Category: Hadith

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumatatu, tarehe 26 Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 30, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    56- بَاب: الْجَهْرِ فِي الْمَغْرِبِ

    1. Mlango: Kisomo cha kusikika katika swala ya Magharibi

    439- عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ يَقْرَأُ فِي الْمَغْرِبِ بِالطُّورِ.( ) [رواه البخاري: 765].

    1. Imepokewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im رضي الله عنه akisema: “Nimemsikia Mtume ﷺ anasoma surat Tuur katika swala ya magharibi.” [Bukhari: 765]

    57- بَاب: الْجَهْرِ فِي الْعِشَاءِ

    1. Mlango: Kisomo cha kudhihirishaau kusikika katika swala ya Ishaa

    440- عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: صَلَّيْتُ خَلْفَ أَبِي الْقَاسِمِ ﷺ الْعَتَمَةَ فَقَرَأَ: ]إِذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ[[الانشقاق: 1] فَسَجَدَ، فَلاَ أَزَالُ أَسْجُدُ بِهَا حَتَّى أَلْقَاهُ.( )[رواه البخاري: 766].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Nimeswali nyuma ya Abu Qaasim ﷺ swala ya ishaa akasoma: “Idhas samaaun shaqqat (Al-Inshiqaaq:1) katika rakaa ya mwanzo, alipofika kusujudu akasujudu basi na mimi tokea siku hiyo kila nikisoma sura hiyo na nikafika mahali pa kusujudu nasujudu na nitaendelea kufanya hivyo mpaka siku nitakayokutana na mtume ﷺ huko akhera.” [Bukhari: 766]

    441- عَنْ الْبَرَاءِ رضي الله عنه : أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ كَانَ فِي سَفَرٍ، فَقَرَأَ فِي الْعِشَاءِ فِي إِحْدَى الرَّكْعَتَيْنِ بـ وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ. [التين: 1] [رواه البخاري: 767].

    1. Imepokewa kutoka kwa Al Baraa bin ‘Azib رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ alikuwa katika safari, akasoma katika swala ya isha katika rakaa za mwanzo: “Wattiini wa zzaytuun. (At-Tiin:1)” [Bukhari: 767]

    442-وَفِي رِوَايَةٍ أُخْرَى قَالَ: وَمَا سَمِعْتُ أحدًا أَحْسَنَ صَوْتًا مِنْهُ أَوْ، قِرَاءَةً. [رواه البخاري: 769].

    1. Riwaya nyengine ya Al Baraa رضي الله عنه amesema: “Na sijapata kumsikia mtu ana sauti nzuri na kisomo kizuri kwa kusoma Qur’an kama sauti niliyokuwa nikiisikia anasoma Mtume ﷺ na kisomo chake ni kizuri kuliko kisomo cha mtu yeyote.” [Bukhari: 769]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumapili, tarehe 25 Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 29, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    54- بَاب: الْقِرَاءَةِ فِي الظُّهْرِ

    1. Mlango: Kisomo katika swala ya Adhuhuri

    436- عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ ﷺ يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَتَيْنِ الْأُولَيَيْنِ مِنْ صَلاَةِ الظُّهْرِ بِفَاتِحَةِ الْكِتَابِ وَسُورَتَيْنِ، يُطَوِّلُ فِي الْأُولَى، وَيُقَصِّرُ فِي الثَّانِيَةِ، وَيُسْمِعُ الْآيَةَ أحيانًا، وَكَانَ يَقْرَأُ فِي الْعَصْرِ بِفَاتِحَةِ الْكِتَابِ وَسُورَتَيْنِ، وَكَانَ يُطَوِّلُ فِي الْأُولَى، وَكَانَ يُطَوِّلُ فِي الرَّكْعَةِ الْأُولَى مِنْ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَيُقَصِّرُ فِي الثَّانِيَةِ. [رواه البخاري: 759].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ alikuwa akisoma rakaa mbili za mwanzo za swala ya adhuhuri suratil Fat’ha na sura mbili, katika rakaa ya mwanzo anasoma sura ndefu kidogo na katika rakaa ya pili anasoma sura fupi ya aliyosoma katika rakaa ya mwanzo wakati mwengine anasoma kwa sauti tunamsikia, wakati mwengine anasoma wakati wa Laasiri Suratul Fat’ha halafu na sura mbili katika rakaa zilizosalia na alikuwa akarefusha kisomo katika rakaa ya mwanzo na akafupisha kisomo katika rakaa ya pili na alikuwa naasoma katika rakaa ya mwanzo ya swala ya subuhi sura ndefu na akatika rakaa ya pili ya swala ya subuhi akisoma sura fupi.” [Bukhari: 759]

    UFAFANUZI

    Yaani katika swala mtume ﷺ alikuwa nasoma sura yoyote ambayo kama ni ndefu kidogo basi rakaa ya pili baada ya Al Fat’ha sura yake itakuwa fupi, ndiyo alikuwa akifanya hivyo katika swala zote za rakaa nne, tatu au trakaa mbili.

    55- بَاب: الْقِرَاءَةِ فِي الْمَغْرِبِ

    1. Mlango:Kisomo katika swala ya magharibi

    437- عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ أُمَّ الْفَضْلِ سَمِعَتْهُ وَهُوَ يَقْرَأُ: ]وَالْمُرْسَلاَتِ عُرْفًا[[المرسلات: 1] فَقَالَتْ: يَا بُنَيَّ، وَاللَّهِ لَقَدْ ذَكَّرْتَنِي بِقِرَاءَتِكَ هَذِهِ السُّورَةَ، إِنَّهَا لآخِرُ مَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِﷺ يَقْرَأُ بِهَا فِي الْمَغْرِبِ. [رواه البخاري: 763].

    1. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنهما akisema: “Ummu Fadhwl alimsikia Ibn Abbas anasoma katika swala walmursalaat ghurfa akasema Ummu Fadhwl kumwambia Ibn Abbas: “Ewe kijana wangu, Wallah kwa kisomo chako hichi umenikumbusha kisomo cha mtume ﷺ kwa sababu sura hii ndiyo sura ya mwisho niliyomsikia mtume ﷺ anaisoma katika swala ya magharibi.” [Bukhari: 763]

    438- عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ ﷺ يَقْرَأُ فِي الْمَغْرِبِ بِطُولَى الطُّولَيَيْنِ.( )[رواه البخاري: 764].

