mut‘a =ndoa ya muda]‎

    ‎4. Ndoa hiyo ishuhudiwe na mashahidi wawili, Waislamu, waadilifu, wenye ‎kusikia, kuona, na uwezo wa kusema (si viziwi, si vipofu, si mabubu), ‎waliokwisha balighi, wenye kuwajuwa wanandoa au kujuwa uwepo wa ‎wanandoa hao. Mtume ‎ﷺ‎ amesema: ‎
    لا نكاح إلا بولي وشاهدي عدل” [رواه ابن حبان والبيهقي وصححه الذهبي]‏‎. ‎
    ‎“Hakuna ndoa pasipo kuwepo walii na mashahidi wawili, wanaume ‎waadilifu.” Ameipokea Ibn Hibban, Bayhaqi na Adh-dhahabi…‎

    ‎5. Mahari yatajwe wazi wazi, mbele ya mashahidi: kiasi gani, yamelipwaje, ‎ect., ect. Yasipotajwa kwa makusudi ndoa fasid , imeharibika, na ikisahauliwa ‎kutajwa basi ‎مهر المثل‎ mahari yaayoweza kutolewa kwa mwanamke kama ‎huyo. Kwa maana nyengine, mahari ni lazima, tena ni mali ya Biharusi, ‎pekee, na kuyataja ni sharti, yasipotajwa basi ‎مهر المثل‎ . Mahari si gharama za ‎ngoma, wala sherehe za harusi. Ni mali ya Biharusi, isipokuwa akiridhia ‎kuyatoa kumpa amtakaye kwa lengo alitakalo la halali.‎

    ‎6. Pasiwepo kizuizi chochote, kati ya wanandoa, kinacho wazuwia kuoana: ‎Kama 1. Nasaba ya damu -Ukoo; 2. Ukwe; 3. Udugu wa ziwa; 4. Tofauti ya ‎dini ya mwanamume, au umajusi wa mwanamke; 5. Mwenye kuolewa asiwe ‎kwenye Eda ya mtaliki wake, au ya mume aliyefariki, na 6. Pasiwepo mke ‎mwenza ambaye ni dada wa anayetaka kuolewa. Ndoa haisihi; mpaka ‎kizuwizi kiondoke, kama ni kizuwizi cha kuweza kuondolewa basi ‎kiondolewe kwanza: mfano wa tofauti ya dini ya mume kwa mwanamke ‎Mwislamu, au umajusi wa mwanamke muolewa, ect., ect.‎

    ‎7. Wahusika wote waliotajwa kwenye nguzo za ndoa, wawepo mahali ‎pamoja, wakiwa na sifa zao kamilifu: Sharti hili, linaitwa ‎إتحاد المجلس‎ yaani ‎ndoa ifanyike mbele ya watu hao, mahali pamoja, wakiwa na sifa zao ‎kamilifu. Ikikosekana sifa, basi itimizwe kwanza. Na sharti hili ndio ‎linalohusu zaidi ufungaji wa ndoa, kupitia njia za mawasiliano ya simu, vile ‎wahusika wapo nchi mbali mbali, hawapo pamoja kwenye majlisi moja, kwa ‎wakati mmoja. Ikikosekana sharti hili au sharti lolote miongoni mwa masharti ‎tuliyoyataja, basi ndoa haijuzu. Ndoa ni fasidi, imeharibika, yaani haina ‎uhalali, isipokuwa ikirekibishwa kasoro hiyo. Vengunevyo ndoa imeharibika. ‎

    Ama maadili na sunna za ndoa, ni mengi, miongoni mwake kualika watu wa ‎nyumbni na majirani, kusherehekea kwa dufu; kuitangaza ndoa katika jamii; ‎kuandaa karamu, pasi na isirafu wala kujioesha, kusaidia samani za biharusi, ‎ect., ect. ‎

    Suala la kujiuliza, katika muktadha wa Swali lilioulizwa, ni hili.‎
    Je ndoa iliyofungwa kwa njia ya simu, au mawasiliano ya mitandao, kama ‎intaneti na kamera-mubashara, vile wahusika wapo nchi mbali mbali, ‎inasihi?‎
    Au, Je nguzo za ndoa na masharti yake yote zinaweza kupatikana kupitia njia ‎ya simu, au mawasiliano ya mitandao au kamera za moja kwa moja? ‎

    Wanachuoni wametofauiana kuhusu kujuzu au kutokujuzu ndoa iliyofungwa ‎au inayotakikana kufungwa kupitia mojawapo wa njia hizo.‎

    Wapo wanaosema, moja kwa moja kuwa haijuzi, na wapo wanasema ‎inajuzu, laini kwa masharti maalum, na hawa ndio wengi, hasa katika zama ‎zetu hizi, ambapo uelewa wa mawasiliano ya simu na intaneti, umezidi ‎kueleweka zaidi, iwe kwa sifa njema au kwa sifa mbaya. Wenye kuzingatia ‎upande wa sifa mbaya wanasema ndoa haijuzu. Wanaoangalia upade wa sifa ‎njema, wanasema inajuzu, lakini kwa mashartti maalum.‎

    Wanao pinga moja kwa moja, wanasema kwamba Ndo ni ahadi nzito sana, ‎ni ahadi takatifu inayochukuliwa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kuhalalisha ‎tupu za wanandoa na kuhalalisha vizazi vitavyo tokana na ahadi ya kufunga ‎ndoa hiyo; hivyo si jambo la kulichukulia kijuu juu tu, kupitia vivuli vya ‎watu ambao yaweza kuwa ni kweli vivuli vyao, lakini yawezekana vile vile – ‎tena ni uwezekano mkubwa sana, kuwa SI vivuli vyao =si picha zao halisi=, ‎wala si sauti zao halisi, ni vitu vilivyo igizwa na watu waovu, kwa makusudi ‎kwa kubabaisha watu, au kuchakachuliwa, tu, na wahadaifu, wachache wa ‎uadilifu na wenye nia mbaya dhidi ya Uwislamu na taasisi zake. ‎

    Na zaidi mawasiliano ya aina hiyo, hayawezi kuthibitisha sifa ziliofichika ‎mwilini mwa wanaotaka kuoana, hasa mume, kama uadilifu, uwislamu, ‎ufuataji wa sharia za Uwislamu, na kadhalika. Mtume ‎ﷺ‎ ameashiria kuwa ‎‎“akikujieni msiye ridhia dini yake msimuozeshe.” Utatambuaje sifa hiyo ‎kupitia simu na kamera? ‎
    Mashahidi wanaweza kuhadaiwa, au hata kutokuwajua sawasawa wanandoa, ‎zaidi ya kuambiwa tu kuwa yule ndiye Fulani, na huyu hapa kwenye picha ni ‎Fulani, na unayoisikia ni sauti ya fulani, ect., ect. Hivyo, ndoa ya njia hiyo ‎haisihi, hasa tukielewa kuwa kunakosekana vile vile sharti la ‎إتحاد المجلس‎ . ‎
    Huu ndio msimamo wa wanazuoni wanaoitwa muhafidhuun, ambao ‎hujulikana kwa majina mbali mbali, meingine wanajiita wenyewe, kama vile ‎Answarussunna, Masalafi, na mengine wanapachikwa kwa hulka yao ya ‎ufuataji wa mtu fulani, kama Mawahabi na kadhalika. Na huu ndio msimamo ‎rasmi wa Kamati ya Kudumu ya wanazuoni wa Saudi Arabia, ambayo ndio ‎wasemaji rasmi wa utawala wa Saudi Araib, na ambyo ndani yake wamo ‎watu kama Sheikh AbdulAziz bin Bazi, Sheikh Abur-Rzaaq ‘Afifi, ‘Abdallah ‎bin Manii‘ na ‘Abdullah bin Ghadyaan. Kwa ufupi, ni msimamo wa ‎washadidivu wengi, ndani ya Saudi Arabia na nje yake.‎

