Category: Hadith

  • DARSA YA BM.14.3\1 MLANGO WA KUCHINJA

    Hadithi ya Leo, Jumatatu, tarehe 12, Rajab, 1446, sawa na tarehe 13, JANUARI, 2025

    KUHUSU wa KUCHINJA

    SEHEMU YA KWANZA

    باب الذبائح14.3
    مقدمة
    UTANGULZI

    Neno *الذبح* kwa upande wa Lugha ya Kiarabu, maana yake ni mnyama aliyechinjwa, au atayechinjwa *الذبيحة*, na kwa maana hiyo ni kukatwa mishipa ya  shingoni mwa mnyama anayetakiwa kuchinjwa. 

    وشرعًا: ذبح حيوان مقدور عليه مباح أكله، يعيش في البر غير جراد، بقطع حلقوم ومريء، أو عَقْر ما لم يقدر عليه منه.
    Kwa upande wa Sharia, hata hivyo, maana yake ni kuchinjwa mnyama halali, aliyedhibitiwa, na ambaye anaishi nchi kavu (isipokuwa nzige) kwa kukata mishipa yake rohoni, au kwa kumwindwa kisharia.

    وحكمه ثابت، بالكتاب، والسنَّة، والإجماع.
    Na Asasi ya Kuchinja mnayama halali, imethibiti kupitia Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Sunna ya Mtume ﷺ tokea Sunna ya kauli hadi ya vitendo, na imethibiti vile vile kupitia Ijma’a ya wanazuoni wote.

    Kwa upande wa Qur’ani, Mwenyezi Mugu Amesema:

    حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنْزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ
    Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama,ILA MKIMDIRI KUMCHINGA. .(Al-Maida 5:3)

    ومن السنة ما رواه الدارقطني أنَّ النَّبي -صلى الله عليه وسلم- بعث ببديل ابن ورقاء يصيح في فِجَاج مني: “ألا إنَّ الذكاة في الحلق واللبة”.
    Kwa upande wa Hadithi, Mtume ﷺ alimtuma Budayl bin Warqa’, aende kwa mahujjaji, mini Mina, kuwatangazia “Juweni kuwa kuchinja ni kukata mishipa ya kooni kwenye kupitia chakula!” Ameipokea Dara-Qutny.

    وما جاء في البخاري (5509)، ومسلم (1968) من حديث رافع بن خديج قال: كنا مع رسول الله -صلى الله عليه وسلم- في سفر، فندَّ بعير من إبل القوم، ولم يكن معنا خيل، فرماه رجل بسهم، فحبسه، فقال -صلى الله عليه وسلم-: “إنَّ لهذه البهائم أوابد كأوابد الوحش، فما فعل منها هذا، فافعلوا به هكذا”.
    Hadithi nyengine imepokewa na Bukhari na Muslim, kutoka kwa Rafi’ bin Khudayj akisema: “Tulikiwa safarini na Mtume !ﷺ Ikatokea ngamia mmoja kutokana na ngami wa jamaa wasafiri, akakimbia, na hapakuwepo mtu yeyote mwenye farasi wa kumkimbilia kumkamata. Basi mtu mmoja akamdunga ngamia huyo kwa mshare wake, akaanguka.” Mtume ﷺ akasema: “Juweni kuwa mifugo hii, ni viumbe kama viumbe mwitu; hivyo huyu aliyemdunga kwa mshare wake amemuwinda, na nyingi mnapokuwa hamna njia nyengine ya kumkamata mnyama wenu aliyekimbia, basi mdungeni kwa mishare yenu.”

    Wanazuoni wakazidi kufafanua kwa kusema:

    “أجمعوا على أنَّ المرء إذا ذبح ما يجوز ذبحه، وسمَّى الله، وقطع الحلقوم والودجين، وأسَالَ الدَّمَ، فإنَّ الشاة مباح أكلها”.
    “Wanazuoni wote wamekubaliana kuwa mchinjaji akichinga mnyama anayejuzu kujichinwa, akapiga Bismillahi, na akakata mishipa mwili mikuu ya damu rohoni, damu ikachururika, basi ni halali kula mnyama huyo.”

    وأجمعوا على أنَّ ما أبيح أكله لا يباح إلاَّ بالذكاة، كما أجمعوا على أنَّ الميتة حرام.
    Na wamekubalina, kwa kauli moja, kuhusu wanyama wa nchi kavu, kuwa haijuzu kumla isipokuwa baada ya kuchinjwa, kama walivyo kubaliana kuwa nyamafu ni haramu kuliwa.

    وصفة الذبح، والنحر، والعقر: واحدة في جميع الشرائع السماوية من حيث وجوب إسالة الدم، ومن حيث وجوب إجراء عملية الذبح أو النحر في الموضع الَّذي حدَّده الشرع في جسم المذبوح أو المنحور.
    Na kuchinha mnyama halali, ni kukata mishipa ya rohoni, au kujeruhi kichinjwa, kwa mujibu wa Sharia zote za Vitabu vilivyoteremshwa kutoka Mbinguni, ambapo ni wajibu wa kutumia ala ya kuchururisha damu, kwa kujeruhi mwili wa mnyama aliyechinjwa.

    ولولا توحد الشرائع السماوية في أصول الذكاة، لما أحل الله للمسلمين ذبائح أهل الكتاب، كما أحل ذبائح المسلمين.
    Na pasi na kuwepo Sharia za kuchinja ndani ya Vitabu vvyote vilivyo teremshwa kutoka Mbinguni, wasingeruhusiwa Waialamu kula wanyama waliochinjwa na Ahlul-Kitab, kupitia shaia hizo hizo walioteremshiwa Waislamu, ndani ya Qur’ani.

    ويشترط للذكاة ذبحًا أو نحرًا أربعة شروط:
    Kuna Masharti mane kuhalalisha kichinjwa halali kuliwa.