    1. Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Thaabit رضي الله عنه akisema: “Nimemsikia Mtume ﷺ anasoma katika swala ya magharibi rakaa mbili za mwanzo sura ndefu ndefu.” [Bukhari: 764]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • KCWW. 51/7 MLANGO WA MATUMAINI

    Hadithi za Marudio Jumapili, tarehe 25 Mfungo Sita, 1446, sawa ‎na 29 Septemba 2024.‎

    KUHUSU KUWA NA MATUMAINI NA MWENYEI MUNGU

    SEHEMU YA NANE NA YA MWISHO.‎

    ‎51- Mlango wa Matumaini

    Amesema Mwenyezi Munguسبحانه وتعالي ‏‎ :-‎

    Na rehema Yangu imeenea (imefunika) kila kitu (al-A’raaf: 156)‎

    ‎443. Imepokewa kutoka kwa Abu Nujayh, ‘Amr bin ‘Abasa –al-‎Sulamiyyرضي الله عنه ‏‎ akisema: Nilikuwa nikihisi, enzi za Ujahiliyya ‎‎[kabla ya Uwislamu] kwamba watu, kwa ujumla, wamepotea; hawafuati ‎haki hata kidogo kwani walikuwa wanaabudu masanamu. (Hadithi ndefu ‎kuhusu kusiliumu kwake Makka hadi kukutana tena na Mtume ‎ﷺ ‏Madina. ‎Anaendelea: ) ‎

    Basi nikafunga safari kwenda Madina. Nilipofika nikamwendea na ‎kumwambia: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Unanikumbuka?” ‎Akasema: “Ndiyo! Wewe ndiye yule uliyekutana nami Makka.” ‎

    Nikasema:“Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nieleze kile ‎Alichokuelimisha Mwenyezi Mungu na ambacho mimi sikijui! Nielimishe ‎kuhusu Swala.” ‎

    Akasema: “Swali swala ya asubuhi, na kisha jizuwiye kuswali ‎mpka baada ya kuchomoza Jua na kuinuka urefu wa mkuki – kwani, ‎wakati huo, huwa linachomoza baina ya pembe mbili za Shetani, na ‎wakati huo ndio makafiri wanalisujudia Jua. ‎

    Baada ya hapo, unaweza kuswali, kwani swala wakati huo inatambuliwa ‎na huandikiwa thawabu yule mwenye kuiswali, mpaka kivuli cha mkuki ‎kilingane na urefu wake. Ifikapo wakati huo, jizuwiye kuswali; kwani ‎wakati huo ndio pale Moto wa Jahannam unapokolezwa kuni. Kivuli ‎kikipindukia zaid [ya urefu wa kivuli cha mkuki], unaweza kuswali; ‎kwani swala wakati huo inatambuliwa na huandikiwa thawabu yule ‎mwenye kuiswali hadi kuswali swala ya Asr. ‎

    Baada ya Asri, jizuiye kuswali mpaka Jua lichwe, kwani linakuchwa ‎baina ya pembe mbili za Shetani, na wakati huo ndio makafiri ‎wanalisujudia.” ‎

    Nikasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Nieleze kuhusu ‎udhu.” Akasema: ‎

    ‎“Yeyote yule anayejisogezea maji ya kutawadha, akasukutua, na kutema, ‎kisha akapandisha maji puani na kuyatoa, basi kwa kufanya hivyo, ‎makosa yote ya viungo vya uso wake, kinywa chake na pua yake ‎hupukutika na hutoweka, pamoja na maji hayo. ‎

    Kisha akiosha uso wake, kama alivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu, ‎basi makosa yote ya uso –kwa pande zote mbili za ndevu zake- ‎hupukutika na maji hayo. ‎

    Kisha akiosha mikono yake mwili, hadi kwenye vifundo viwili, basi ‎makosa ya mikono yake hupukutika, pamoja na maji, kwenye ncha za ‎vidole vake. ‎

    Kisha akipangusa kichwa chake, basi makosa ya kichwa chake ‎hupukutika, na maji, kwenye ncha za nwele zake. ‎

    Kisha akiosha miguu yake miwili hadi kwenye vifundo viwili vya miguu, ‎basi makosa ya miguu yake hupukutika, pamoja na maji, kupitia ncha za ‎vidole vyake. ‎

    Akisimama akaswali, akamshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu na ‎kumtukuza kama Anavyo stahiki kusifiwa na kutukuzwa, na akaelekeza ‎moyo wake wote kwa Mwenyezi Mungu, basi makosa yake yote ‎hutoweka na kuwa hana makosa kabisa, kama siku aliyozaliwa na mama ‎yake.”‎

    Basi ‘Amr bin ‘Abasa akamsimulia Hadithi hii Abu Umama –‎swahaba wa Mtume ‎ﷺ ‏‎. Abu Umama akamwambia ‘Amr: “Ewe ‘Amr! ‎Tahadhari na unayosema! Mtu anapewa malipo yote hayo uliyotaja ‎mahali pamoja!” ‎

    ‎‘Amr akamjibu: “Ewe Abu Umama! Mimi nimesha zeeka, mifupa yangu ‎imeshadhoofika, mauti yananisogelea, na sina haja kumsingizia ‎Mwenyezi Mungu wala Mjumbe Wake! Lau ningekuwa sikumsikia ‎Mtume ‎ﷺ ‏akisema maneno hayo, si mara moja, si mara mbili, si mara tatu ‎‎(akahisabu mpaka saba) basi nisingeliyasimulia kamwe. Lakini, ukweli ni ‎kwamba nimemsikia akisimulia mara nyingi sana.” Ameipokea Muslim. ‎‎[Angalia pia Hadithi Nan.131]‎

    Amesema Imam Nawawi: Maneno ya Mtume ‎ﷺ ‏‎: “Baina ya pembe ‎mbili za Shetani.” yaani kuelekea kwenye kichwa chake, na ni mfano wa ‎kumaanisha kuwa wakati huo ndio wakati ambao Shetani na wafuasi ‎wake wanafanya vitimbi vyao vya kufuru na kutaka kuwashirikisha ‎wengine.” ‎

    ‎444. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ariyy ‎رضي الله عنه ‏akisema: Amesema Mtume ‎ﷺ ‏‎ ‎

    ‎“Akiutakia kheri umma Mwenyezi Mungu, basi humchukua Mtume wao ‎kabla ya wao, na kumfanya awe mtayarishaji wao wa mambo mazuri, na ‎pia hazina yao Siku ya Kiyama. ‎

    Na akiutakia shari umma basi huuangamiza vile Mtume wao yungali hai; ‎akiona kwa macho yake jinsi wanavyo angamizwa. Na huko ni ‎kumliwaza kwa walivyo mkadhibisha na kukataa kufuata maamrisho ‎yake kwao.” Ameipokea Muslim.‎

    UFAFANUZI.‎

    Hadithi hizi mbili na Aya iliyotangulia, zinatuhitimishia maudhui ya ‎mlango huu, ya kuwa na matumaini mema na Mwenyezi Mungu. Kwani ‎Kutawadha udhu kamilifu, na kuswali rakaa mbili kwa utulivu na – sunna ‎ya baada ya kutawadha- kunatosha kuwa ndio sababu ya kufutiwa ‎dhambi zote –isipokuwa dhambi kubwa kubwa ‎الكبائر ‏‎. ‎

    Na itoshe, kwetu sisi, kushukuru kwamba Umma huu, ambao sisi tumo, ‎tumerehemewa na Mwenyezi Mungu ‎سبحانه وتعالى ‏‎ kwa kumchukua ‎Mtume Wake na kutuacha sisi tumfuatie mmoja mmoja, ili atutangulie ‎mbele ya Mwenyezi Mungu. Hiyo, peke yake, inatosha kutupa matumaini ‎makubwa kwa Mola wetu.‎