    Wacnachuoni, wengi, hata hivyo, wanakubali kufungwa ndoa kupitia njia za ‎mawasiliano ya moja kwa moja, kupitia simu, kamera mubashara, mitandao ‎ya intaneti na kadhalika kwa masharti maalum. Miongoni mwake, ni:‎
    ‎1. Kuwezekana, KWA UHAKIKA, kukutana, kwa wakati mmoja, kwenye ‎mawasiliano hayo: ‎إتحاد المجلس‎, watu wasiopugua wane, ambao ndio nguzo za ‎ndoa, kupitia mawasiliano hayo na hivyo kupatikana ‎‏ إتحاد المجلس‎, kwa njia ‎hiyo, pasipo na shaka wala wasiwasi au udhanifu. Nao ni : 1. Mume, 2. Walii, ‎na 3. Mashahidi wawili waadilifu, na nyongeza ya Muozeshaji rasmi, ‎mwenye kibali cha kufungisha ndoa za Kiislamu, ili ndoa hiyo iweze ‎kusajiliwa rasmi na kutolewa shahada ya ndoa itayotambuliwa na ‎kuheshimiwa katika nchi zote walizopo wahasuika wakuu wa ndoa hiyo, ‎anayeitwa: ‎المأذون‎ yaani mwenye kibali cha kuozesha, kama Qadhi na ‎kadhalika. Watu wote hao wawe na sifa zao kamili, kila mmoja kwa sifa ‎zake za lazima, ili kufungisha au kufungishwa ndoa, wakati wa kufungishwa ‎ndoa hiyo; yaani wakati mmoja, mahali pamoja kupitia mawasiliano hayo ‎rasmi ‎

    Hivyo, awepo Muozeshaji rasmi, wa kuongoza taratibu za ndoa hiyo, kwa ‎mujibu wa Sharia za Kiislamu, na kwa mujibu wa taratibu rasmi za kutambua ‎usajili wa ndoa hiyo, ni miongoni mwa masharti ya kufunga ndoa kupitia ‎mawasiliano ya simu. Yakikamilika masharti hayo, hakuna tatizo; ndoa ni ‎sahihi, ilimradi itafungwa kwa masharti hayo, na itafungwa na muozeshaji ‎rasmi kwa taratibu rasmi za Kiislammu. ‎

    Hivyo, ikiwezekana, kwa uhakika, kukutanishwa wote hao, kupitia njia hiyo ‎ya mawasiliano, pasipo shaka wala wasi wasi kuhusu utambulisho sahihi wa ‎wanandoa wahusika, kuwa ni wao wenyewe, wafungaji wa ndoa ni wao, na ‎sura ni zao, na sauti ni zao, na kila mmoja ana sifa zake za lazima, kwa ‎shughuli hiyo, na kweli wapo huko walipo, wakati wa kufungishwa ndoa ‎hiyo, basi ndoa inaweza kufungwa kupitia utaratibu huo; venginevyo haijuzu. ‎

    Huu ni msimamo wa majopo mbali mbali ya wanazuoni wa Kiislamu, ‎pamoja na majopo ya Mabaraza ya Fatwa ya nchi mbali mbali za Kiislamu, ‎kama wanachuoni wa Misri, Baraza la fatwa la Al-Azhar, Majopo ya Fatwa ‎ya mataifa ya kama ya Ghuba la Arabuni, Malaysia, Indonesia, Mashariki ya ‎Kati, Mataifa ya Kiislamu ya Afrika ya Kaskazini, na wanazuoni wengi, ‎wanao angalia mawasiliano ya simu intaneti na kamera-mubashara kuwa ni ‎mawasiliano yanayoweza kuaminika, iwapo hatua zote zitachukuliwa ‎kuhakikisha usalama wake. Hakuna junaha. ‎

    Hata baadhi ya wanakamati ya kudumu ya wanazuoni wa Saudi Araiba, ‎timbuko na zizi la Mawahabi na washadidivu na wang’ang’anivu, ‎wamekubali uhalali wa kufungesha ndoa kwa njia hizo za mawasilano, kwa ‎masharti hayo na kwa tartibu hizo,. Mmoja wao ni Sheikh wangu, Sheikh ‎Abdul Aziz bin Baz ‎رحمه الله ‏‎ . Wengine, hata hivyo, wameshikilia msimamo ‎wao uleule wa ushadidivu na ukakamavu, miongoni mwao Ibn Uthaymin, ‎Fawzan, Ubaykan na wengine. ‎

    Kwa ufupi, inajuzu kufunga ndoa kupitia njia za mawasiliano ya simu na ‎kadhalika, endapo kuna dharura ya kufanya hivyo, na endapo kutakuwepo ‎uhakika wa kutokuwepo uhadaifu, uigizaji, uchakachuaji au ubabaishaji, iwe ‎kwa makusudi au kwa kuingiliwa na wenye nia mbaya na Sharia za ‎Kiislamu, kuhusu ndoa, na wahusika wote wakaweza kukutanishwa kwa ‎wakati moja, kwenye chombo kimoja cha mawasilano, na kila mmoja akwa ‎na sifa zake za lazima, wakati wa kufung ndoa hiyo kwa njia hiyo. ‎INAJUZU. Venginevyo haijuzu. ‎

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم‎ ‎

    Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au ‎kuongeza ‎chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na ‎kwenye ‎Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la ‎kusambaza na ‎kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • NINI HUKUMU YA KUVAA HIRIZI AU KINGA

    Nimeulizwa, NANUKUU: ‎

    ‎“Habib Abdulqadir nina suala. Nini Hukumu ya kuvaa hirizi, au Kinga? Na ‎Nini hukumu juu ya mwenye kutengeneza Hirizi hizo? Naomba ufafanuzi wa ‎kina, maana ni tabia iliyozagaa sana katika jamii zetu.”‎

    JIBU

    BISMILLAH

    Neno “Hirizi” lina maana pana, ila maana zote zinalenga katika ‎kumaanisha KINGA, na hivyo hutumiwa kwa kitu chochote kile ‎kinachoaminiwa kuwa ni kinga ya jambo baya, au jambo lisilotakiwa. ‎

    Kwa upande wa lugha, hirizi ni hifadhi au kinga ya jambo fulani. ‎Neno jengine linalotumiwa ni ‎حجاب‎ hijab, ‎طلاسم‎ twalsam-twalasim,na ‎عزيمة‎ ‎‎‘aziima-‘aza’im yote yana maana moja ya kukinga, kulinda, kunusuru, ‎kusitiri, kuchunga na kadhalika. ‎

    Na ni kutokana na maana hizo ndimo tunapata neno hijabu ‎linalotumiwa kwa upande wa Sharia, kumaanisha vazi la kujisitiri, kwa ‎Kiswahili ni Buibui, au kwa lugha ya siku hizi, ‘abaya. [ingawa hayo ‎yanayoitwa ma’abaya yamegeuzwa, siku hizi, kuwa ni vivutio zaidi kuliko ‎kuwa ni stara au hifadhi ya mwili ‎والله المستعان‎ ] ‎

    Kwa upande wa itikadi na imani, hata hivyo, tunapozungumzia Hirizi ‎neno hilo linamaanisha kinga ya zindiko ili usifikwe na jambo fulani. ‎

    Iwapo zindiko hilo ni la maandishi maalum, basi maneno mengine ‎yanayotumiwa –hata kwa Kiswahili- ni Talasimu, Azima, Hijabu, Zindiko ‎na Sihiri. ‎

    Lakini, iwapo zindiko hilo linahusishwa na kitu maalum, kuwa kina ‎nguvu za kukulinda na jambo fulani lisikufike, basi maneno yanayotumiwa, ‎katika Kiswahili, ni Kago, Ndumba, Tunguri, Ndonga na Kinga. Ni maana ‎hizo mbili: kinga ya maandishi na kinga ya kuamini kuwa kitu fulani ‎chenyewe kina nguvu za kukulinda na jambo fulani au kukulinda na kitu ‎fulani chengine, ndizo nitazozungumzia hapa.‎