    أحدها: أهلية الذابح، أو النَّاحر، أو العاقر، وهو أنْ يكون عاقلاً، قاصدًا التذكية، فلا تحل ذكاة مجنون، وسكران، وطفلٍ دون التمييز؛ لأنَّه لا قصد لهم.
    SHARTI LA KWANZA: Linamnhusu mchinjaji, au muwindaji, ambaye anapaswa awe mwenye akili timamu, aliyekusudia kuchinja. Na kwa maana hiyo, haijuzu kula mnyama aliyechinjwa na mwenda wazimu, au mlevi, au mtoto mdogo chini ya umri wa Tamyiiz, kwa sababu wote hao hawna mamlaka ya kukusudia kuchinja.

    الثاني: الآلة: وهو أنْ يذبح بآلة محدَّدة تقطع، أو تخرق بحدها، لا بثقلها سواءٌ من حديد، أو حجر، أو خشب، أو غيرها، غير عظم وظفر؛ فلا تحل الذبيحة بهما.
    SHARTI LA PILI: Linahusu ala iliyotumiwa; yaani lazima patumiwe ala yenye makali, yenye uwezo wa kukata mishipa kooni, au kuchoma mwilini kwa ncha na makli yake; siyo kumuua kwa kumpiga mtarimbo wa chuma, au kumpiga jiwe, au kumpiga gongo, au kumpiga kitu chochote chengine, kama kumpiga kwa pembe, au kwa fupa kubwa. Mnyama yoyote ataye uliwa kwa kupigwa kupitia vitu kama hivyo, haijuzu kumla.

    الثالث: أنْ يقطع الحلقوم: وهو مجرى النفس، والمريء: وهو مجرى الطعام والشراب، ولا يشترط قطع الودجين، بل يستحب، والودجان: عرقان بجانب الرقبة.
    SHARTI LA TATU: Wajibu wa kukata mishipa ya damu shingoni na rohoni, panapo pita chakula na kinywaji. Siyo lazima kukata shingo nzima, bali koo na mishipa ya damu kooni tu. Bali Sunna ni kukata mishipa ya sehemu hiyo tu, shingoni.

    الرَّابع: التسمية عند حركة يده بالذبح بقوله “باسم الله”، ولا يجزئ غيرها، ووجوبها إذا ذكرها، ويسقط مع السهو، وهو مذهب الجمهور.
    SHARTI LA NNE: Kupiga Bismillahi wakati wa kuanza kuchinja, kwa kusema Bismillahi. Na haijuzu kutumia maneno mengine, isipokuwa Bismillahi. Akisahau kupiga Bismillahi hapana junaha. Huo ndio msimamo wa Wanazuoni wote wa Kiislamu.
    Baada ya Utangulizi huo, sasa tusome Hadithi alizotuwekea Imam Ibn Hajar katika Mlango huu wa Vichinjwa.
    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • DARSA YA BM.14\4 MLANGO WA KUWINDA NA KUCHINJA

    Hadithi ya Leo, Ijumaa, tarehe 9, Rajab, 1446, sawa na tarehe 10, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUWINDA NA KUCHINJA

    SEHEMU YA NNE

    1334 – وَعَنْ عَدِيٍّ قَالَ: {سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنْ صَيْدِ اَلْمِعْرَاضِ فَقَالَ: “إِذَا أَصَبْتَ بِحَدِّهِ فَكُلْ، وَإِذَا أَصَبْتَ بِعَرْضِهِ، فَقُتِلَ، فَإِنَّهُ وَقِيذٌ، فَلَا تَأْكُلْ”} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ.

    1. Imepokewa kutoka kwa Adiyy رضي الله عنه akisema: “Nilimuuliza Mtume  kuhusu kitu kilichowindwa kwa mkuki.” Akasema: “Mkuki utaompiga mnyama na kumuua, kula. Na mkuki utaompiga mnyama pasi na kupitia makali mkuki, na mnyama yule akafa, usile. Kwa sababu mnyama huyo sasa ni sawa na mnyama aliyeuwawa kwa bakora au jiwe.” Ameipokea Bukhari.

    UFAFANUZI

    Hadithi hii inatufundisha kuhusu kuwinda kwa kutumia kichwa cha  mkuki, kilichochomekwa kwenye mpinni mrefu wa mti, kuwa ukimkuta mnyama uliyomdunga amechomwa na kichwa cha mkuki, basi ni halali kuliwa. Lakini ukimkuta amegongwa na mpini wa kichwa cha mkuki, na amekufa, basi usimle maana huyo ameuliwa na kitu chengine kisichokuwa kichwa cha mkuki wako. Na makatazo haya yanaendana na Aya ya 3 ya Surat, Al-Maida, inayokataza aina mbali mbali za wanayama waliouawa au kufa kupitia vitu mbali mbali. Mwenyezi Mungu ameorodhesha wanayama hao kwa kusema:

    حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنْزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَنْ تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ …(المائدة،5:3)
    Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. … (Al-Maida, 5:3)

    Hivyo, mnayama yeyote atayeuliwa kwa kisichokuwa ala ya kuulia au kuchinjia ni haramu kuliwa. 

    1335 – وَعَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ رضي الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {“إِذَا رَمَيْتَ بِسَهْمِكَ، فَغَابَ عَنْكَ، فَأَدْرَكْتَهُ فَكُلْهُ، مَا لَمْ يُنْتِنْ”} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ.

    1. Imepokewa kutoka kwa Abi Tha’labah رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Ukilenga mshale wako na mnyama akapotea, ukaja ukamkuta amekufa, kula, ilimradi awe hajaoza.” Ameipokea Muslim.