    YALIYOMO NA YATOKANAYO.‎

    ‎1.‎ Fadhila za Udhu na fadhila za rakaa mbili za sunna ya Udhu.‎
    ‎2.‎ Umuhimu wa kutawadha kikamilifu na kuswali kwa unyenyekevu.‎
    ‎3.‎ Inakatazwa kuswali baada ya Swala ya Alfajiri, wakati wa ‎kuchomoza Jua, hadi liinuke kadiri ya urefu wa mkuki.‎
    ‎4.‎ Inakatazwa kuswali baada ya Swala ya Laasiri na wakati Jua ‎linakuchwa. ‎
    ‎5.‎ Nyakati hizi mbili ni vibaya –yaani makuruhu- kuswali swala ‎yoyote, pasi na dharura.‎
    ‎6.‎ Fadhila za Kuswali Swala ya Dhuha, na wakati wake ni tokea ‎baada ya Jua kuinuka urefu wa mkuki, hadi majira ya Swala ya ‎Adhuhuri –i.e. kivuli cha urefu wa mkuki kuwa sawa na urefu wa ‎mkuki weneywe, upande wa magharibi-. ‎
    ‎7.‎ Fadhila za Sunna baada ya Adhuhuri na kabla ya kuswali Swala ya ‎Laasiri. Kwani wakati huo, hata malaika huswali pamoja, na ‎kushuhudia Sunna zako.‎
    ‎8.‎ Wajibu na Umuhimu wa unyenyekevu katika Ibada.‎
    ‎9.‎ Ukosefu wa unyenyekevu, katika ibada, unapunguza thawabu za ‎ibada hiyo.‎
    ‎10.‎ Fadhila na Umuhimu wa Mwislamu kuwa na matumaini mema na ‎Mwenyezi Mungu.‎
    ‎11.‎ Kuwa na matumaini na Mwenyezi Mungu ni kutenda mema na SI ‎kubweteka.‎
    ‎12.‎ Kubweteka na kujipa matumaini kwa Mwenyezi Mungu ni ‎kujidanganya.‎
    ‎13.‎ Kutawakali ni kumuamini Mwenyezi Mungu na kutenda ya ‎aliyokuamrisha kuyatenda.‎
    ‎14.‎ Fadhila za Abu Nujayhi ‎رضي الله عنه ‏
    ‎15.‎ Uangavu, umakini na ukali wa ubongo wa Mtume ‎ﷺ‎ kumtambua ‎mtu, aliyekutana naye, zaidi ya miaka 10 iliyopita!‎
    ‎16.‎ Hima, hekima na busara ya Mtume ‎ﷺ‎ katika kuongoza na ‎kuelimisha Maswahaba wake.‎
    ‎17.‎ Umma wa Muhammad ‎ﷺ ‏‎ umebahatika kwa kutopatilizwa, kabla ‎ya yeye kuitikia Wito wa Mola wake.‎
    ‎18.‎ Kutangulia kwa Mtume, yeyote yule, kwenda kwa Mola wake ni ‎rehema kwa Umma wake.‎
    ‎19.‎ Watu walioangamizwa kabla ya vifo vya Mitume wao, ‎wamelaaniwa na kutengwa na Rehema za Mwenyezi Mungu.‎
    ‎20.‎ Hatari ya kwenda kinyume na mafundisho na mafunzo ya Mtume ‎Muhammad ‎‏’ﷺ ‏‎; kwani hakuna usalama kwa kufanya hivyo.‎
    ‎21.‎ Uokofu ni kufuata aliyokuja nayo Bwana wetu, Muhammad ‎ﷺ‎ , tu.‎

    والله أعلم
    ‏ ‏
    وبالله التوفيق‎ ‎

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم.‏

    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    Kutoka Kitabu cha: Kitalu cha Waja Wema: Maneno ya Muokozi ‎wa ‎Umma, ‎ambacho ni tafsiri kamili ya ‎رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين للإ ‏مام ‏النووي ‏‎ ‎kilicho tungwa na Imam An-Nawawi na kufasiriwa kwa ‎Kiswahili ‎na Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aal Shaykh Abi Bakr bin Salim ‎آل الشيخ ابى ‏بكر بن سالم‎.‎

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 28, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    53- بَاب: وُجُوبِ الْقِرَاءَةِ لِلْإِمَامِ وَالْمَأْمُومِ فِي الصَّلَوَاتِ كُلِّهَا، فِي الْحَضَرِ وَالسَّفَرِ، وَمَا يُجْهَرُ فِيهَا وَمَا يُخَافَتُ

    1. Mlango: Wajibu wa kusoma Imam na maamuma katika swala yote ikiwa wako safarini au hawamo safarini na kisomo gani kinasomwa kwa sauti na kisomo gani kinasomwa kwa sauti ya chini chini

    433- عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رضي الله عنه قَالَ: شَكَا أَهْلُ الْكُوفَةِ سَعْدًا إِلَى عُمَرَ رضي الله عنه ، فَعَزَلَهُ وَاسْتَعْمَلَ عَلَيْهِمْ عَمَّارًا، فَشَكَوْا حَتَّى ذَكَرُوا أَنَّهُ لاَ يُحْسِنُ يُصَلِّي، فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ فَقَالَ: يَا أَبَا إِسْحَاقَ! إِنَّ هَؤُلاَءِ يَزْعُمُونَ أَنَّكَ لاَ تُحْسِنُ تُصَلِّي، قَالَ: أَمَّا أَنَا، وَاللَّهِ فَإِنِّي كُنْتُ أُصَلِّي بِهِمْ صَلاَةَ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ مَا أَخْرِمُ عَنْهَا، أُصَلِّي صَلاَةَ الْعِشَاءِ، فَأَرْكُدُ فِي الْأُولَيَيْنِ،( ) وَأُخِفُّ فِي الْأُخْرَيَيْنِ. قَالَ: ذَاكَ الظَّنُّ بِكَ يَا أَبَا إِسْحَاقَ. فَأَرْسَلَ مَعَهُ رجلًا – أَوْ رِجَالًا – إِلَى الْكُوفَةِ، فَسَأَلَ عَنْهُ أَهْلَ الْكُوفَةِ، وَلَمْ يَدَعْ مَسْجِدًا إِلاَّ سَأَلَ عَنْهُ، وَيُثْنُونَ عَلَيْهِ مَعْرُوفًا، حَتَّى دَخَلَ مَسْجِدًا لِبَنِي عَبْسٍ، فَقَامَ رَجُلٌ مِنْهُمْ، يُقَالُ لَهُ أُسَامَةُ بْنُ قَتَادَةَ، يُكْنَى أَبَا سَعْدَةَ، قَالَ: أَمَّا إِذْ نَشَدْتَنَا، فَإِنَّ سَعْدًا كَانَ لاَ يَسِيرُ بِالسَّرِيَّةِ،( ) وَلاَ يَقْسِمُ بِالسَّوِيَّةِ، وَلاَ يَعْدِلُ فِي الْقَضِيَّةِ.( )قَالَ سَعْدٌ: أَمَا وَاللَّهِ لاَدْعُوَنَّ بِثَلاَثٍ: اللَّهُمَّ إِنْ كَانَ عَبْدُكَ هَذَا كَاذِبًا، قَامَ رِيَاءً وَسُمْعَةً،( ) فَأَطِلْ عُمْرَهُ، وَأَطِلْ فَقْرَهُ، وَعَرِّضْهُ بِالْفِتَنِ. وَكَانَ بَعْدُ إِذَا سُئِلَ يَقُولُ: شَيْخٌ كَبِيرٌ مَفْتُونٌ، أَصَابَتْنِي دَعْوَةُ سَعْدٍ. قَالَ الرَّاوي( ) عَنْ جَابِرٍ: فَأَنَا رَأَيْتُهُ بَعْد قَدْ سَقَطَ حَاجِبَاهُ عَلَى عَيْنَيْهِ مِنْ الْكِبَر وَإِنَّهُ لَيَتَعَرَّضُ لِلْجَوَارِي( )فِي الطِّرِيقِ يَغْمِزُهُنَّ. [رواه البخاري: 755].