    A)‎ Hirizi kwa maana ya kinga ya maandishi. ‎
    ‎ ‎
    Kuna maadishi ya aina mbili, yanayo tumiwa katika kuandika hirizi. ‎

    a)‎ Kwanza ni maandishi ya majina ya mashetani, majini au michoro ya ‎mazingaombwe ya shaghala-baghala, wakidai kuwa ni kiatu cha ‎Nabii Sulaiman, au Nyota ya kitu fulani, au sura za vitu maalumu, au ‎nambari maalumu, ect., ect. Hizi ndizo zinazoitwa Talasimu, na ‎Hirizi; kwa Kiarabu zinaitwa: ‎تمائم ‏‎ au ‎تولة‎. Hizi ni kufuru. Kiatu cha ‎Nabii Sulaiman si kinga wala si dawa ya kitu chochote; iweje mchoro ‎wake uwe kinga ya jambo lolote lile. Ubahalula. Uzandiki. Ujinga. ‎Ulanguzi wa wadanganyifu wa kuwaibia na kuwala wajinga. ‎Haramu kabisa, bali ni kufuru. Vile vile huitwa ‎رقيا الشيطان‎ au ‎رقي‎ tu.‎

    b)‎ Maandishi ya Qur’ani au Majina ya Mwenyezi Mungu na kadhalika. ‎Haya huitwa ‎حجاب الشرعي‎ au ‎الرقيا الشرعيHakuna junaha iwapo ‎maandishi hayo ni Aya za Qur’ani au Majina ya Mwenyezi Mungu, ‎kwa sharti kwamba pasiaminiwe kuwa MAANDISHI HAYO ndiyo ‎yanayo kukinga au kukulinda. Bali mwenye kukukinga na kukulinda ‎ni Mwenyezi Mungu aliyesema maneno hayo. Yaani unatumia Aya ‎za Qur’ani au Majina Matakatifu ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya ‎kutabaruku tu, ukiamini kuwa mwenye kukinga na kulinda ni ‎Mwenyezi Mungu, ‎

    Mwenyezi Mungu amesema, kuhusu Qur’ani: ‎

    ‏﴿وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِلْمُؤْمِنِينَ وَلا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلا خَسَارًا﴾ [الإسراء: 82]‏‎.‎
    Na tunateremsha katika Qur’ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa ‎Waumini. Wala hayawazidishii madhalimu ila khasara. (Al-Isra’, 17:82)‎

    Na amesema, katika Surat Al-An‘am, Aya ya 155:‎
    ‏﴿وَهَذَا كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴾ [الأنعام: 155]‏‎.‎

    Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na ‎mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemiwe. (Al-An‘am, 6:155)‎

    عن محمد بن عبد الرحمن بن أبي ليلى عن عيسى أخيه قال: دخلت على عبد الله بن عكيم أبي معبد ‏الجهني أعوده وبه حمرة فقلنا: ألا تعلق شيئًا؟ قال: الموت أقرب من ذلك، قال النبي صلى الله عليه ‏وآله وسلم: «مَنْ تَعَلَّقَ شَيْئًا وُكِلَ إِلَيْهِ (رواه الترمذي وإبن ماجه )‏

    Imepokewa kutoka kwa Abdurrhaman Ibn Abi Layla kutoka kwa Isa ‎kutoka kwa ndugu yake akisema: “Nilimtembelea Abullah bin Ukaym; Abi ‎Ma‘bad al-Juhaniyy, akiwa mgonjwa, akiwa amekaa na Hamza bin Abdil ‎Muttalib (Ami yake Mtume ‎ﷺ‎ ). Tukamwambie kwanini huvai hirizi ‎yoyote ile ya kujikinga? Akajibu kwa kusema: “Mauti yamesha nikaribia ‎zaidi kuliko kufanya hivyo. Na nimemsikia Mtume ‎ﷺ‎ akisema: ‎‎“Atayejifunga kitu (kama hirizi) ataachiwa nacho kimsaidie kama kinaweza ‎kumsaidia.” Ameipokea Tirmidhi na Abu Daud.‎

    Wanazuoni wameifasiri kuwa ukivaa kitu chochote kile, basi ‎utaachiwa wewe na kitu chako hicho kikusaidie kama kinaweza ‎kukusaidia; yaani utasokomezwa nacho. Hivyo, ukivaa maandishi ya Aya ‎za Qur’ani basi Mwenyezi Mungu hatokusokomeza kwa asiyekuwa yeye ‎akusaidie, bali atakusaidie yeye Mwenyewe, maana Qur’ani ni maneno ‎Yake, ambayo ameyaelezea kuwa ni dawa na tiba na rehema. ‎

    Kwa maana hiyo, atayevaa au kujitundikia Aya za Qur’ani basi ‎hawezi kuachiliwa na Mwenyezi Mungu asaidiwe na asiye kuwa Yeye; ‎lazima atamsaidia Yeye mwenyewe kumtibu, kumlinda na kumhifadhi. ‎Hivyo ndivyo walivyo fasiri wanazuoni wakubwa wakubwa wa Tafsiri za ‎Qur’ani, kama Imam Al-Qurtuby katika Tafsiri yake: ‎الجامع لأحكام الفرآن (10 ‏‏:320 )‏‎ . Wengine ni Twabary, Ibn Kathiir na wengine.‎

    عن عمرو بن شعيب عن أبيه عن جده: أن رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم قال: «إِذَا فَزِعَ أَحَدُكُمْ ‏فِي النَّوْمِ فَلْيَقُلْ أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّةِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ ‏يَحْضُرُونِ؛ فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ». قال: وكان عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما يعلمها مَنْ بَلَغَ من ولده، ‏ومَنْ لم يَبْلُغْ منهم كتبها في صك ثم علَّقَهَا في عُنُقِه رواه أبو داؤود والترمذي‎.‎

    ‎ ‎ Vivyo hivyo, imepokewa kutoka kwa Amr bin Shu‘ayb kutoka kwa ‎Baba yake kutoka kwa Bab u yake akisema: Amesema Mtume ‎ﷺ‎ : ‎Akishtuka mmoja wenu usingizini kutokana na ndoto mbya, basi aseme: ‎أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّةِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونِ؛‎ kwani hatosibiwa na kitu chochote, kile. Na amesema kuwa ‘Abdullah bin ‎Amr ‎رضي الله عنهما‎ alikuwa akiwafundisha dua hiyo watoto wake waisome ‎wanapo shtushwa na ndoto mbaya usingizini, na kwa wale ambao ‎walikuwa bado hawakubalighi, basi alikuwa akiiandika dua hiyo kwenye ‎karatasi na kuikunjakunja na kisha kuitundika shingoni mwa mtoto huyo.” ‎Ameipokea Abu Daud na Tirmidhi.‎

    Hivyo, kitendo cha Sayyidina ‘Abdullah bin ‘Amr ‎رضي الله عنهما‎ ‎kunukuu dua aliyofundisha Mtume ‎ﷺ‎ kujikinga na vitisho vya usingizini, ‎na kuiandika kwenye karatasi na kisha kuitundika karatasi hiyo kwenye ‎shingo ya watoto wake wadogo ni dalili kuwa inajuzu kuvaa hirizi ya dua ‎ya kumuomba Mwenyezi Mungu, pekee, na kama dua inajuzu, basi ‎Qur’ani inajuzu zaidi, maana Mwenyezi Mungu amesema kuwa Qur’ani ‎ni dawa, uponesho na rehema kwa Waumini. ‎

    Vivyo hivyo, wafuasi wakubwa wakubwa wa Maswahaba wa ‎Mtume ‎ﷺ‎ kama Ataa’, Mujahid na Sa‘id bin al-Musayyib ‎رضي الله عنهم‎ ‎walikuwa wakiwaandikie watu hirizi za Aya za Qur’ani na dua za Mtume ‎ﷺ‎ na kuwapa wazivae kama hirizi. (Muswannaf In Abi shayba, juzuu ya ‎‎3, kurasa 43 hadi 44)‎