    UFAFANUZI

    Hadithi hii inazungumzia mtu aliyewinda mnyama kwa kumdunga mshale, lakini mnyama huyo akakimbia na kupotea, usiweze kumpata. Ila baadaye ukamgudua, kuwa mshare wako ndio uliomuua, basi unaweza kumla, ilimradi awe hajaoza. Akisha oza haijuzu kumla maana sasa ni mzoga, na mzoga ni haramu kuliwa. Mwenyezi Mungu Amesema: _Mmeharimishiwa nyamafu, na damu,_

    YALIYOMO NA YATOKANAYO (kwenye Hadithi hizi mbili)

    1. Mnyama aliyewindwa kwa kutumia kichwa cha mkuki wenye mpini wa mti au wa chuma, anajuzu kuliwa ikiwa kilichomuua ni ncha ya mkuki wenyewe, si kugonwa na mpimi wa mkuki.
    2. Haijizu kula mnayama aliyegongwa na kitu kama mti, gongo au mpini wa kitu; huyo anajulikana katika Saria kuwa َالْمَوْقُوذَةُaliyekufa kwa kupigwa na kitu kikamuua.
    3. Haijuzu kula mnyama yoyote aliyekufa-maji, isipokuwa mnyama anayeishi baharini peke yake.
    4. Haijuzu kuwinda kwa mnyama asiyeweza kumjeruhi kiwindwa alicho tomezewa kwenda kumwinda kwa makucha yake au meno yake ya Nabu,
      Haijuzu kula mnyama aliyekwisha oza, maana akisha oza huyo ni mzoga, yaani nyamafu, haramu kula mzoga.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • DARSA YA BM.14\3 MLANGO WA KUWINDA NA KUCHINJA

    Hadithi ya Leo, Alhamisi, tarehe 8, Rajab, 1446, sawa na tarehe 9, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUWINDA NA KUCHINJA

    SEHEMU YA TATU

    1333 – وَعَنْ عَدِيِّ بنِ حَاتِمٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اَللَّهِ  { “إِذَا أَرْسَلَتَ كَلْبَكَ فَاذْكُرِ اسْمَ اَللَّهِ، فَإِنْ أَمْسَكَ عَلَيْكَ فَأَدْرَكْتَهُ حَيًّا فَاذْبَحْهُ، وَإِنْ أَدْرَكْتَهُ قَدْ قُتِلَ وَلَمْ يُؤْكَلْ مِنْهُ فَكُلْهُ، وَإِنْ وَجَدْتَ مَعَ كَلْبِكَ كَلْبًا غَيْرَهُ وَقَدْ قُتِلَ فَلَا تَأْكُلْ: فَإِنَّكَ لَا تَدْرِي أَيَّهُمَا قَتَلَهُ، وَإِنْ رَمَيْتَ سَهْمَكَ فَاذْكُرِ اسْمَ اَللَّهِ، فَإِنْ غَابَ عَنْكَ يَوْماً، فَلَمْ تَجِدْ فِيهِ إِلَّا أَثَرَ سَهْمِكَ، فَكُلْ إِنْ شِئْتَ، وَإِنْ وَجَدْتَهُ غَرِيقاً فِي اَلْمَاءِ، فَلَا تَأْكُلْ” } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِمٍ .

    1. Imepokewa kutoka kwa Aadiyy bin Haatim رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Ukimuachilia mbwa wako kwenda kuwinda, piga Bismillahi. Akikamata mnyama na ukamdiriki mnyama huyo akiwa hai, mchinje. Lakini ukimkuta mnyama aliyemuwinda ameshauliwa na mbwa wako, lakini hajaliwa na mbwa wako, basi kula. Lakini ukimkuta mbwa wako na mbwa mwingine wamemuua mnyama, usile. Kwa sababu hujui mbwa yupi kati ya wawili hao ndiyo aliyemuua mnyama huyo. Vile vile ukilenga mshale kumpiga kiwindwa, sema Bismillahi. Akipotea mnyama huye uliyemuwinda kwa muda wa siku moja lakini ulipomgundua ukakuta kwamba hakuna kilichomuua ila mshale wako, kula ukitaka. Lakini ukimkuta amezama kwnye maji na amekufa, usile.” Muttafaq alayhi.

    UFAFANUZI

    Hadithi hii inazungumzia hukumu ya mnyama aliyewindwa na mbwa aliyefunza kuwinda, kwamba wakati wa kumtomeza mbwa wako akawinde, basi kwanza piga _Bismillahi._ Ukimkuta mnyama aliyewindwa bado yupo hai, basi mchinje na ni halali kuliwa.  Lakini ukimkuta mbwa wako na mbwa mwengine, na mnyama aliyewindwa amekufa, basi usimle; maana hujuwi ni mbwa gani kati ya mbwa wawil hao ndiye aliyemuua. Hali kadhalika, ukilenga mshale wako kumdunga mnyama, basi piga _Bismillahi_ kwanza. Ukimkuta yuhai mchinje, na ukimkuta ameshakufa basi ni halali maana umeshampigia _Bisamillahi._ Lakini akikimnbia na kupotea na mshare wako mwilini mwake, kisha baadaye ukamgundua basi ni halali kumla, ilimradi hajaoza. Lakini ukimkuta amekufa kwa kuzama ndani ya maji, basi si halali kumla; maana huwezi kujuwa ni kitu gani ndicho kilicosababisha kwanza kufa kwake, ni mshare wako au ni kuzama ndani ya maji. 

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Kujuzu kuwinda kwa kutumia mbwa aliyefunzwa kuwinda kama Alivyo ruhusu Mwenyezi Mumgu kwa kusema: {وَمَا عَلَّمْتُمْ مِنَ الْجَوَارِحِ} Na kupitia kuwinda kwa kutumia wanyama mliowafumza kuwinda.
    2. Wanyama wanaoweza kutumiwa kuwinda ni Mbwa, Kipan ga, Paka-mwitu, Chui mdogo na mfano wake.
    3. Haijuzu kuwinda kwa kutumia mnyama, isipokuwa mnyama huyo awe amefunzwa kuwinda, na amefunzika; Mwenyezi Mungu Amesema: {مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّهُ} wenye kujeruhi mliowafunza alichokuleteeniMwenyezi Mungu.
    4. Haijuzu kuacha kwa makusudi kupiga Bismillahi wakati wa kumtomeza kwenda kuwinda.
    5. Mwenye kuacha kwa makusudi kupiga Bismillahi wakati wa kumtomeza mnyama kwenda kuwinda, basi kilichowinda haijuzu kukikla:
    6. Hakuna Junaha kula kiwindwa kilichosahauliwa kupigiwa Bismillahi wakti wa kumtomeza mnayama wa kuwinda.
    7. Lazima mnyama aliyefunzwa kuwinda awe na uwezo wa kukamata na kujeruhi alichotumwa kukiwinda. Masharti mengine ni:
      a) Akitomezwa anatomezeka na kutii amri
      b) Akikatazwa na kukemewa anatii amri
      c) Akikamata mnyama hamli, bali anamjeruhi tu
      d) Awe anatunzwa sawasawa na kulindwa.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • DARSA YA BM.14\2 MLANGO WA KUWINDA NA KUCHINJA