    1. Imepokewa kutoka kwa Jabiir bin Samura رضي الله عنه akisema: “Wat wa Kufa walimshitaki Sa’d kwa Umar رضي الله عنه Madina (Sa’d alikuwa gavana wa Umar huko Kufa) Umar akamuuzulu wadhifa aliompa huko na badala yake akamtawadha Ammar kuwa ndiyo awe anaongoza Kufa, wakaenda kumshitaki kwa Umar kwamba haswalishi vizuri, Umar akamtumia ujumbe: “Ewe Abu Ishaq watu wako wa Kufa wanadai kwamba wewe huwaswalishi vizuri” akajibu kwa kusema: “Wallah mimi siwaswalishi swala isipokuwa swala niliyokuwa nikiswali na mtume ﷺ na akimuona mtume ﷺ anavyoswalisha, sijapunguza chochote katika swala zangu, nawaswalisha swala ya isha na ninasoma katika rakaa mbili za mwanzo nasoma sura ya wastani lakini katika rakaa mbili za mwisho nafupisha sana kisomo, nafanya wepesi” anasema Umar: “Walio kushitaki wamekushitaki kutokana na udhanifu tu ewe Abu Ishaq” basi akatuma watu akimfuatanisha na Sa’d arudi Kufa na huyo aliyefuatanishwa naye akatakiwa awaulize watu wa Kufa nini wanavyomuelewa na kumfahamu Sayyidina Sa’d, kwa hivyo wakapita misikiti yote ya Kufa wakiuliza nakwa watu wote wanamsifu tu mpaka akaingia msikiti mmoja wa Bani ‘Absi akasimama mtu mmoja katika watu hao anaitwa Usama in Qataadah na anaitwa kwa jina la utani Aba Sa’ada, yeye akasema: “Ikiwa unataka tukueleze ukweli basi Sa’d ni mtu anajiweka nyuma, anatuma wanajeshi kwenda mahala yeye mwenyewe haendi wala hagawi kwa usawa na uadilifu, wala hafanyi uadilifu katika hukumu zake anazozitoa Sa’d yuko hapo hapo, alivyosikia hivyo akasema: “Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu nitaapiza kwa dua tatu: Ewe Mola wangu ikiwa mja wako huyu anayoyasema haya ni muongo na amesimama hapa kwa kujionesha na kutaka umaarufu tu basi nakuomba umpe umri mrefu lakini vilevile umzidishie ufakiri wake na umuonje kwa fitina na mitihani mbalimbali” anasema Jaabir: “Basi nikamuona mtu huyo ambaye aliapizwa na Sa’d nilikutana nae baadae akiwa mzee sana amejawa na maaswi akisema: Maapizo ya Sa’d yamenipata” anasema msimulizi wa hadithi hii kutoka kwa Jaabir kwamba: Na mimi nilimuona mtu huyu baadae kope zake na nywele zake zinaning’inia kutokana na uzee na anapita vichochoroni akiwakonyeza konyeza wanawake na kuwagusa gusa na kuwatomeza tomeza.” [Bukhari: 755]

    434- عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رضي الله عنه : أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «لاَ صَلاَةَ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِفَاتِحَةِ الْكِتَابِ».[رواه البخاري: 756].

    1. Imepokewa kutoka kwa ‘ubadah bi Swamitرضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Hana swala yeyote yule ambaye hatosoma suratul Fat’ha ndani ya swala.” [Bukhari:756]

    435- عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه : أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ دَخَلَ الْمَسْجِدَ، فَدَخَلَ رَجُلٌ فَصَلَّى، فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ ﷺ فَرَدَّ، وَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ» فَرَجَعَ يُصَلِّي كَمَا صَلَّى، ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ ﷺ ، فَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ»فَرَجَعَ يُصَلِّي كَمَا صَلَّى، ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ ﷺ ، فَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ» ثلاثًا، فَقَالَ: وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ، مَا أُحْسِنُ غَيْرَهُ، فَعَلِّمْنِي. فَقَالَ: «إِذَا قُمْتَ إِلَى الصَّلاَةِ فَكَبِّرْ، ثُمَّ اقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنْ الْقُرْآنِ، ثُمَّ ارْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَعْدِلَ قَائِمًا، ثُمَّ اسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، وَافْعَلْ ذَلِكَ فِي صَلاَتِكَ كُلِّهَا».[رواه البخاري: 757].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ aliingia msikitini akatokea mtu akaswali sunna kisha akamuendea na kumsalimia, mtume ﷺ akamjibu salam yake lakini kamwambia: “Rudi ukaswali kwani hujaswali” yule mtu akaenda akaswali kama alivyoswali mwanzo kisha akarudi kumsalimia mtume ﷺ , akamuitikia mtume ﷺ kisha akamwambia: “Rudi ukaswali tena kwa sababu hujaswali” yule mtu akarudi akaswali kama alivyoswali mara ya mwanzo na ya pili kisha akamjia mtume ﷺ akamsalimia, mtume ﷺ akamwambia: “Hapana rudi ukaswali kwani bado hujaswali” mara tatu yule mtu akasema: “Ninaapa kwa yule amekuleta ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa haki, sijui kufanya vizuri zaidi ya nilivyofanya, basi nifundishe” Mtume ﷺ akamwambia: “ukisimama kwenda kuswali piga takbira kisha soma Qur’an unayoweza kuisoma kisha rukuu na ukirukuu tulia katika rukuu yako kisha inuka usimame wima na utulie, kisha sujudu na unaposujudu tulia sawasawa kisha inuka katika sijida ukae kitako na tulia katika kitako na fanya hivyo hivyo katika swala yako yote na rakaa zote.” [Bukhari:757 ]

    UFAFANUZI

    Hadithi hii inaitwa hadithi ya Al Musiiu fiy Swalat(Mtu aliyeswali kimakosa swala yake na vipi mtume ﷺ amemfundisha kufanya). Na ndiuyo maana hadithi hii inatumiwa na Maimamu wote kwamba ukitaka kwenda kuswali hakuna kunuia kwa makelele kusema nina swali swala ya isha maamuma, Hapana. Kama alivyosema mtume ﷺ anamwambia: “ukisimama elekea qibla sema: Allahu Akbar basi ushanuia. Nia yako ni huko kusimama ndiyo niya ya kuswali na swala unaijua mwenyewe unayoswali…….siyo kuomboleza.