    Imam Malik ‎رحمه الله‎ amesema: Hakuna junaha kuvaa hirizi za Aya ‎za Qur’ani. Msimamo huo umeelezewa vile vile na wanazuoni wakubwa ‎wakubwa, kama Ibn Hajar katika Fat-h al-Baary Sharh Swahih al-Bukhari, ‎juzuu ya 6, ukurasa 142, alipokuwa akifafanua makatazo ya Hadithi yenye ‎kukemea kuvaa hirizi za talasimu za maandishi yasiyokuwa Qur’ani ,kwa ‎kusema:‎

    هذا كله في تعليق التمائم وغيرها مما ليس فيه قرآن ونحوه، فأما ما فيه ذكر الله فلا نـهي فيه؛ فإنه ‏إنـما يجعل للتبرك به والتعوذ بأسـمائه وذكره .‏
    Makatazo yote haya ya hirizi za matalasimu ni kuhusu ‎maandishi yasiyokuwa Qur’ani au yasiyokuwa majina ya Mwenyezi ‎Mungu. Ama utajo (Qur’ani) wa Mwenyezi Mungu haukukatazwa; ‎kwani Qur’ani imefafanuliwa na Mwenuezi Mungu kuwa inajuzu ‎kutabaruku nayo na vile vile kujilinda kwa Majina Matakatifu ya ‎Mwenyezi Mungu. ‎

    Na kuna Hadithi nyingi sana zinazosema kuwa inajuzu kujizingua ‎kwa Aya za Qur’ani au dua maalumu za kuzingua, ambazo ametufundisha ‎Mtume ‎ﷺ‎ . Na tofauti ya kuzingua na kujilinda, yaani hirizi ya maandishi ‎ya Qur’ani ni kwamba kuzingua ni tiba baada ya kufikwa na tatizo; vile ‎hirizi ni kinga usifikwe na matatizo; ila Aya ni zile zile, na maneno ni yale ‎yale ya Mwenyezi Mungu. Hakuna junaha.‎

    Kwa ufupi hakuna junaha kuandika au kuvaa hirizi za maandishi ‎ya Aya za Qur’ani, au dua za Majina Matakatifu ya Mwenyezi Mungu, au ‎hata dua zilizopokewa za kujilinda kutoka kwa Mtume ‎ﷺ‎ . Yaani dua ‎ambazo hamna ushirikina wowote ndani yake, na hivyo kutabaruku na ‎maneno ya Mwenyezi Mungu.‎

    Ama maandishi yoyote mengine, yasiyokuwa hayo ni haramu,, ‎kufuru na ushirikina. Na hayo ndiyo yale maandishi ya matalasimu ya ‎majina ya mashetani, majini, picha za mazingaumbwe mbali mbali, ‎michoro ya ramani, nyota, Mwezi, Jua,, na kadhalika, yote ni haramu, ‎kufuru, haijuzu hata kidogo. Ni talasimu za kishetani na kufuru. ‎Mwenyezi Mungu amesema: ‎

    ‏ وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ ‏السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ ‏فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ ‏وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا ‏بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ (البقرة 2 :102)

    _‏Nawakafuata yale waliyoyazua mashetani kuuzulia Ufalme wa Sulaiman. ‎Na wala Sulaiman hakukufuru, bali mashetani ndio walio kufuru, ‎wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, ‎Haatuta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha mtu ‎yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru! ‎Wakajifunza kutoka kwa hao wawili yale ya kumtenganisha mtu na mkewe. ‎Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa utashi wa Mwenyezi Mungu. Na ‎wanajifunza yanayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua ‎kwamba aliye chagua haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na ‎hakika ni uovu mno walio jiuzia nafsi zao; laiti wangelijua. (Al-Baqara, ‎‎2:102)‎_Na Mtume ‎ﷺ‎ amesema kuwa mazinguo ya talasimu za mashetani, na ‎Shanga, Tunguri na kadhalika ni ushirikina.‎

    إن الرقى والتمائم والتولة شرك “. رواه أحمد و أبو داود
    ‎“Mazinguo ya mashetani, Kago na Tunguri ni ushirikina.” Ameipokea ‎Ahmad na Abu Daud.‎

    B)‎ Kinga nyengine, ambazo si za maandishi, ni kinga zinazoaminiwa ‎kuhusiana na vitu mbali mbali, viwe venye roho au au visivyo na ‎roho, kwa imani ya kuwa vitu hivyo, vyenyewe, vinakulinda na ‎kukuhifadhi. Yaani itikadi potofu kuhusu vitu mbali mbali kuwa vina ‎nguvuza kukulinda jambo fulani, au kukupatia manufaa fulani. ‎Kinga za aina hii, kwa Kiarabu huitwa kwa majina mbali mbali, kama ‎Tamaaim, Tiwala, Khazar, Wada’, na kadhalika, ambazo kwa ‎Kiswahili ni sawa na maneno Kago, Ndumba, Tunguri, Ndonga, ‎Zindiko, Fingo, Hijabu, Azima na kadhalika, Kinga za aina hii ni ‎ushirikina na ukafiri uliokubuhu; maana ni kumtupilia mbali ‎Mwenyezi Mungu kama alivyesema:‎

    ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنْكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِنْكُمْ بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ ‏‏(النحل 16 : 54) ‏
    Na anapo kuondosheeni madhara, mara kundi moja miongoni ‎mwenu, linamshirikisha Mola wao (An-Nahl, 16:54)‎

    Na badala yake kugeukia kuamini kuwa Kago hizo zina nguvu ya ‎kuwalinda, kukuhifadhi na kuwakinga na jambo lolote lile wasilo litaka ‎liwafike, iwe kujikinga na maradhi, husuda, kijicho, shetani, jinni na ‎kadhalika, au viwanufaishe na jambo lolote lile, kama kukupa utajiri, ‎kwaharaka, biashara ichangamke, au kupasi mtihani na kadhalika. Ni ‎ushirikina. Vyote hivyo ni Shirk. Haramu. Kufuru. ‎
    ‎ ‎
    Mtume ‎ﷺ‎ amesema kuhusu Talasimu na Kago kwa aina zake zote:‎

    ‏((من تعلق تميمة فلا أتم الله له، ومن تعلق ودعة فلا ودع الله له، ومن تعلق تميمة فقد أشرك))[رواه ‏‏ أحمد وغيره )‏
    Ataye vaa kinga basi Mwenyezi Mungu asimkinge. Na atayejivesha hirizi ‎‎(tamiima) amemshirikisha Mwenyezi Mungu,” Ameipokea Ahmad na ‎wengine. ‎

    عمران بن حصين “أن النبي صلى الله عليه وسلم أبصر على عضد رجل حلقة – قال: أراه قال: من ‏صفر -، فقال: ويحك ما هذه قال من الواهنة قال: أما إنها لا تزيدك إلا وهنا، انبذها عنك، فإنك لو ‏مت وهي عليك ما أفلحت أبدًا”2. ورواه ابن ماجة‏

    Imepokewa kutoka kwa ‘Imraan bin Al-Huswayn ‎رضي الله عنه‎ ‎akisema: Mtume ‎ﷺ‎ alimuona mtu amejifunga kikuku mkononi- nadhani ‎cha shaba- akamuuliza: Ndiyo nini hiki? Akamibu kinaniondolea udhaifu. ‎Mtume ‎ﷺ‎ akamwambia: Kwa kweli hakikuzidishii kitu ila udhaifu tu. ‎Kivue ukitupilie mbali! Kwani lau kama utakufa na kikuku hicho kipo juu ‎ya mwili wako basi hutaweza kuokoka hata kidogo.” Ameipokea Ibn ‎Maja na Ahmad. ‎