    Hadithi ya Leo, Jumattanoe, tarehe 7, Rajab, 1446, sawa na tarehe 8, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUWINDA NA KUCHINJA

    SEHEMU YA PILI

    1332 – عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  { “مَنِ اتَّخَذَ كَلْباً، إِلَّا كَلْبَ مَاشِيَةٍ، أَوْ صَيْدٍ، أَوْ زَرْعٍ، اِنْتَقَصَ مِنْ أَجْرِهِ كُلَّ يَوْمٍ قِيرَاطٌ” } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Atayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa kuswaga wanyama, mbwa wa kuwinda au mbwa wa kulinda shambani, thawabu zake kila siku zitapunguka kwa ukubwa wa Qirat moja.” Muttafaq alayhi.

    UFAFANUZI

    Hadithi hii, inayotungulia mlamgo huu wa Viwindwa, inatutahadharisha na dhambi za kufuga mbwa pasi na sababu ya msingi ya Kisharia, kuwa atayefanya hivyo, kwa lengo jengine lisilotajwa kwenye Hadithi husika, atapata dhambi za kupunguziwa thawabu za amali zake njema, wingi au uzito wa Qirati moja kila siku.

    Na Mtume ﷺ amefafanua katika Hadithi nyengine maana ya Qirati kwa kusema:
    قال ﷺ: “من تبع جنازة مسلم، وكان معها حتَّى يفرغ من دفنها، فإنَّه يرجع بقيراطين: كل قيراط مثل جبل أُحُد“.
    “Ataye sindikiza jeneza kwenda kuzika, mpaka pakamalizwa kuzikwa maiti, basi akiondoka kurudu kwake atatunukiwa thawabu za Qirati mbili, kila Qirati moja na sawa na ukubwa au uzito wa Jabal Uhudu.” Muttafaq alayhi.

    Hivyo, ni haijuzu kufuga mbwa kwa ajili ya mapambo tu; isipokuwa mbwa wa kuswaga wanyama wa mifugo, mbwa wa kuwinda au kulinda majumba na shambani. Hakuna junaha kufuga mbwa wa aina hiyo, wala hakuna junaha kuwashidanisha katika utiifu na kukimbia. Miongoni mwake ni mbwa wa kumuongoza mtu kipofu, ambaye kwa utiifu na uaminifu ni bora, zaidi, kuliko mbwa wa aina nyengine. 
    
    Wanazuoni wametuongezea ufafanuzi kwa kusema:

    الكلب حيوان ليس سبُعًا, ولا بهيمة، فهو من الخلق المركَّب؛ لأنَّه لو تمَّ له طباع السبعية، ما ألف النَّاس، ولو تمَّ له طباع البهيمة، ما أكل لحم الحيوان، وهو نوعان: أهلي، وسلوقي؛ نسبة إلى أسلوق وهي مدينة باليمن تنسب إليها الكلاب السلوقية، وكذا النوعين في الطبع سواء.
    “Mbwa si miongoni mwa wanayama pori, wala si miongoni mwa wanyama wa Mifugo ya kuliwa, na kwa maana hiyo, ni mnyama mwenye tabia iliyo changanyika, kimaumbile. Kwa sababu lau kama angelikuwa ni mnyama mwenye hulka za wanyama pori, asingeweza kuwazowea watu kimaumbile. Na kwa vile hana hulka ya wanyama wa mifugo, haijuzu kumla. Na mbwa wapo wa aina mbili: Mbwa wa mjini, anayechanganyika na kuishi katika jamii za watu hadi kuwazowea, na mbwa anayejulikana kwa jina la Saluuqiy, ambaye asili yake ni kutoka mji wa Asluuq huko Yemen, ambako ndiko wanakotoka mbwa wote wa aina ya Sauuqiyym katika enzi ya Mtume ﷺ. Na mbwa yeyote mwenye hulka ya mchanganiyo wa tabia hizo mbili, anaingia katika mkumbo wa kuitwa mbwa. Miongoni mwake ni buldogi (Bulldog, Dobermann) na kadhalika. Na wale ambao inajuzu kuwafuga ni wale wenye hulka ya Kufunzwa kuwinda wanayama halali, Kulinda mashamba na majumba, Kuswaga mifugo na Kuongoza vipofu. Hawa ndio wanaojuzu kufugwa na kufunzwa vizuri. Wasiokuwa wao, huitwa mbwakoko.

    Zaidi ni kuwa mate ya mbwa-koko, ambaye mwenye hulka ya kunusa na kula mizoga, ni najsi nzito katika Uwislamu. Mtume ﷺ amesema, kupitia kwa Abu Hurayra:

    عن أبي هريرة أنَّ رسول الله -صلى الله عليه وسلم- قال: “إذا شرب، وفى رواية إذا ولغ الكلب في إناء أحدكم فليغسله سبعاً، إحداهنَّ بالتراب” البخاري (172)، ومسلم (279)
    Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema “Amesema Mtume ﷺ “Mbwa (koko) akinywa kitu kutoka kwenye chombo cha mmoja wenu, au akiramba chombo cha mmoja wenu, basi akioshe chombo hicho mara saba, mojawapo wa mara hizo achanganye na mchanga.” Muttafaq alayhi.

    فهذا يدل على أنَّ نجاسة الكلب نجاسة مغلَّظة لشدَّة قذارته.
    Hii ni dalili wazi kuhusu Uchafu wa Unajisi wa mate ya mbwakoko, unaoweza kumdhuru mtu; ndiyo maana akatakiwa aoshe chombo chake kilicho rambwa na mbwakoko, mara saba kwa maji safi na mojawapo wa maosho hayo, maji yachanganwe na mchanga safi.