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • KCWW. 51\6 MLANGO WA MATUMAINI

    Hadithi za Marudio Jumamosi, tarehe 24 Mfungo Sita, 1446, sawa na 28 Septemba ‎‎2024.‎

    KUHUSU KUWA NA MATUMAINI NA MWENYEZI MUNGU

    SEHEMU YA SITA

    ‎51- Mlango wa Matumaini

    Amesema Mwenyezi Munguسبحانه وتعالي ‏‎ :-‎

    ‎1.‎ Na rehema Yangu imeenea kila kitu (Al-A‘raaf, 7: 156)‎

    ‎434. Imepokewa kutoka kwa Jabir ‎رضي الله عنه ‏‎ akisema: Amesema Mtume ‎ﷺ ‏‎: “Mfano wa Swala tano [kuziswali kila siku] ni mfano wa kuwepo mto wenye maji ‎mengi, mbele ya mlango wa nyumba ya mmoja wenu, ambaye hukoga kwenye mto ‎huo mara tano kila siku.”Ameipokea Muslim. ‎

    ‎435. Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Abbasرضي الله عنهما ‏‎ akisema: Nimemsikia ‎Mtume ‎ﷺ ‏‎ akisema: “Hatokufa Mwislamu akaswaliwa swala ya maiti na watu ‎arubaini, wasio mshirikisha Allah na kitu chochote kile, isipokuwa Mwenyezi ‎Mungu Atawakubalia dua zao njema wanazo muombea maiti huyo.”Ameipokea ‎Muslim. ‎

    ‎436.. Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas‘udرضي الله عنه ‏‎ akisema: Tulikuwa ‎kama watu arubaini, hivi, pamoja na Mtume ‎ﷺ ‏‎ ndani ya kuba [hema la duara] ‎akasema: “Je, mtaridhika mkiwa robo ya watu wa Peponi?’ Tukasema: “Ndiyo!” ‎Akasema: “Je, mtaridhika mkiwa thuluthi moja ya watu wa Peponi?” Tukasema: ‎‎“Ndiyo!” Akasema: ‎

    ‎“Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake! Mimi nataraji kuwa ‎mtakuwa nusu ya watu wa Peponi; kwa sababu haingii mtu Peponi isipokuwa ‎mwenye kuisalimisha nafsi yake kwa Mwenyezi Mungu. Na wingi wenu nyinyi, ‎kulingana na wingi wa wale wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, ni kama wingi ‎wa unyoya mweupe kwenye ngozi ya ng’ombe mweusi, au unyoya mweusi kwenye ‎ngozi ya ng’ombe mwekundu.” Muttafaq ‘alayhi. ‎

    ‎ ‎ ‎437. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa al-Ash‘ariyyرضي الله عنه ‏‎ akisema: ‎Amesema Mtume ‎ﷺ ‏‎: “Itapofika Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu Atamkabidhi ‎kila Mwislamu mmoja, Yahudi mmoja au Nasrani mmoja, na kumwambia: Huyu ni ‎fidia yako ya kuokoka na Moto.” ‎

    Riwaya nyengine ya Abu Musa vile vile, inasema: “Amesema Mtume ‎ﷺ‎: ‎‎“Watakuja watu miongoni mwa Waislamu Siku ya Kiyama, wakiwa na madhambi ‎mengi, mfano wa milima, lakini Mwenyezi Mungu Atawasamehe dhambi zao hizo.” ‎Ameipokea Muslim. ‎

    Amesema Imam Nawawi: Maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Huyu ni ‎fidia yako ya kuokoka na Moto.” inaweza kueleweka zaidi kutokana na Hadithi ‎nyengine, iliyopokelewa kutoka kwa Abu Hurayra, isemayo: “Kila mtu ana makaazi ‎yake Peponi na makaazi mengine Motoni. Mwenye kuamini akiingia Peponi, basi ‎makaazi yake ya Motoni huchukuliwa na kafiri; kwa sababu anastahiki makaazi ‎hayo kwa ukafiri wake” Na maana ya “Fidia yako” ni kwamba: ulihatarika kuingia ‎Motoni na huyu ndiye fidia yako; kwa sababu Mwenyezi Mungu Ameshatuwekea, ‎tangu azali, idadi ya wataoujaza Moto. Hivyo, wakisha ingia makafiri Motoni, kwa ‎kufuru zao, wanakuwa kama wamewafidia Waislamu nafasi zao Motoni. Na ‎Mwenyezi Mungu anajua zaidi!‎

    ‎438. Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umarرضي الله عنهما ‏‎ akisema: Nimemsikia ‎Mtume ‎ﷺ ‏‎ akisema: “Mwenye kuamini atasogezwa karibu na Mola wake, Siku ya ‎Kiyama, mpaka afunikwe na rehema Zake, kisha Amhoji kwa madhambi yake; ‎Atamwambia: “Unakumbuka dhambi fulani na dhambi fulani?” Atajibu: “Ndiyo ‎Mola wangu! Nakumbuka.” Atamwambia: “Nilikusitiri nazo [nilikufichia] duniani, ‎na leo Mimi Nakusamehe na kukufutia.” Basi atakabidhiwa ukurasa wa amali zake ‎njema.” Hadithi zote hizi ni Muttafaq ‘alayhi

    UFAFANUZI

    Hadithi za sehemu hii zinaendelea kutufahamisha kuwa mwenye kumuamini, kwa ‎dhati, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hapaswi kukata tamaa na Rehema za ‎Mwenyezi Mungu, ilimradi tu anajitahidi kufanya amali njema, na kutaraji Rehema ‎za Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa amali njema muhimu kabisa ni Swala ‎Tano za kila siku, ambazo anaye dumisha kuziswali, kila siku, hufutiwa dhambi ‎zake zote kama alivyosema Mwenyezi Mungu :‎
    وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ (هود,11 : 114 ‏‏) ‏‎ ‎
    ‎“Na dumisha Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu ‎na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao ‎kumbuka.” (Huud, 11:114). ‎

    Hivyo, mfano wa kudumisha Swala tano kila siku, ni mfano wa mtu anayelazimika ‎kuogelea, mara tano, kwenye maji mengi yaliyopo mbele ya nyumba yake, kila ‎anapo toka au kurudi nyumbani, na hivyo kumfanya asafike na kila uchafu uliyopo ‎juu ya mwili wake. ‎