    عن عقبة بن عامر الجهني “أن رسول اللّه صلى الله عليه وسلم أقبل إليه رهط فبايع تسعة وأمسك ‏عن واحد. فقالوا: يا رسول اللّه، بايعت تسعة وأمسكت عن هذا؟ قال: إن عليه تميمة فأدخل يده ‏فقطعها، فبايعه. وقال: من علق تميمة فقد أشرك”.( رواه أحمد والحاكم )‏

    Imepokewa kutoka kwa ‘Uqba bin ‘Amir al-Juhaniyy ‎رضي الله عنه‎ ‎akisema: Alikuwa Mtume ‎ﷺ‎ na kikundi cha watu 10. Basi akapokea Bay’a ‎‎(Ahadi ya Utiifu) kutoka kwa watu tisa, lakini akajizuwia kumpa mkono ‎mtu mmoja. Wale watu wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ‎umekubali Ahadi ya watu tisa, lakini umemkatalia huyu! Mtume ‎ﷺ‎ akasema: ‎Kwa sababu amevaa Kago. Basi yule mtu akaingiza mkono wake na ‎kuikata kamba ya ile Kago. Mtume ‎ﷺ‎ akampa mkono wa Bay’a, na kisha ‎akasema: Anayejivesha Kago amemshirikisha Mwenyuezi Mungu.” ‎Ameipokea Ahmad na Al-Hakim.‎

    Naam, hakuna junaha ikiwa una maradhi maalumu, kama upungufu ‎wa madini fulani,, mwilini, na madaktari wakakuambia kuwa unahitaji ‎kuongeza madini fulani mwilini mwako, na wakapendekeza kutumia dawa ‎maalumu, au kuvaa kitu maalumu kitacho kusaidia kupata hayo madini ‎unayohitajia, basi hakuna junaha. Maana hapo una matatizo ya upungufu ‎wa kitu fulani mwilini mwako na madaktari wamekupa njia ya kujitibu. ‎Huko si kuamini kuwa hicho ulichovaa ndicho kinacho kusaidia, bali ni ‎kuamini kuwa umepewa dawa ya matatizo yako ya kiafya. Ni sawa na ‎kuandikiwa virutubisho fulani mwilini, kama Vitamin C. Hakuna junaha ‎hapo.‎

    Kuna hadithi nyingi za kuharamisha kutumia vitu vyovyote vile kwa ‎imani kuwa vitu hivyo vyenyewe, ndio kinga, au hirizi inayo kulinda na ‎kukuhifadhi, au hata kukunufaisha kitu fulani. Miongoni mwa kago hizo, ‎za kishirikina, katika nchi zetu za Afrika ya Mashariki na kwengineko, ni ‎Makucha ya Simba, Kaure za pwani, Shanga, Mafupa ya wafu, Mafuvu ya ‎maiti, nywele za mkia wa simba au tembo, meno ya papa, au ya simba, ‎kucha za kima, meno ya sokwe, mafupa ya albino, ngozi ya albino, damu ‎ya hedhi (wanaita Limbwata), pembe za wanyama mbali mbali na ‎kadhalika. Vyote hivyo vinaingia katika jina la Kago, Ndunguri, Hijabu, ‎Pagao, Hirizi, Zindiko, Sihiri, Kinga, Fingo, Lindo na kadhalika na vyote ni ‎harmu, ushirikina na kufuru. Mwenye kuvaa ili vimlinde amekufuru. ‎Mwenye kuvitengeneza na kuwapa watu wavivae ili viwalinde amekufuru ‎maradufu. ‎

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم ‏

    Imejbiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza ‎chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye ‎Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • JE INAJUZU KWA MWENYE HEDHI KUSHIKA SIMU YAKE YA MKONONI AMBAYO NDANI YAKE MNA PROGRAM YA MUSAHAFU?

    Nimeulizwa, NANUKUU:-
    Assallam alleykum warahmatullah wabarakatuh

    Kuna swali Alhabib

    Huku niliko watu wanasoma Qur an wakiwa katika hedhi, ila wanasoma kwa simu, je’ hii inafaa ?

    JIBU

    BISMILLAH!

    Kusoma Qur’ani bila ya udhu, pasi na kuugusa MSAHAFU, hakuna mushkeli kwa maulamaa karibu wote.

    Sayyidina Umar alimkaripia Swahaba mmoja alimyemsaili kwanini anasoma Qur’ani mara tu baada ya Sayyidina Umar kutoka kwenda Haja. Alimjibu kwa kumwambia: “Na nani aliyekupa fatwa hiyo kuwa huwezi kusoma Qur’ani bila ya Udhu? Musaylama al-Kadh-dhaab?!! Ameipokea Malik katika Muwatta’.

    Hivyo, unasoma Qur’ani kimoyo moyo pasi na udhu. Hakuna junaha.

    Na kuna hadithi kadhaa swahihi kuwa hakuna ulazima wa kuwa na udhu kwa kusoma Qur’ani kutoka moyoni, au pasi na kuugusa msahafu. Hivyo hata mwenye Hedhi anaweza kusoma Qur’ani bila ya udhu, ilimradi haugusi MSAHAFU wenyewe moja kwa moja مباشرة. Na neno moja kwa moja, linamaansisha kuwa lau kama Msahafu umo ndani ya kitu chengine, kama sanduku, basi hakuna junaha kugusa au kubeba sanduku hilo. Hapana khilafu hapo hata kidogo. Unaweza kubeba sanduku lako la nguo ambalo ndani yake mna msahafu. Unaweza kubeba mkoba wako ambao ndani yake mna msahafu. Unaweza kuwa na msahafu kwenye mfuko wa wa kanzu, pasi na kuwa na udhu.

    Hivyo, unachotaka kukijibu wewe, mwenyewe, ni:-

    Je, Mobile iliyo na Qur’ani inafaaa kuigusa au haifai, na unapofungua programe ya Qur’ani ukaisoma, huku umeishika hiyo Mobile, unakuwa umeugusa msahafu au la.

    Kwa maoni na mtazamo wangu, hujagusa msahafu, na hivyo unaweza kusoma kutoka katika Mobile pasi na udhu.

    Dini ni nyepesi, ni sahala, ni nia ya msomaji, na khasa tukizingatia kuwa hakuna Ijmaa kwamba huwezi kuugusa Msahafu bila ya udhu. Swala hili, nimesha lijibu mwahala mwengine, katika ukumbi huu huu. Rudia huko.

    Hata hivyo, maimamu watatu Abu Hanifa, Malik na Shafi رحمهم الله wanasema huwezi kugusa msahafu -moja kwa moja- pasi na udhu. Kwao wao Udhu ni SHARTI la kugusa msahafu. NI SHARTI si FARADHI wala SI HARAMU. Yaani hakuna dhambi kuugusa pasi na udhu!

    Ni kutokana na hali hizo, na umuhimu wa faida kubwa zinazoweza kupatikana kwa kusoma Qur’ani kutoka kwenye SIMU, sioni junaha kusoma mwenye hedhi kutoka katika SIMU, ambayo SI MSAHAFU, bali ni chombo kilichokusanya mambo mengi, miongoni mwake ni PICHA za kurasa za msahafu, na SI MSAHAFU wenyewe. Haya ni kwa maslahi ya WOTE المصالح المرسلة. Na masilahi ya umma hutangulizwa mbele penye haja ya kufanya hivyo, kuliko kuyazuwia.

    وبالله التوفيق

    الحقير عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم

    Imejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chchote, na kuweka kwenye FB yako au kwenye WhatsApp na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.

    kcwajawema@gmail.com

  • **NINI HUKUMU YA KUGUSA MSAHAFU PASI NA UDHU

    Nimeulizwa, NANUKUU:-

    Nna suala Habib Abdulqadir. Nini hukumu ya kugusa msahafu pasi na udhu. Je inajuzu au haijuzu. Dalili ni nini?