    NYONGEZA
    اكتُشفت بالمكبرات الحديثة أنَّ في لعاب الكلب ميكروبات معدية فتاكة؛ ولذا صارت نجاسته مغلظة، فلا يطهر ما أصابته إلاَّ بغسله سبع مرَّات، إحداهن بالتراب الَّذي يحمل قوَّة الإنقاء والتطهير.
    Wataalamu wa tafiti za matibabu, wamethibitisha, kupitia vyombo vyao vya kitabibu, kuwa mate ya mbwakoko yana vimelea hatari sana, ambavo haviwezi kuondoka kikamilifu na kufa, isipokuwa kwa kuoshwa na kuchanganya maji na mchanga. Hivyo, chombo kilicho rambwa au kuingia mate ya mbwakoko, hakitwahiriki isipokuwa kwa kuoshwa kwa maji mara saba, na mara moja kuchanganya na mchanga safi.
    Hivyo, ni muhimu sana kwa wenye kufunga mbwa anayejuzu kufugwa, kumfundisha na kumlinda asinuse wala kula mizoga, na hivyo inamaanisha amtunze kikamilifu tokea upande wa kumpa chakula, sawawasa, hadi kumfunza asile mizoga.
    اختلف العلماء هل اقتناؤه واتخاذه لغير حاجة، محرم، أو مكروه؟
    Wametofautiana wanazuoni kuhusu hukumu ya kufuga mbwa, kuwa je ni Haramu kufuga mbwa, pasi na haja, au ni makuruhu?
    فذهب الإمامان الشَّافعي وأحمد: إلى أنَّ اقتناءه محرَّم لما جاء من الأحاديث الصحيحة من شدَّة نجاسته، وعدم دخول الملائكة بيتًا هو فيه، ونقص الثواب والأجر باقتنائه لغير حاجة.
    Imam Shafi’I na Imam Ahmad bin Hanbal wamechukua msimamo kuwa kufuga mbwa, pasi na sababu ya kisharia, ni haramu, na dalili zao ni kuwa mbwa ametajwa kuwa ni nasi, kufika hadi kutoingia Malaika kwenye nyumba aliyomo mbwa, kama alivyo onya Mtume ﷺ na, zaidi, kuwa kufuga mbwa kunapelekea mtu kupunguziwa, kila siku, thawabu za amali zake njema uzito au ukubwa wa Jabal Uhud.
    قال في المجموع: وحكى الروياني عن أبي حنيفة جوازه.
    Abu Hanifa, hata hivyo, amechukua msimamo wa kuwa inajuzu kufuga mbwa; si haramu.

    قال النووي: ويجوز اقتناء الكلب للصيد أو الزرع أو الماشية بلا خلاف.
    Amesema Imam An-Nawawy: “Inajuzu kufuga mbwa wa kuwinda, au wa kulinda mashamba (na Majumba) au mbwa wa kulinda mifugo; hakuna khilafu katika hilo.
    وأمَّا اقتناؤه لحفظ الدور والدواب فوجهان مشهوران:
    Ama kufuga mbwa kwa ulinzi wa majumba na wanayama, kuna kauli mbili maarufu.
    أحدهما: لا يجوز؛ للخبر.
    KWANZA: Kuwa haijuzu, kuendana na Hadihi
    الثاني: يجوز؛ لأنَّه لحفظ مال، فأشبه الزرع والماشية.
    PILI: Inajuzu kwa sababu ya kulinda mali, miongoni mwake mali za mashamba na za mifugo.
    واختلف العلماء في جواز بيع الكلب:
    Khilafu nyengine ipo katika kujuzu au kutokujuzu kuuza mbwa.
    فذهب الإمامان الشَّافعي وأحمد: إلى بطلانه، وأنَّه لا يجوز؛ لما جاء في البخاري (5346)، ومسلم (1567) من حديث أبي مسعود عقبة بن عامر قال: “نهى رسول الله -صلى الله عليه وسلم- عن ثمن الكلب، ومهر البغي، وحلوان الكاهن”. وغيره من الأحاديث.
    Imam Shafi’I na Imam Ahmad wamechukua msimamo kuwa haijuzu kuuza mbwa kulingana na Hadihi ya Uqba bin Mas’ud na iliyopokewa na Bukhari na Muslim, isemayo:
    “Amekataza Mtume ﷺ thamaniya mbwa, au ujira wa umalaya na malipo ya mpiga ramli na kutazamia.” Kuna Hadithi nyengine zaidi zenye kukataza kupokea thamai ya mbwa.
    وقال بتحريم بيعه وبطلانه كل من: الحسن البصري، وربيعة، وحماد، والأوزاعي، وداود.
    Miongoni mwa wanazuoni waliochukua msiamamo wa uharamiu ni Al-Hasan Al-Basriyy, Rabi’a, Hammad, Al-Awza’I na Daud.
    وذهب أبو حنيفة: إلى جواز بيع الكلاب كلها، وأخذ ثمنها، وضمانها على من أتلفها. واختلف أصحاب مالك: فبعضهم أجاز بيع الكلب المأذون في إمساكه، وبعضهم قال: لا يجوز.
    Abu Hanifa amechukua msimamo wa kujuzu kuuza mbwa na kupokea thamani yake, na kama atatokea mtu akahusika na kupotea thamani hiyo, basi anapaswa kulipishwa. Ama wafuasi wa Imam Malik, wametofautiana; baadhi yao wamejuzisha aliye ruhusiwa kumfuga (yaani mbwa wa kulinda mifugo, mashamba na majumba, na mbwa wa kuwinda), lakini haijuzu kuchukua thamani ya mbwa wasiokuwa hao.
    واحتج من أجاز بيعه بما أخرجه مسلم (1569) من حديث جابر قال: “زجر النَّبي -صلى الله عليه وسلم- عن ثمن الكلب والسنور”، ولأنَّه يُباح الانتفاع به، ويصح نقل اليد فيه، والوصية به، فصح بيعه؛ كالحمار.
    Hoja na dalili ya wenye kujuzisha ni Hadithi iliyopokewa na Muslim kutoka kwa Jabir ikisema: “Amekataza Mtume ﷺ kuchukua thamani ya mbwa na thamani ya paka” Hii ni kwa sababu mbwa na paka (isipokuwa mbwa koko), ianjuzu kuwatumia kwa manufaa ya mwanaadamu, na inajuzu kupeyana zawadi, hata kuweka wasia juu yao, hivyo inajuzu kuwauza kama inavyo juzu kuuza puda.” Ameipokea Muslim, H.1569.
    وممَّن أجاز بيعه من السلف: جابر بن عبد الله، وعطاء، والنخعي.
    Miongoni mwa wanazuoni wa kale, waliojuzisha kuuza na kununua mbwa (sipokuwa mbwakoko) na paka, ni Jabir bin Abdillahi, ‘Atwa’a na An-Nakhai’y.