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    ‎1.‎ Umuhimu wa kudumisha Swala tano kila siku.‎
    ‎2.‎ Kudumisha Swala tano kunapelekea kufutiwa madhambi yote madogo ‎madogo.‎
    ‎3.‎ Umuhimu wa Waumini walio hai kumuombea msamaha maiti Mwislamu.‎
    ‎4.‎ Shafaa, kwa aliyekufa, ni KUMUOMBEA na SI KUMUOMBA maiti! ‎Kumuomba maiti ni SHIRK!‎
    ‎5.‎ Swala ya maiti ni muhimu sana na ni Ibada ya kumuombea maiti.‎
    ‎6.‎ Umuhimu wa watu wengi sana kumswalia maiti; huenda pakapatikana, ‎miongoni mwao, watu 40 au zaidi, wasiomshirikisha Mwenyezi Mungu na ‎kitu chochote, na ambao wakimuombea msamaha watakubaliwa.‎
    ‎7.‎ Dua ya mja asiyemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote hairudi ‎mikono mitupu. Hivyo, ukikutana na mcha Mungu (yuhai kama wewe) ‎muombe akuombee dua!‎
    ‎8.‎ Maombezi ya mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ‎hayakubaliwi.‎
    ‎9.‎ Wingi wa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa waja Wake, ‎ni sawa na WINGI wa manyoya ya ng’ombe mweusi, mwenye UNYOYA ‎MMOJA MWEUPE, mwilini mwake!‎
    ‎10.‎ Washirikina ni wengi sana kuliko Waumini halisi. Mwenyezi Mungu ‎Amesema: ‎‏ وما أكثر الناس ولو حرصت بمؤمنين ‏‎“Hata ufanye hima gani, bado ‎wengi wa wanadamu si watu wenye kuamini (ni washirikina).‎
    ‎11.‎ Dharura ya kuwa macho, kwa kila ulifanyalo, kuhakikisha ‎HUMSHIRIKISHI Mwenyezi Mungu na kitu chochote kile: khasa katika ‎KUOMBA!‎
    ‎12.‎ Waja wengi wataoingia Peponi watatoka kwenye Umma wa Muhammad ‎ﷺ ‏‎ ‎‎.‎
    ‎13.‎ Hatoingia Peponi ila mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu. ‎
    ‎14.‎ Bishara njema kwa Waumini wa Muhammad ‎ﷺ ‏
    ‎15.‎ Pepo na Moto zimeshaumbwa na Mwenyezi Mungu na kila moja itakuwa na ‎ujazo sawasawa wa idadi ya viumbe Vyake. (Yaani ukubwa wa kila moja ‎unaweza kuchukua viumbe vyote alivyo viumba Mwenyezi Mungu)‎
    ‎16.‎ Waliokufuru au kumshirikisha Mwenyezi Mungu, watatolewa kwenye ‎nafasi za ujazo wao Peponi, na walio muamini wanachukua nafasi zao ‎Peponi; vile nafasi za ujazo wao Motoni –kwa kumuamini Mwenyezi ‎Mungu- zitachukuliwa na wale walionyimwa nafasi zao Peponi, kwa ‎kumshirikisha Mwenyezi Mungu. [Ufafanuzi wa Imam Nawawi, ambao ni ‎sahihi, unatokana na Hadithi Swahihi aliyoinukuu katika Ufafafnuzi wake, ‎رحمه الله ‏‎)‎
    ‎17.‎ Dharura na umuhimu wa kuamini, na hatari na tahadhari ya kumshirikisha ‎Mwenyezi Mungu na kitu chochote.‎
    ‎18.‎ Fadhila za Mwenyezi Mungu kwa baadhi ya waja Wake, wenye kumuamini ‎kwa dhati, ambao atawasitiri duniani na Akhera.‎
    ‎19.‎ Kukiri kosa ni sawa na kuomba kufutiwa kosa ‎ألإعتراف يمحو ألإقتراف‎.‎
    ‎20.‎ Umuhimu wa kumsitiri Mwislamu kadiri iwezekanavyo.‎
    ‎21.‎ Mlango wa Toba upo wazi na ni mpana sana.‎

    وبالله التوفيق ‏

    الحقير إلى الله تعالى عبد القادر شريف آل الشيخ ابى بكر بن سالم

    INAENDELEA….. ‎

    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
    Kutoka Kitabu cha: Kitalu cha Waja Wema: Maneno ya Muokozi wa Umma, ‎ambacho ni tafisri kamili ya ‎رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين للإ مام النووي ‏kilicho ‎tungwa na Imam al-Nawawi na kufasiriwa kwa Kiswahili na Sayyid Abdulqadir ‎Shareef.‎
    NI RUHUSA KUNUKUU NA kuweka kwenye FB yako au kwenye Whatsup na ‎kwenye Makundi ya Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha Dini. Changia kusambaza Dini, ujipatie thawabu.‎
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Ijumaa, tarehe 23 Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 27, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    50- بَاب: رَفْعِ الْبَصَرِ إِلَى الْإِمَامِ فِي الصَّلاَةِ

    1. Mlango: Ruhusa ya kumuangalia Imam ndani ya swala

    430- عَنْ خَبَّابٍ رضي الله عنه ، قِيلَ لَهُ: أَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَقْرَأُ فِي الظُّهْرِ وَالْعَصْرِ؟ قَالَ: نَعَمْ. قِيلَ لَهُ: بِمَ كُنْتُمْ تَعْرِفُونَ ذَاكَ؟ قَالَ: بِاضْطِرَابِ لِحْيَتِهِ. [رواه البخاري: 746].

    1. Imepokewa kutoka kwa Khabbab رضي الله عنه akisema: Aliulizwa je, Mtume ﷺ alikuwa anasoma chochote katika swala ya dhuhuri na laasiri? Khabba akasema: “Ndiyo” akaulizwa: “Mlijuaje kama anasoma?” akasema: “Tulikuwa tunaangalia ndevu zake zinavyotikisika.” [Bukhari: 746]

    51- بَاب: رَفْعِ الْبَصَرِ إِلَى السَّمَاءِ فِي الصَّلاَةِ

    1. Mlango: Kuhusu kuinua macho kuangalia mbinguni ilhali umo ndani ya swala

    431- عَنْ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «مَا بَالُ أَقْوَامٍ يَرْفَعُونَ أَبْصَارَهُمْ إِلَى السَّمَاءِ فِي صَلاَتِهِمْ» فَاشْتَدَّ قَوْلُهُ فِي ذَلِكَ، حَتَّى قَالَ: «لَيَنْتَهُنَّ عَنْ ذَلِكَ، أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ».[رواه البخاري: 750].

    431.Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ : “Kwanini baadhi ya watu wanainua nyuso zao na kuangalia mbinguni ilhali wamo ndani ya swala.” Basi mtume ﷺ akawa anakaripia sana jambo hilo mpaka akasema: “Ama watu hao waache kufanya hivyo venginevyo Mwenyezi Mungu atawapofoa macho.” [Bukhari: 750]

    52- بَاب: الِالْتِفَاتِ فِي الصَّلاَةِ

    1. Mlango: Kugeuka geuka ndani ya swala

    432- عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ عَنْ الِالْتِفَاتِ فِي الصَّلاَةِ فَقَالَ: «هُوَ اخْتِلاَسٌ يَخْتَلِسُهُ الشَّيْطَانُ( )مِنْ صَلاَةِ الْعَبْدِ».[رواه البخاري: 751].

    1. Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها akisema: “Nilimuuliza Mtume ﷺ kuhusu kugeuka geuka ndani ya swala, akanijibu kwa kusema: “kufanya hivyo ni uchochezi anaoufanya shetwani kumchochea mwenye kuswali ageuke geuke kwenye swala.” [Bukhari:751 ]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • BM.14.11\5a3 MLANGO WA UHARAMU WA JUJIMILIKISHA MALI YA MTU MWENGINE

    Hadithi ya Leo, Ijumaa, tarehe 23, Mfungo Sita, 1446, sana na tarehe 27, Septemba, 2024

    SEHEMU YA TATU

    KUHUSU UHARAMU WA KUJIMILIKISHA MALI YA MTU

    1257 – وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ خَبَّابٍ [ قَالَ ]: سَمِعْتَ أَبِي  يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ  يَقُولُ: { ” تَكُونُ فِتَنٌ، فَكُنْ فِيهَا عَبْدَ اَللَّهِ اَلْمَقْتُولَ، وَلَا تَكُنْ اَلْقَاتِلَ” } أَخْرَجَهُ ابْنُ أَبِي خَيْثَمَةَ. وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ.

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Habab رضي الله عنه akisema: “Nilimsikia baba yangu akisema: “Amesema Mtume : “Kutazuka fitina\chokochoko katika siku zijazo. Zikitokea fitina hizo ni bora wewe uwe aliyeuliwa na siyo aliyeua.” Ameipokea Abu Haithama na Dara-Qutni.