    JIBU

    BISMILLAH

    Msahafu ni Kitabu cha maandishi juu ya kurasa yenye kuwakilisha matamshi ya Maneno ya Mwenyezi Mungu: Qur’ani.

    Na Qur’ani ni ile inayosomwa kutoka mdomoni, ndiyo maana ya neno Qur’ani. Inaposomwa Qur’ani, kwa sauti, ndipo inapokuwa yanasomwa maneno ya Mwenyezi Mungu, na ni wajibu kunyamaza kimya na kusikiliza usomwaji wa Maneno hayo Matakatifu.

    Kwa maana hiyo, Qur’ani haiwi Qur’ani mpaka isomwe, itamkwe. Qur’ani haiwezi kuguswa kwa mkono, kama unavyo gusa msahafu. Na ikisomwa basi Mwislamu anapaswa kufanya mambo mawili.

    1. Kunyamaza kimya, na kutulia tuli, na 2. Kusikiliza kwa umakini mafunzo yake na makatazo yake: Ndiyo maana ya فاستمعوا له وأنصتوا… “Kaeni kimya na takeni kuisikiliza,, yaani chukueni hima kusikiliza kwa masikio yenu na moyo wenu, yanayosomwa.
      Mwenyezi Mungu amesema kwenye Surat Al-A‘raaf:
      وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (ألأعراف 7 :204 )
      “Na isomwapo Qur’ani isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa.” Al-A‘raaf, 7:204)

    Na kusomwa Qur’ani hakuhitaji udhu, kunahitaji utulivu na usafi wa moyo na utiifu wa mwenye kusikiliza yanayosomwa. Nimeshajibu suala hili la kuweza kusoma Qur’ani pasi na udhu. Sayyidina Umar رضي الله عنه alimkaripia mtu aliyemwambia: “Mbona unasoma Qur’ani na huna udhu?”, alipomuona ametoka chooni, kurudi kwenye majlisi, huku akisoma Qur’ani. Sayyidina Umar alimwambia: “Na nani aliyekupa fatwa hiyo? Musaylama al-Khadh-dhaab?” Muwatta’ Malik.

    Ndiyo maana hata mwenye hedhi na nifasi, wanaweza kusoma Qur’ani, kutoka moyoni mwao, na kuisikilizwa au kusikiliza inaposomwa na mtu mwengine. Hakuna junaha. Hivyo, hakuna haja ya kuwa na Udhu kwa kusoma Qur’ani.

    Ama msahafu ni maandishi ya Maneno hayo, yaliyoandikwa kwenye kurasa صحف =swuhuf, zinazoweza kufunguliwa moja baada ya nyengine. Ndio maana ukaitwa: Mus-hafu=Msahafu, yaani kitabu chenye kurasa zenye kufunguliwa moja baada ya nyengine. Hivyo, suala lako linaulizia kuhusu kujuzu au kutokujuzu kugusa msahafu; SI kusoma Qur’ani. Qur’ani inaweza kusomwa bila ya udhu.

    Suala hili lina khilafu, kidogo, baina ya wanazuoni. Vile wote wanakubaliana kuwa ni jambo jema kugusa msahafu ukiwa na udhu, wanatofautiana kuhusu kuwajibika au kutowajibika kuwa na udhu unapogusa msahafu.

    Wanazuoni wengi, miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu za Sunni, wanasema SI lazima uwe na udhu, ila ni mustahabb: ni jambo jema kuaw na udhu, kuonesha heshima na taadhima ya kitabu kilichoanndikwa maneno ya Mwenyezi Mungu. Ila hakuna ulazima.

    Huo ndio msimamo wa wanazuoni wengi sana, kwamba SI lazima, bali ni mustahabb: inependekezwa, maana inapendeza na ni jambo jema la kuonesha heshima tu, ila SI faradhi, kwamba ukishika pasi na udhu basi uanpata dhabi.

    Wengine, hasa Imam Shafi, anasema ni budi uwe na udhu, na hoja yake kuu ni uelewa wake wa Aya 79 ya Surat al-Waaqi‘a: isemayo:

    إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ (77) فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ (78) لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ (79 ) الواقعة.

    “Hakika hii bila ya shaka ni Qur’ani Tukufu. Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. Hapana akigusye ila walio takaswa.”

    Yeye ameelewa maneno yasemayo: “… hapana akigusaye ila aliyetwahir.”, kwamba ni mwenye udhu.

    Wanazouni, karibu wote wanasema, maana ya Aya hiyo, ni: “Hii ni Qur’ani Tukufu, iliyohifadhiwa katika Kitabu kinacholindwa ambacho hapana akigusaye ila walio TAKASWA,” nao ni Malaika. Hivyo tunazungumzia Lawh al-Mahfuudh, siyo msahafu. Aya inazungumzia Qur’ani, haizungumzii Msahafu.

    Na dalili ni kwamba Qur’ani inasema: الْمُطَهَّرُونَ = Waliotakaswa. Haisemi متطهرون Waliojitwahirisha, au waliotia udhu. Kuna tofauti kubwa baina ya kusema ALIYETAKASWA na ALIYEJITWAHIRISHA. Aliyetakaswa ni Malaika, ametakaswa na kila aina ya uchafu, dhambi, uasi na kadhalika. Lakini aliyejitwahirisha ni yule aliye tia udhu. Kama tofauti iliyopo baina ya Aliyesafishwa, na Aliyejisafisha. Aliyesafishwa ni tayati msafi huyo, hana haja ya kujisafisha. Aliyejisafisha ni mtu ambaye hakuwa safi, lakini akajisafisha. Wa mwanzo ni Malaika na wa pili ni mwanadmu na majini.

    الْمُطَهَّرُونَ :Muttwahharuun = Waliotakswa, na waliotakasika ni Malaika, si Wanadamu. Malaika wametakaswa, wamesafishwa hawana haja ya kutawadha wala kujisafisha, hawali hawanywi, kazi yao ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutekeleza majukumu walilyopewa, tu. Kamwe hawaasi; hivyo hawana haja ya kujitakasa wala kujisafisha. Wamesha takaswa na wamesha safishwa.

    Lakini متطهرون : Mutatatwahhiruun = ni Walio jitwahirisha, au kwa maneno mengine, waliotawadaha, wenye udhu. Mwanadamu hakutakaswa, waliotakaswa ni Malaika. Hivyo, kinacho zungumziwa katika Aya hiyo, SI utohara, yaani kuwa na udhu, bali UTAKASO wa waliotakaswa na Mwenyezi Mungu, na hao ni Malaika, na Kitabu kinacho zungumziwa ni Lawh al-Mahfuudh, si Msahafu.

    Zaidi ni kwamba hata Aya yenyewe inazungumzia Qur’ani, si Msahafu: inasema إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ‏. Haisemi Mushafu kariim. Msahafu ni Kitabu cha maandishi, vile Qur’ani ni ile inayosomwa na kutoka mdomoni mwa mwenye kusoma.

    Na lau kama ingelikuwa ni haramu kugusa msahafu pasi na udhu, basi Mtume ﷺ lazima angelisema hivyo. Hakuna Hadithi hata moja, si ya kauli wala vitendo inayosema kuwa ni vibaya kugusa msahafu bila ya udhu.

    Hivyo, hakuna ulazima kutawadha ukishika msahafu, wala hakuna ulazima kuwa na udhu ukisoma Qur’ani, iwe kutokana na hifadhi yako, au kutokana na msahafu. Iwe msahafu huo umeushika mwenyewe, au ameushika mtu mwengeine. Ila ni jambo linalopendeza na kutiliwa mkazo kutawadha unapotaka kusoma Qur’ani au unapotaka kuushiika Msahafu, maan huwezi kuishika Qur’ani, bali unashika msahafu. Qur’ani ni ile inayosomwa na kutoka mdomoni mwako ndio Qur’ani.

    Kwa ufupi, kila mtu ajichagulie kile akionacho kuwa ndio sahihi kwake yeye. Ila hakuna mwana chuoni yeyote asemaye kuwa unapaa dhambi ukigusa msahafu pasi na udhu. Hata Imam Shafi hasemi hivyo.