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Haijuzu kufuga mbwa, yoyote, pasi na sababu ya kisheria.
    2. Mwenye kufuga mbwa, pasi na sababu ya kisheria, anapunguziwa, kila siku, thawabu za amal zake njema, Qirati mmoja, mfano wa ukubwa au uzito wa Jabal Uhud.
    3. Miongoni mwa Hekima na Mafunzo ya Dini ya Uwislamu ni kulinda na kuhifadhi miili hadi viwiliwili vya mwnadamu kutokana na kila chenye madhara juu yake.
    4. Inajuzu kufuga mbwa wa aina tatu
      a. Mbwa wa ulinzi wa mifugo na wa kuswaga mifugo, ambao kazi yao kubwa ni kuilinda mifugo kutokana na wanyama mwitu, kama mbwamwitu, chui na kadhalika.
      b. Mbwa wa ulinzi wa mashamba, majumba na mali, hasa mashamba makubwa ambayo ni vigumu sana kwa wenye mashamba hayo kuyalinda hadi pembezoni mwake. Au majumba ambayo, wenye majumba hayo hawawezi kuyalinda kutwa kucha nje yake.
      c. Mbwa aliyefunzwa kuwinda wanayama halali, ambaye akitomezwa kwenye kumshika mnyama mwitu anaenda na kumkamata, pasi na kuishia kumla.
    5. Mbwakoko ni najsi mate yake, na njia pekee ya kutwahirisha palipo ramba na mbwakoko ni kupaosha mara saba, mara moja kuchanganya maji na mchanga.
    6. Tafiti mbali mbali zilizofanywa na wataalamu wa Magonjwa mbali mbali, na wakagundua kuwa mate ya mbwakoko ni hatari sana kwa mwanaadamu.
      Kugunduliwa na wataalamu wa tafiti mbali mbali, kuwa mate ya mbwakoko yana vimelea hatari sana, na njia pekee ya kuviua ni kuyaosha kwa maji na mchanga, ni dalili tosha ya Ukweli na Uhalali wa Utume wa Mtume Muhammad, ﷺ.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • DARSA YA BM.14\1 MLANGO WA KUWINDA NA KUCHINJA

    Hadithi ya Leo, Jumaane, tarehe 6, Rajab, 1446, sawa na tarehe 7, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUWINDA NA KUCHINJA

    SEHEMU YA KWANZA

    بَاب اَلصَّيْدِ وَالذَّبَائِحِ

    1. Mlango kuhusu Kuwinda na Kuchinja
      UTANGULIZI Neno الصيد hutumiwa kwa upande wa Lugha, kumaanisha Kiwindwa kinacho windwa. Amesema Mwenyezi Mungu katika Kitabu Chake:

    *يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنْتُمْ حُرُمٌ ۚ *.
    Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwindwa nanyi mmeharimia katika Hija. Al-Maida, 5:95)

    أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ (المائدة)
    Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini na kuvila, kwa faida yenu na kwa wasafiri (Al-Maida, 5-95-96)

    وتعريفه شرعًا: الصيد: هو اقتناص حيوان حلال متوحش طبعًا، غير مملوك، ولا مقدور عليه.
    Kwa upande wa Sharia, hata hivyo, maana yake ni Kuwinda mnyama halali, ambaye ni mnyama mwitu, hamilikiwi na mtu yeyote, wala hapatikani bure bure tu.

    وهو مباح بالكتاب، والسنَّة، والإجماع، والقياس:
    Na Uhalali wake umethibiti kupitia Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Sunna ya Mtume ﷺ tokea ya kauli hadi ya vitendo, na imethibiti, vile vile, kupitia Ijma’ na Qiyaas.
    قال تعالي: {أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ} [المائدة: 95 – 96].
    Kwa upande wa Qur’ani ni Auya mbili tulizo zinukuu hapo juu.

    Kwa upamde wa Hadithi, basi zipo nyingi sana, miongoni mwake ni Hadithi ya mwanzo ya mlango huu, iliyopokewa na Bukhari na Muslim, kutoka kwa Abu Hurayra.

    والأحاديث كثيرة، ومنها ما في البخاري (2322)، ومسلم (1575) من حديث أبي هريرة قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم-: “من اتخذ كلبًا -إلاَّ كلب صيدٍ، أو زرعٍ، أو ماشيةٍ- انتقص من أجره كل يوم قيراط“.
    Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Ataye fuga mbwa, isipokuwa mbwa wa kuswaga wanyama, mbwa wa kuwinda au wa kulinda shambani, thawabu zake kila siku zitapunguka kwa ukubwa wa Qirati moja.” (na qirati moja ni sawa na ukubwa au uzito wa Jabal Uhud.)

    وقد أجمع العلماء على حله، وإباحة أكله، ويقتضيه القياس الصحيح.
    Kwa upande wa Ijma’a, ni kuwa Wanazuoi wote wamekubaliana kuwa Viwindwa vyote ni haalali kuliwa, isipokuwa kilicho haramishwa kwa jina, na msimamo huo huo ndio wa daili ya Qiyas.

    ويُشترط لحلِّ الصيد أربعة شروط:
    Kuna masharti mane kuhusu kiwindwa halali:

    أحدها: أهلية الصَّائد، وهو الَّذي تحل ذبيحته.
    Kwanza: Kuhusu mwindadaji mwenyewe, naye ni yule ambaye inajuzu kula aliochokichinja.
    الثاني: الآلة، وهي نوعان:
    PILI: Kifaa kilichotumiwa kuwindia. Navyo ni aina mbili:

    إمَّا آلة حادة، أو سهم يخرق الجلد.
    Ama kitu kikali kinachoweza kukata mishipa ya damu, kama kisu, au kitu kikali kama mshare unaoweza kutoboa mwili wa kiwindwacho na kuingia mwilini mwake.
    والنوع الثاني: الجارح المعلَّم؛ كالكلب، والصقر.
    Aina ya pili ni Kufunzwa kiwindaji kwenda kuwinda, kama mbwa au Kipanga. Hivyo haijuzu kuliwa alichoenda mwenyewe kukimata bila ya kutumwa.