    1258 – *وَأَخْرَجَ أَحْمَدُ نَحْوَهُ: عَنْ خَالِدِ بْنِ عُرْفُطَةَ عن رسول الله 

    1. Riwaya ya Ahmad kutoka kwa Khalid bin ‘Urfutwah رضي الله عنه sawa na hadithi ya hapo juu.

    UFAFANUZI
    Hadithi hii, inayotufungia Mlango huu na vile vile KItabu cha Hudud, katika Kitabu cha Bulughul Maram, katika riwaya zake zote mbili, kuoka kwa Mtume  inatutahadharisha kuwa kutatokea fitina na chokochoko katika Umma wa Kiislamu, ambapo watu mbali mbali, wataingizwa au kujikuta wanapaswa kuingia katika fitina hizo, na hivyo kuzuka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja anataka kumuua mwenziwe. Hivyo Mtume ﷺ ametuonya kutojiingiza kaatika chokochoko hizo, na badala yake amesema kuwa ikilazimika basi bora uwe miongoni mwa wataouawa, kuliko kuwa mingoni mwa wauwaji. Hivyo, mwenye kumuamioni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, asijiingize kwa njia yoyote ile, si kwa kauli wala kwa silaha katika chokochoko na Fitina zitazozuka, akaanza kupigana na kuwaua watu wengine. Kama ni lazima apigane basi ni kheri yeye auwawe lakini katu asipigane na kuua.

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Onyo la Mtume ﷺ kwa watu wote wa Umma wake, kuwa kutazuka Fitina na chokocoko, ambapo kutazuka mtafaruko mkubwa sana wa kuuwana Waislamu wenyewe kwa wenyewe, na hivyo kila mmoja ajaribu kadiri awezavyo asijiingize kwa njia yoyote katika Fitina hizo.
    2. Fitina hizo ziatzushwa na kuchochewa na Maadui wa Uwislamu na Waislamu, na kupigiwa debe na baadhi ya Waislamu, tokea upande wa viongozi wao hadi waislamu wa kawaida.
    3. Mwenye kujikuta ameingizwa kwenye Fitina na Chokochoko, bila ya kutaka, basi afadhali awe ni mtu aliyeuliwa pasi na haki, kuliko kuwa miongoni mwa wauwaji wa Waislamu wenziwao.
    4. Haramu na ni Dhuluma kushangilia na kuunga mkono mauwaji ya Waislamu.
    5. Mwenye kujiingiza au kuunga mkono dhuluma dhidi ya Uwislamu na Waislamu, SI Mwislamu.
    6. Mtume ﷺ amesema: لا طاعة لمخلوق قى معصية الخالق “ Hakuna kumtii Kiumbe kwa kumuasi Muumba.”
    7. Dhambi za kumuua Muumini mmoja, pasi na haki, ni sawa na kuwaua wanaadamu wote duniani.
    8. Wajibu wa kujichunga na kujilinda na Wafitinishaji na Wauwaji wa Waislamu na Waumini wa Kiislamu, Duniani.
    9. Kuna Hadithi nyingi sana, kutoka kwa Mtume ﷺ zenye kuonya na kutahadharisha, kuhusu Fitina na Chokochoko, mbali mbali, zinazotungwa na kuoteshwa na Maadui wa Uwislamu na Waislamu, na ambazo huunga amkono na baadhi ya Waislamu wa Kawaida, bali hata baadhi ya Viongozi wao katika jamii zao na nchi zao.
    10. Hadithi zifuatazo ni baadhi ya Tahadhari zilizotolewa na Mtume ﷺ kwa Waislamu:

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    Limejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIA ZA MTUME ﷺLeo Alhamisi, tarehe 22 Mfungo Sita, 1446, H., sawa na tarehe 26, Septemba, 2024.WASIA WA 122مئتا وصية من وصايا الرسول ﷺجمعها ورتبها ثم فسرها إلى السواحليةالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIA ZA MTUME *ﷺ.Zimekusanywa na Kufasiriwa kwa Kiswahili naSayyid Abdulqadir ShareefMTIMISHI WA HADITHI ZA MTUME

    الوصية المئة والثانية والعشرون
    لا تَسُبُّوا الأمواتَ**
    122: Msiwatukane walio kufa
    وعن عائِشةَ رضي اللَّه عنها قالتْ: قال رسُولُ اللَّهِ ﷺ: « لا تَسُبُّوا الأمواتَ، فَإنَّهُمْ قد أفْضَوْا إلى ما قَدَّموا » رواه البخاري.

    Imepokewa kutoka kwa Bi. ‘Aisha *رضي الله عنها* akisema: Amesema Mtume ﷺ: “Msiwatukane walio kufa; kwani wameshayafikia waliyo yatenda.” Ameipokea Bukhari.,

    UFAFANUZI

    Kutukana maana yake ni Kumchamba mtu, Kumtusi, Kumnyonyoa, Kumkebehi, Kumaibisha, Kumkashifu kwa yasiyojulikana, Kumuaibisha mbele za watu na Kumfedhehesha. Ama mtu aliyekuwa akipotosha watu kwa makusudi, na kukufurisha wasiokuwa yeye na watu wake, na akawa ameacha athari zinazoendelea kuwapotosha watu na kuwakufurisha, basi ni wajibu kuendelea kuwatahadharisha watu kuhusu upotoshaji wake huo na uporovu wa kuwapotosha na kuwakufurisha watu, ili watu waache na kupuuza upotoshaji wake huo; na kwa maana hiyo, unachokizungumzia siyo Kinara wa upotoshai huo, bali UPOTOSHAJI WAKE, na kwa maana hiyo hakuna junaha kuwazindua watu kuhusu UPOTOSHAJI HUO. BALI NI WAJIBU JUU YA WANAZUONI KUWAZINDUA WATU NA UOVU HUO. UOVU ENDELEVU. HUO NI WAJIBU WA KUAMRISHA MEMA NA KUKATAZA MAOVU!

    *KUTOKA *NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIYA YA MTUME ﷺ*
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO!
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu!
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *Mrumiahi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*مختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME*Leo Siku ya Alkhamis, tarehe 22 Rabiil Awal, 1446, H., sawa na tarehe 26, Septemba, 2024. *

    (10)
    كِتَاب أبْوَابِ الأَذَانِ
    KITABU CHA MILANGO YA ADHANA

    49- بَاب: مَا يَقُولُ بَعْدَ التَّكْبِيرِ

    1. Mlango: Mtu anasema nini baada ya kupiga Takbiri katika swala

    427- عَنْ أَنَسٍ ﷺ: أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ وَأَبَا بَكْرٍ وَعُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، كَانُوا يَفْتَتِحُونَ الصَّلاَةَ: بِـــ: الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ.[رواه البخاري: 743].

    1. Imepokewa kutoka kwa Anas رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ na Abu Bakr na Umar رضي الله عنها walikuwa wanaanza kisomo katika swala zao kwa kusema: Alhadulillah Rabbil ‘Alaamiyn.”[Bukhari: 743]

    UFAFANUZI

    Hii ndiyo hadithi ambayo watu wa madhehebu ya Abu Hanifa na Ahmed wanasema kwamba Bismillah siyo lazima kuisema kwa sauti, unaisema kisirisiri halafu ndiyo unaanza kusema: Alhamdulillah Rabbil ‘alaamiyn. Lakini Imam Shaf’i anasema: Hapana kwa sababu ipo mtume ﷺ alikuwa akiswalisha kwa kusema: Bismillah Ar-rahmaani Rahiim, Alhamdulillah Rabbil ‘alaamiyn, yaani Aya moja moja na isitoshe Shafi’I anasema: Bismillah Rahmaani Rahiim ni sehemu ya suratil Fat’ha kwa sababu inaitwa Sabi’ul Mathani, sura ya Aya saba ukiondoa Bismillah Rahmaan Rahiim suratil Fat’ha inabakia na Aya sita kwa hivyo Shafi’I anasema: Hapana ilisomwa kwa sauti na lazima isomwe isipokuwa hakuna ulazima kusoma kwa sauti.