    Kwa maana hiyo –hata kwa Imam Shafi- ni واجب خير wajibu wa kujichagulia, si wa kupatilizwa. ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ (الحج 32 ) “ Hivyo, na mwenye kutukuza na kuadhimisha ishara za Mwenyezi Mungu basi ishara ya uchamungu kutoka nyoyoni.” (Al-Hajj,22:32)

    وبالله التوفيق

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ ابى بكر بن سالم

    Imejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kuongeza au kuondoa chochte, NA kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • JE INAJUZU KWA MWENYE HEDHI KUSOMA QUR’ANI?‎

    Nimeulizwa, kwa mara nyengine tena, suala la hapo juu. NARUDIA:-‎

    Nimeulizwa kwenye Ukumbi wa Waja Wema, kuhusu kujuzu au kutokujuzu ‎kwa mwenye Hedhi au Nifasi, kusoma Qur’ani: NANUKUU:-‎

    ‎“Wakati wa kulala tunatakiwa kuomba dua na duwa hizo ni sura za Quran. ‎Sasa kama mtu ana hedhi asiombe dua alale hivohivo kwani haruhusiwi ‎kusoma Quran?‎

    Na kama anatakiwa aombe dua ni dua zipi hizo”‎

    JAMANI SWALI HILO ‎

    Mtu akiwa kwenye hedhi anaweza akatia udhu wa swala kwa ajili ya ‎kufanya dhikr?‎

    Nini hukumu ya Kugusa au kusoma Qur’ani?”‎

    JIBU.‎

    BISMILLAH!‎

    Kwanza niondoe dhana ya kwamba mwenye hedhi anaweza kutia udhu. ‎Hawezi. Na ndio sababu kubwa ya kutoweza kuswali. Kwa hivyo, hilo ‎tuliweke upande kabisa. Akitia Udhu basi hana udhu, yaani hajajitwahirisha, ‎bali amejisafisha viungo tu. Hivyo, hawezi kuwa na udhu.‎

    Kugusa na kusoma, au kusoma tu kwa mwenye UDHU –yaani Mwislamu ‎ambaye mwili wake upo katika hali ya tohara ndio msimamo wa Maulamaa ‎wote. Hivyo, inapendekezwa na wanazuoni wote mtu kuwa na udhu ‎wakati wa kusoma Qur’ani au kugusa Qur’ani. INAPENDEKEZWA, SI ‎wajibu!‎

    Hata hivyo, wametofautiana kwa mtu ambaye hana udhu, au mwili wake ‎hauko katika hali ya usafi kutokana na Janaba, Hedhi au Nifasi. ‎

    Kwa maana hiyo, Hukumu ya Kugusa au Kusoma Qur’ani inawagusa watu ‎wa aina mbili.‎

    ‎1.‎ Mtu asiye na UDHU, lakini ana uwezo wa kujitwahirisha; kwa maana ‎hiyo vile vile mwenye Janaba.‎
    ‎ ‎
    ‎2.‎ Mtu ambaye hawezi kujitia UDHU, hata kama atataka, kwa maana ‎hiyo mwenye Hedhi au Nifasi.‎

    Ama kuhusu Mtu asiye na Udhu, lakini ana uwezo wa kujitwahirisha, kuna ‎ikhtilafu kubwa na pana, tokea kuhusu KUGUSA msahafu, hadi KUSOMA ‎Qur’ani bila ya kugusa Msahafu, na kila mmoja anatoa daili zake, tokea za ‎kuunga mkono msimamo wake, hadi za kudhoofisha dalili za asiyekubaliana ‎naye. Hivyo, hili nitalijibu peke yake, baadaye; ili mtu ajiamulie mwenyewe ‎ametosheka na msimamo wa nani.‎

    Hapa nitajibu suala la pili, nalo ni Mtu ambaye hawezi kujitia Udhu, hata ‎kama akitaka, kutokana na Hedhi au Nifasi. ‎

    Kimsingi, hakuna Hadithi, hata dhaifu, yenye kumkataza mwanamke ‎mwenye Hedhi au Nifasi, kusoma Qur’ani, iwe kutokana na hifadhi yake ‎mwenyewe, au kutokana na msahafu alioshikiwa na mtu mwengine mbele ‎yake – pasi na yeye kuugusa. Na kutokana na ukweli huo, basi maulamaa ‎wote wa madhehbu nne kubwa, Shaafi’iyya, Malikiyya, Hanafiyya na ‎Hanbaliyya wanakubaliana na hilo. Kwani mwenye Hedhi au Nifasi, ‎anakatazswa mambo mane tu, hakuna la ziada.‎

    ‎1.‎ Kuswali, kwani uwajibu wa Kuswali unaondoka. Hivyo basi ‎hatakikani hata kulipa Swala zinazompita, wakati akiwa katika hali ya ‎Hedhi au Nifasi. Hii ni kwa mujibu wa Hadithi na Qur’ani. ‎

    ‎2.‎ Kufunga, lakini uwajibu wa kulipa upo; maana Kufunga si mwaka ‎mzima, bali ni kwa majira yake tu ya kuingia mwezi wa Ramadhani. ‎Hivyo, siku ambazo ameshindwa kuzifunga kutokana na kuwa katika ‎hali ya Hedhi au Nifasi, atazalipa wakati wowote mwengine, ambapo ‎hayumo tena katika Hedhi au Nifasi. Hii ni kwa mujbu wa Hadithi na ‎Qur’ani.‎

    ‎3.‎ Kuingiliana kimwili na mumewe. Haramu, mpaka atwahirike na ‎kukoga. Hii vile vile kwa mujibu wa Hadithi na Qur’ani.‎

    ‎4.‎ Kutufu al-Ka’ba, hii kwa mujibu wa Hadithi na Amri ya Mtume. Hata ‎hivyo, anaruhusiwa kufanya amali zote nyengine za Hija, ikiwa ‎pamoja na Kusimama Arafha, kulala Muzdalifa, kulala Mina, Kupiga ‎mawe, Kwenda Sa’y, na kusoma dua na nyiradi zote. ‎

    Kwa ufupi anaruhusiwa MAMBO YOTE ANAYOFANYA ‎MWENYE KUHIJI WA KAWAIDA, ISIPOKUWA KUTUFU TU. ‎Hii ni kwa mujibu wa Hadithi na Amri na maelekezo ya Mtume ‎صلي ‏الله عليه وسلم‎ ‎

    Kwa maana hiyo, ni mambo hayo mane pekee ndiyo watu wote ‎wanakubaliana kuwa mwenye Hedhi au Nifasi hawezai kuyafanfya. ‎

    Mengine hawakubaliani. Na sababu kubwa ya kutokubaliana na hiyo ya ‎
    kutokuweko dalili wazi wazi, si kutoka katika Qur’ani wala Hadithi, ambayo ‎ama inaweza kuwa na maana mbali mbali, au ikiwa ni Hadithi basi Hadithi ‎yenyewe ina ila kutokana na wapokezi wa Hadithi hizo. ‎

    Tuanze na suala la mwenye Hedhi au Nifasi kusoma Qur’ani pasi na kuigusa. ‎

    KUSOMA QUR’ANI PASI NA KUGUSA MSAHAFU.‎

    Hedhi au Nifasi, si hali ambazo yule mwenye kuzipata, ana uwezo nazo ‎kuiondoa, mara tu inapomjia. Kwa maana hiyo, hali hizo mbili zinaingia ‎katika ‎وما إستكرهوا عليه‎ yaani mambo ambayo hamna nguvu nayo kuyazuwia, ‎mara tu yakisha kufikeni. Na Mtume ‎صلي الله عليه وسلم‏‎ amesema: ‎رفع عن أمتي ‏الخطاء والنسيان وما إستكرهوا عليه‎ ‎