    الثالث: إرسال الآلة قاصدًا للصيد؛ فلا يحل إنْ استرسل بنفسه.
    SHARTI LA TATU: Kutumwa kiumbe kiwindaji, kwenda kuwinda kiwindwaji, na Si kutokana na kukurupka mwenyewe akakamata mnyama kwa ajili ya afsi yake.

    الرَّابع: قول الصائد: “باسم الله” عند إرسال جارحه، أو سهمه؛ فلا يُباح ما لم يذكر عليه اسم الله تعالى من عالِمٍ عامد.
    SHARTI LA NNE: Kupiga Bismillahi, wakati wa kumtuma mnyama wako kwenda kuwinda, au wakati wa kulenga mshare wako au mkuki wako au hata bunduki yako, kumlenga mnyama uliyemkusudia kumwinda. Hivyo, haijuzu kula mnayma aliyewindwa, bila ya kupiga Bismillahi; kwa makusudi, ilhali unagua kuwa umefanya hivyo kwa makusudi.

    Wanazuoni wakazidi kutufafanulia kwa kusema:

    والصيد أفضل مأكول؛ لأنَّه حلال لا شبهة فيه.
    Chakula bora kabisa miongoni mwa vyakula vilivyo halalishwa ni Viwindwa, kwa sababu, kimsingi, ni halali na hamna shubha yoyote (wasiwasi) ndani yake.

    وقال أيضًا: الزراعة أفضل مكتسب؛ لأنَّها أقرب إلى التوكل من غيرها، وأقرب للحل، ومنها عمل اليد، والنفع العام للآدمي، والدواب.
    Wengine wamesema: Mazao ya kilimo ndio chumo bora kabisa, kwa sababu ni pato lenye kutegemea kutawakali kwa Mwenyezi Mugu, kuliko pato lollote jengine, na hivyo ndiyo halali bora. Ndiyo maana miongoni mwa mapato bora kabisa ni chumo la mikono yako, na pato lolote lemye kunufaisha zaidi mwanaadamu na wanyama, kama maji ya mvua au maji ya mto au majani yanayo ota wenyewe.

    وقيل: التجارة أفضل المكاسب، وأفضلها التجارة في البز والعطر، وأبغضها التجارة في رقيقٍ، وصَرْفٍ؛ للشبهة.
    Wegine wamesema kuwa Pato bora kabisa ni pato linalotokana na biashara, hasa biasahra ya mavazi na ya manukato, na pato baya kabisa ni pato la kutokana na kuuza watumwa, au kuwakodisha; kwa sababu mna shubha ndani yake.

    ويُسن التكسب، ومعرفة أحكامه؛ قال تعالى: {هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِنْ رِزْقِهِ} [الملك: 15].
    Kufanya kazi ya kujipatia pato lako mwenywe ni Sunna, na inapendekezwa kujifunza Hukumu zake. Mwenyezi Mumgu Amesema: “

    Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa. (Al-Mulk,67:15)

    فالأخذ بالأسباب المباحة المشروعة من التوكل.
    Hivyo, kuchukua hatua sahihi na halali, ili kujipatia riziki yako, ni miongoni mwa Kuktawakali kwa Mwenyezi Mugu. [syo OmbaOmba majiani au kwenye milango ya watu, wakupe au wasikupe. Haijuzu, ni kujiongezea kunyimwa kupewa na Mola wako!]

    Baada ya Utamgulizi huo, sasa tusome Hadithi alizotuwekea Imam Ibn Hajr:

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! ‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • Kitabu cha Vyakula

    DARSA YA BM.13\1 KUHUSU KITABU CHA VYAKULA

    Hadithi ya Leo, Alhamisi, tarehe 17, Mfungo Tisa, 1446, sawa na tarehe 19, Disemba, 2024

    KUHUSU VYAKULA

    SEHEMU YA KWANZA
    كِتَاب اَلْأَطْعِمَةِ
    13. KITABU CHA VYAKULA
    UTANGULIZI

    Neno أطعمة maana yake kwa upande wa lugha ya Kiarabu, ni vyakula. Na vyakula ni vitu vyovyotre vinavyo liwa au kunuyewa.

    Mwenyezi Mungu Amesema kwenye Surat A-Baqara:

    إِنَّ اللَّهَ مُبْتَلِيكُمْ بِنَهَرٍ فَمَنْ شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَنْ لَمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّي
    Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo si pamoja nami, na asiye kunywa atakuwa pamoja nami

    قال القرطبي: “دلَّ على أنَّ الماء طعام.
    Amesema Imam Al-Qurtuby, katika kuifasiri Aya hii: “Hii ni dalili kuwa maji ni chakula.”

    Wanazuoni wamezidi kufafanua kwa kusema:

    الأصل في الطعام والشَّراب والِّلباس: الحل؛ فلا يَحرم منها إلاَّ ما حرَّمه الله ورسوله؛ لأنَّها داخلة في عموم العادات المبنية على الحل، والمحرَّم منها محدودٌ ومعدودٌ، ممَّا يدل على بقاء المتروك على أصله، وهو العفو.
    Kila kitu kuanzia chakula, vinywaji na mavazi ni halali; isipokuwa kilichokatazwa na kuharamisha na Mwenyezi Mumgu na Mtume Wake. Hii ni kwa sababu kila kitu kilichoumbwa kinaingia katika vtu vilivyo halalishwa; na hivyo ni halali. Na vitu vya haramu ni vichache na vinajulikana. Hivyo, kila kitu ambacho hakijakataza ni halali, kimsingi, na hivyo hakuna kupatilizwa.