    428- عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَسْكُتُ بَيْنَ التَّكْبِيرِ وَبَيْنَ الْقِرَاءَةِ إِسْكَاتَةً،( ) فَقُلْتُ: بِأَبِي وَأُمِّي يَا رَسُولَ اللَّهِ! إِسْكَاتُكَ بَيْنَ التَّكْبِيرِ وَالْقِرَاءَةِ، مَا تَقُولُ؟ قَالَ:«أَقُولُ: اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ الْخَطَايَا كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الأَبْيَضُ مِنْ الدَّنَسِ،( ) اللَّهُمَّ اغْسِلْ خَطَايَايَ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ».[رواه البخاري: 744].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ alikuwa ananyamaza baada ya kupiga Takbiri na baina ya kuanza kusoma kwa sauti, nikamwambia: “Najitolea fidia mimi na mama yangu kwa nafsi yako ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi pale unaponyamaza baada ya kupiga Takbir na kabla ya kuanza kusoma kisomo cha sauti huwa unaomba dua gani?” Mtume ﷺ akasema: “Ninasemaاللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ الْخَطَايَا كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الأَبْيَضُ مِنْ الدَّنَسِ،( ) اللَّهُمَّ اغْسِلْ خَطَايَايَ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ [Ewe Mola wangu utenge mwili wangu na nafsi yangu mbali na makosa yangu kama ulivyotenganisha Mashariki na magharibi, Ewe Mola wangu nisafishe na unitakase kutokana na makosa yangu na dhambi zangu kama ilivyosafishwa nguo nyeupe kutokana na taka, Ewe Mola wangu nioshe mwili wangu kutokana na madhambi yangu kwa maaji na theluji na umande].” [Bukhari: 744]

    429- عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: حَدِيثُ الْكُسُوفِ، وَقَدْ تَقَدَّمَ.( )
    وَفِي هذِهِ الرِّوايَةِ قَالَتْ: قَالَ: «قَدْ دَنَتْ مِنِّي الْجَنَّةُ، حَتَّى لَوْ اجْتَرَأْتُ عَلَيْهَا لَجِئْتُكُمْ بِقِطَافٍ مِنْ قِطَافِهَا، وَدَنَتْ مِنِّي النَّارُ حَتَّى قُلْتُ: أَيْ رَبِّ، وَأَنَا مَعَهُمْ؟ فَإِذَا امْرَأَةٌ – حَسِبْتُ أَنَّهُ قَالَ: – تَخْدِشُهَا( )هِرَّةٌ،( ) قُلْتُ: مَا شَأْنُ هَذِهِ؟ قَالُوا: حَبَسَتْهَا حَتَّى مَاتَتْ جُوعًا، لاَ أَطْعَمَتْهَا، وَلاَ أَرْسَلَتْهَا تَأْكُلُ – حَسِبْتُ أَنَّهُ قَالَ:( )- مِنْ خَشِيشِ -أَوْخَشَاشِ( )-الأَرْضِ».[رواه البخاري: 745].

    1. Imepokewa kutoka kwa Asmaa binti Abu Bakr رضي الله عنهما kuhusu hadithi ya kupatwa jua imeshatangulia, Katika riwaya hiiamesema: “Amesema Mtume ﷺ : “Nimesogezewa pepo nikaiona mpaka nikawa hata ningeliweza kurusha mkono wangu nikachuma matunda ya miti yake….., na nimesogezewa moto nikauona mpaka nikaogopa na kumuomba Mola wangu nikasema: Ewe Mola wangu kwani na mimi nitakuwa na hao watakao ingizwa motoni?” anasema: “Na nikaangalia katika moto nikaona mwanamke anaparurwa kwa makucha na paka, nikauliza: Nini dhambi za mwanamke huyu? Nikaambiwa: Mwanamke huyu alimfunga paka mpaka akafariki kwa njaa hakumpa chakula wala hakumfungulia akamuacha akatoke nje akajitafutie rizqi yake kutokana na vyakula vilivyokuwepo juu ya ardhi.” [Bukhari: 700]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *MTumishi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • BM.14.11\5a.2 MLANGO WA UHARAMU WA JUJIMILIKISHA MALI YA MTU MWENGINE

    Hadithi ya Leo, Alhamisi, tarehe 22, Mfungo Sita, 1446, sana na tarehe 26, Septemba, 2024

    SEHEMU YA PILI

    KUHUSU UHARAMU WA KUJIMILIKISHA MALI YA MTU

    1256 -* وَعَنْ سَعِيدِ بْنِ زَيْدٍ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  :” مِنْ قُتِلَ دُونَ مَالِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ.” رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ*

    1. Imepokewa kutoka kwa Said bin Zayid رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Mtu yeyote Atayeuwawa akiwa anatetea mali yake atakufa kifo cha Shahid.” Wameipokea Maimamu wanne na ameisahihisha Tirmidhi.

    UFAFANUZI
    Hadithi hii, inayotufungulia Mlanmgo wa luharamu wa kujimilikisha kitu cha mtu mwengine, inatufundisha kuwa mtu akiuliwa, ilhali anatetea mali yake, kwa nguvu zote alizopewa na anazoweza kuzitumia ni wajibu mtakaatifu; na hivyo akiuliwa ilhali anatetea mali yake halali, basi atakuwa amefariki akiwa shahidi, kwa sababu ameuawa akitetea mali yake, kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu. Ndiyo maana mwenye kuuawa akitetea mali yake anakufa kifo cha daraja ya Shahidi katika Uwislamu.

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Hadithi ni dalili ya uhalali wa mtu kutetea mali yake ya halali; kwa sababu aliyekosa kuuawa katika vita vya Jihadi, akauawa akiwa anatetea mali yake, anapata daraja ya shahidi alioyeuawa vitani.
    2. Mwenye kutetea mali yake halali anatetea Tamko la Mwenyezi Mungu liwe juu na tamko la shetani liwe chini; hivyo yumo katika vita vya Jihadi.
    3. Pamoja na kupata thawabi za Shahidi, ila anaoshwa na kuvishwa sanda na kuswaliwa; isipokuwa daraja yake ni daraja ya Shahidi wa Jihadi.
    4. Ikiwa mwenye kuuawa akitetea mali yake anapata daraja ya Shahidi, basi atayeuawa akiteteea Watu wake wa nyumbani, au kujitetea mwenyewe, au kutetea nchi yake, anapata, vile vile, daraja ya Shahidi akiuawa kwa kutetea vyote hivyo.
    5. Daraja ya Shahidi katika Uwislamu, ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu kuwa Msimfikirie aliyeuawa akitetea Njia ya Mwenyezi Mungu, kuwa ni maiti, bali yuhai anaruzukiwa na Mola wake, anaruzukiwa.
      وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ (169) فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (170)
      Wala kabisa msiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanruzukiwa na Mola wao. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezzi Mungu kwa fadhila zake na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwmbaa haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. (Al-Imran, 3:168-69)

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    Limejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com