    Pili, ni budi kuwa Maswahaba wa kike, si tofauti na waislamu wengine ‎waliokuja baada yao. Walikuwa wakipatwa na Hedhi na Nifasi kama ‎mwanamke yeyote yule mwengine. Lau kama ingelikuwa ni haramu kwa ‎mwenye Hedhi au Nifasi kusoa Qur’ani – na tukumbuke Maswahaba wengi ‎walikuwa wakisoma kutokana na hifadhi zao na si kutokana na Miswahafu- ‎basi Mtume ‎صلي الله عليه وسلم‎ angelikwisha wakataza kufanya hivyo. Na ‎hapana hata mwanamke mmoja Swahaba aliyeuliza au kusema kuwa ‎hakuna ruhusa kusoma Qur’ani ukiwa na hedhi au nifasi. Kwa vile, hakuna ‎habari yoyote kwamba aliwakataza, basi ni wazi kuwa si haramu. ‎

    Tatu: Hata hao maulamaa wachache mno – wa kuweza kuhesabika kwenye ‎kiganja kimoja cha mkono – ambao wanatoka Madhehebu ya Dhwahiriyya, ‎wamesalim amri hatimae kwa kusema kwamba: Aruhusiwe mwenye Hedhi ‎na Nifasi kusoma kutoka moyoni mwake, kwani venginevyo itamaanisha ‎kumzuwia kusoma Qur’ani kwa muda mrefu: siku saba na kuendelea! Ila ‎wansema kwamba ruhusa hiyo ni ya dharura tu; yaani kusoma kama nyiradi ‎zake za Qur’ani, au kama ni mwalimu anawalaqini wanafunzi wake (yaani ‎anasoma aya na wanafunzi waigize msomo wake) au aya chache tu, mara ‎kwa mara, ili kujiepuehsa kusahau. Kama uonavyo, ni hoja dhaifu sana! ‎Iweje umruhusu kusoma kidogo, lakini usimruhusu kusoma nyingi! ‎Kiwango hicho kimetolewa wapi?!‎

    Nne. Kwa vile Bibi Aisha, alizuwiliwa kutufu tu, na si amali nyengine yeyote ‎ya Hija, ikiwa pamoja na visomo mbali mbali anavyosoma mwenye kuhiji, ‎iwe dua yake mwenyewe tu au dua ya Qur’ani, basi ni wazi kuwa ni ‎KUTUFU PEKEE ndiko kunako hitajia UDHU, katika amali zote za Hija. ‎

    Kama ingelikuwa na Kusoma Qur”ani nako ni mambo yanayokatazwa kwa ‎mtu mwenye Hedhi, basi Mtume angelimwambia :Na usisome Qur’ani. ‎Lakini hakumwambia. Hivyo, kusoma Qur’ani kwa mwenye Hedhi ‎hakuwezi kuingizwa kuwa kunahitaji Tohara ya mwili, tena kwa jambo ‎ambalo huna uwezo nalo kuliondoa. (i.e. kinyume na Janaba –kama ‎tutavyokuja kuona pale nitapozungumzia ikhtilafu za maulamaa kuhusu ‎kusoma Qur’ani kwa mwenye janaba- pasi na kuugusa msahafu)‎

    Tano. Mwili wa Mwislamu si Najsi. Na wala hauwezi kunajisika, kwa maana ‎kwa kutenda jambo fulani basi mwili wake unakuwa najisi. Unaweza ‎ukachafuka, au ukachafuzwa kwa kuguswa na najisi. Lakini ukichafuliwa ‎kwa najisi, basi panachafuka pale palipoguswa na najisi hiyo, na si mwili ‎wote wa Mwanadamu. ‎

    Kwa mfano, mtu ametawadha. Lakini, akarukiwa na mkojo kwenye mguu ‎wake. Basi anatakiwa kuosha hapo paliporukiwa na mkojo tu, hadi pasafike. ‎Udhu wake upo pale pale; maana minogoni mwa mambo mane yenye ‎kutengua udhu, hamna kurukiwa na najisi kiungoni. ‎

    Kwa maana hiyo, midam mwili wa Mwanadamu, kimsingi si najsi, basi pale ‎anapokuwa katika hali ya Hedhi au Nifasi – ambayo hana uwezo wa ‎kuondoa hali hiyo- basi anaendelea kuwa twahir kimwili, ila hana tohara ya ‎kumuwezesha kuswali na kutufu tu; kwa sababu ibada mbili hizo zinahitaji ‎Udhu. ‎

    Na lau kama anapokuwa katika Hedhi au Nifasi huwa SI TWAHIR basi mtu ‎asingeliweza kumgusa mkewe pale anapokuwa katika Hedhi au Nifasi, kama ‎walivyokuwa wakifanya Mayahudi. Na papo, kuna hadithi kem kem zenye ‎kusema kwamba siyo tu Mtume ‎ﷺ‎ alikuwa akiwagusa wakeze ambao ‎walikua katika Hedhi, bali wakati mwengine alikuwa akifanya mambo ‎kadhaa –isipokuwa kumuingilia kimwili tu- mkewe mwenye Hedhi. ‎

    Bi Aisha alikua akimchana nywele Mtume aliyekuwa amekaa itikafu ‎msikitini vile yeye Bi Aisha alikuwa katika Hedhi. Mtume alimuomba Bi ‎Aisha ampke kitu fulani, na Bi Aisha akamjibu: Lakini mimi nina Hedhi! ‎Mtume akamuuliza: Na mkono wako nao una hedhi!‎

    Sita, Mwislamu anatakiwa kusoma Qur’ ani kila akipata nafasi, awe na udhu ‎asiwe na udhu. Kumkataza mwenye Hedhi na mwenye Nifasi kusoma Qur’ ‎ani ni kwenda kinyume na amri hiyo; jambo ambalo litamnyima siyo tu ‎utiifu wa kuisoma Qur’ani kwa muda mrefu, bali pia kumnyima kupata ‎thawabu za kusoma Qur’ani, thawabu ambazo kwa kila herufi moja anapata ‎thawabu kumi. Kwanini apigwe marufuku na neema hiyo, kwa muda mrefu? ‎

    Kutokana na hoja hizo hapo juu, na kutokana na ukweli wa kwamba ‎HAKUNA HADITHI SI YA VITENDO WALA WA MANENO ‎inayokataza kusoma Qur’ani kwa mwanake mwenye Hedhi au Nifasi, ‎tukielewa kwamba Maswahaba wa kike hawakuwa malaika, bali ‎wanaadamu wa kike wanaopata hedhi na nifasi, na kutokana na ukweli wa ‎kwamba kila kitu ni halali mpaka kikatazwe, basi mwenye hedhi au nifasi ‎anaweza kusoma Qur’ani pasi na kuugusa msahafu, na anaweza kusoma ‎kiwango akitakacho cha Qur’ani. Hakuna junaha!‎

    ‎[Suala la kujuzu au kutokujuzu kugusa msahafu pasi na udhu nitalijibu peke ‎yake, in sha Allah]‎

    وبالله التوفيق‎ ‎

    الحقير إلى الله تعالى عبد القادر شريف آل الشيخ ابى بكر بن سالم

    Imejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kuongeza au kuondoa ‎chochte, NA kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye ‎Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • Nimeulizwa DUA ya KUOMBA baada ya Kukimiwa Swala ya Faradhi, NANUKUU:-

    *Naomba kuuliza kwa shekh je ni jinsi gani ya kuitikia *iqama* baada ya kukim swala yaani baada ya kumalizana Laa Olaba illaAllah*

    JIBU
    BISMILLAH

    Inapenfekezwa KUSEMA!
    أقامها الله وأ دامها

    AU kusema:
    اللهم آت سيدنا محمدا الوسيلة والفضيلة، والدرجة العالية الرفيعة، وابعثه اللهم مقامًا محمودًا الذي وعدته، إنك لا تخلف الميعاد، اللهم أقمها وأدمها ما دامت السماوات والأرض

    وبالله التوفيق.