    والأصل في هذا القول وصف النَّبي -صلى الله عليه وسلم- ووصف شريعته:

    Na chanzo cha ufafanuzi huo wa wanazuoni, ni maneno ya Mwenyezi Mungu kuwaelezea wenye kumfuata Mtume Wake, katika mafundisho yake ya Sharia: 

    الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِنْدَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ يَأْمُرُهُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنْزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
    Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye – hao ndio wenye kufanikiwa. (Al-A’faaf, 7:157)

    وهذا يتناول جميع الأشياء: من مطعم، ومشرب، فكل ما ليس بخبيثٍ فهو طيبٌ حلال، فدخل فيه أنواع الحبوب، والثمار، وهي أوسع الأصناف حِلاًّ، ودخل فيه الحيوانات البحرية كلها، ودخل فيه الأنعام الثمانية، والخيل، ودخل فيه الطيور، والدجاج، والطواويس، ونحوها من حيوانٍ، وطيرٍ، إلاَّ ما كان خبيثًا.
    Hivyo, vinaingia kila kitu kuanzia Chakula na Vinywaji, ambavyo si miongoni mwa vitu viouvu na vichafu, basi ni halalali. Kwa maana hiyo, yanaingia mazao na mavuno yote ya chembechembe, matunda, mbogamboga na kadhalika. Wanaingia, vile vile, wanayama wote wa baharini, ambao hawawezi kuishi baharini na nchi kavu kwa pamoja, wanaingia vile vile, wanyama wa mifugo, pamoja na Farasi, kuwa wote ni halali kuliwa. Wanaingia vile vile, ndege wa aina zote, ambao hawawindi kwa makucha yao, kama Njiwa, Zuwarde, Mnana, Kuku, Tausi na kadhalika..

    Hivyo, kila kilicho kizuri ni halali na kila kilicho kiovu ni haramu.

    والخبث يعرف بأمور:
    Na vitu viuovu hujulikana kwa njia mbali mbali.

    • -1 أنْ ينص الشَّارع على خبثه؛ كالخنزير والحمر الأهلية*.
    1. Kitu chochote kilichoelezewa na Sharia kuwa ni kitu kiovu, kama kula nyama ya nguruwe au punda wa mjini (kinyume na nyama ya pundamilia).

    -2 أو ينص على حدِّه؛ ككل ذي نابٍ من السِّباع، وكل ذي مِخْلَبٍ من الطير.

    1. Au kutajwa kwa sifa yake ovu, kama kuharamishwa kula nyama ya kila mnyama anayewinda kwa meno yake chonge (nabu), kama Simba, Chui, Mbwamwitu, Paka, Nyoka, Chatu, au anayewinda kwa makucha yake, kama Kipanga, Mwewe, Tai , Dubu na kadhalika.
      -3 أو يكون خبثه معروفًا؛ كالفأرة، والحية، والحشرات.
    2. Au mwenye kujulikana wazi wazi uovu wake, kama Panya, Buku, Nyoka na vidudu vengine vingi, kama Nzi, Viroboto, Mende, Kunguni, Mijusi, Buibui, Mbungo, Kupe na kadhalika.

    -4 أو يكون الشَّارع أمر بقتله، أو يكون نهى عن قتله.

    1. Au wanayma na viumbe vengine ambavyo Sharia imeamrisha kuviua, au kukataza kuviua, kama aina mahasusi ya nyoka **ذي الطفتين والأبتر, wenye madhara ya kupofoa macho, wakikutikana majumbani, na mijusi.

    -5 أو يكون معروفًا بأكل الجيف؛ كاخنزير، والنسر، والرخم، ونحوهما.

    1. Au wanayama wenye kujulikana kula mizoga, kama Nguruwe, Mbwamwitu, Bweha, Kipanga, Tai, na kadhalika.

    -6 أو يكون متولدًا من بين حلال وحرام، فيغلَّب التحريم، كالبغل.

    1. Au mnyama aliyezaliwa katika uchotara, mmojawapo wa wazazi wake ni halali, lakini mzazi wa piliharamu, kama Nyumbu.

    -7 أو يكون خبثه عارضًا؛ كالجَلاَّلة التي تغذى بالنَّجاسة، والمائعات المتنجسة.

    1. Au mnyama ambaye uovu wake ni wa kutokana na kitendo chake, kama mnyama anayekula najisi, au vitu vya haramu, kama kuku aliyekula kinyesi. Uharamu wake utaendelea mpaka asafike tumboni kutokana na najisi aliyokula, na kila kilicho katazwa kwa unajisi wake.
      -8 أو يكون محرَّمًا لضرره البدني؛ كأنواع السموم.
    2. Au mnyama aliyeharamishwa kutokana na madhara yake ya sumu, kimaubile, kama nyoka wote wenye sumu, Nge, Tandu, Vyura venye sumu.

    9 –أو يكون محرَّمًا لضرره العقلي؛ كالخمر، والمخدرات.

    1. Au kilichoharamishwa kutokana na madhara yake mwilini au akilini, kama Pombe, Bangi, Kasumba, Mirungi na madawa ya kulevya.

    -10 أو مذكَّى؛ تذكية غير شرعية؛ إمَّا لآلته، وإمَّا لمذكِّيه، وإمَّا للقصد من تذكيته.

    1. Au mnayama aliyeuawa au kuchinjwa kinyume na kisharia, kama kumuua kwa kumpiga jiwe, au kumnyonga, au amechinjwa kwa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kama kuchinjwa kwa matambiiko ya kishirikina, au mizimu na mapango, au mchinjaji si Mwislamu, na kadhalika.

    وما لم يوجد فيه سبب الخبث فهو حلال.
    Hivyo, mnyama yoyote au kitu chochote kisichokuwa na mojawapo wa sifa hizo kumi zilizotajwa hapo juu, basi ni halali kula au kunywa. Miongoni mwao ni Mifugo ya kawaida, ikiwa pamoja na Sungura, Kiboko, Tembo, Mamba, Nyati, Pomboo, Nyagumi, Twiga, Pundamilia, Senene, Panzi na Nzige hata Guruguru. Ilimradi auawe kisharia, kama kumchinja, au kumuua kwa mkuki au hata kwa bunduki, kwa nia ya kumhalalisha kumla.

    Baada ya Utnagulizi huo, sasa tusome Hadtithi alizotuwekea Imam Ibn Hjar katika Mlango huu wa Vyakula.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO*

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com