Category: Hadith

  • DARSA YA BM.14.4\12 MLANGO WA AQIQA

    Hadithi ya Leo, Jumatano, tarehe 13, Shaabani, 1446, sawa na tarehe 12, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUCHINJA MNYAMA WA AQIQA

    SEHEMU YA KUMI NA PILI

    1357 – وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا { أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَمْرَهُمْ أَنْ يُعَقَّ عَنْ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ، وَعَنْ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ } رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَه .

    1. Imepokewa kutoka kwa ‘Aisha رضي الله عنها akisema: “Mtume  aliwaamrisha watu wachinje mbuzi wawili wa aina moja, wenye kufanana kwa ajili ya mvulana na mbuzi mmoja kwa msichana.” Ameisahihisha Tirmidhi na kusema ni Hadithi Sahihi.
      1358 – *وَأَخْرَجَ اَلْخَمْسَة ُ عَنْ أُمِّ كُرْزٍ الْكَعْبِيَّةِ نَحْوَه *ُ.
    2. Imepokewa kutoka kwa Ummu Kursi رضي الله عنها sawa na hadithi ya hapo juu.

    UFAFANUZI

    Hadithi hii kutoka kwa Mama Aisha رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا inasema kuwa Mtume ﷺ aliwaamrisha Maswahaba wake wawachinjie watoto wao wa kiume mbazi wawili wawili, kila mmoja, na mbuzi hao wawe wanafanana kwa kila kitu, umri, uzima na kadhalika. Na wawachinjie watoto wao wa kike mbuzi mmoja, kila mmoja.  Hivyo, Hadithi hii inatuondolea mushkeli wa idadi ya wanyama wa Aqiqa wanaotakikana kuchinjiwa watoto na wazee wao, ama iwe kwa kiwango cha chini, ambapo kila mtoto achinjiwe mbuzi au kondoo mmoja mmoja, au kiwango cha juu, ambapo kila mtoto wa kiume achinjiwe mbuzi au kondoo wawili, vile mtoto wa kike anatakiwa achinjiwe kondoo au mbuzi mmoja. 
    Wanazuoni, wakazidi kutufafanulia kwa kusema:

    الحكمة في تمييز الذكر عن الأنثى أنَّ العقيقة هي نسيكة شكر لله تعالى على نعمة تجدد المولود، ولما كان الذكر أعظم نعمة، وامتنانًا من الله تعالى، كان الشكر عليه أكثر، فصار له شاتان، وللجارية شاة
    Na hekima ya kuwepo tofauti baina ya mtoto wa kiume na mtoto wa kike, katika kuwachinjia wanyama wa Aqiqa, ni kuwa Aqiqa ni Ibada ya نسيكة UCHAMUNGU wa utaratibu maalumu na wakati maalumu, katika kumshukuru Mwenyezi Mugu kwa neema ya kupewa mtoto wa kiume, ambaye ndiye atakuja kuwa mwenye kuendeleza kizazi cha Baba mchinjaji na kutunza nasaba yake kwa siku za usoni, na hivyo hiyo ni neema kubwa sana kupewa Baba mtu na Mola wake, na kila neema ikizidi ukubwa wake, basi na shukrani zake nazo zinakuwa kubwa zaidi. Ndiyo maana, mtoto wa kiume anatakiwa achinjiwe mbuzi au kondoo wawili, vile mtoto wa kike, ambaye bado ni neema vile vile, ila yeye hatokuwa muendelezaji wa ukoo wa Baba yake, bali atakuwa muendelezaji wa ukoo wa mumewe, ndiyo maana shukrani zake ni kuchinjia na Baba yake kondoo au mbuzi mmoja. Hakuna, junaha, hata hivyo, kuchinjiwa mtoto wa kike kondoo au mbuzi wawili vile vile. Kwa maneno mengine, uchinjaji wa Aqiqa kwa ajili ya mtoto wa kiume, ni نسك Ibada ya Uchamungu, yenye utaratibu wake maalumu, kama zilivyo Ibada za Hija na Umra, vile uchinjaji wa Aqiqa kwa mtoto wa kike ni Sadaka; haina utaratibu maalumu wala wakati maalumu

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Hadithi hii ni dalili nyengine kuwa Asasi ya Aqiqa ni Asasi halali iiyothibiti kupitia amri ya Mtume ﷺ kwa wafuasi wa Umma wake.
    2. Mtume ﷺ ameamrisha mtoto wa kiume achinjiwe mbuzi au kondoo wawili, na mtoto wa kike achinjiwe mbuzi au kondoo mmoja.
    3. Hadithi ni dalili, vile vile, kuwa Si kila amri inamaanisha wajibu kuitekeleza, maana hakujatajwa adhabu au dhambi yoyote kwa asiyechinja.
    4. Zaidi, ni kuwa kuna Riwaya nyingi zenye kuonesha kuwa kuchinja mnyama wa Aqiqa ni Sunna iliyotiiwa mkazo, si lazima kuchinja.
    5. Kuna tofauti baina ya نسك na صدقة. Nusuk ni Ibada ya vitendo inayotakiwa kutekelezwa kwa wakati wake kama alivyo itetekeleza Mtume ﷺ Vile Sadaka ni ibada ya vitendo, vile vile, ila haina wakati wake maalumu, wala utaratibu maalum, na ni Ibada ya kujitolea.
    6. Kuchinja wanyama wa Aqiqa kwa mtoto wa kiume ni Nusuk , lakini kuchinja mnyama wa Aqiqa kwa mtoto wa kike ni Sadaka.
    7. Si Sunna kumnyoa nywele mtoto wa kike; Mtume ﷺ hakuwanyoa wajukuu zake wa kike, kama Umama binti Abi-Al’as bin Ar-Rabi’, mjukuu wa Zainab binti Muhammad, mtoto mkubwa wa Mtume ﷺ.
    8. Baadhi ya wanazuoni, hata hivyo, wamechukua msimamo wa kumnyoa nywele mtoto wa kike, vile vile, baada ya kumchinjia mnyama wa Aqiqa.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • DARSA YA BM.14.4\11 MLANGO WA AQIQA*

    Hadithi ya Leo, Jumaane, tarehe 12, Shaabani, 1446, sawa na tarehe 11, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUCHINJA MNYAMA WA AQIQA

    SEHEMU YA PILI

    1355 – عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; { أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَقَّ عَنْ اَلْحَسَنِ وَالْحُسَيْنِ كَبْشًا كَبْشًا } رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ، وَعَبْدُ اَلْحَقّ، لَكِنْ رَجَّحَ أَبُو حَاتِمٍ إِرْسَالَه
    1355. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنهما akisema: “Mtume  aliwachinjia wajukuu zake wawili, Al-Hassan na Al-Husayn kila mmoja kondoo mmoja.” Ameipokea Abu Daud na ameisahihisha Ibn Khuzaima na Ibn Jarud na Abdulhaq. Ila Abu Hatim amesema kuwa Riwaya hiyo ni maneno ya Swahaba kumuelezea Mtume ﷺ.
    1356 – وَأَخْرَجَ اِبْنُ حِبَّانَ: مِنْ حَدِيثِ أَنَسٍ نَحْوَه

    1. Imepokewa, vile vile, Riwaya hiyo hiyo, kutoka kwa Anas bin Malik رضي الله عنه sawa na hadithi ya hapo juu.

    UFAFANUZI
    Hadithi hii, inayotufungulia mlango wa Aqiqa inatusimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas, kuwa Mtume ﷺ aliwachinjia wajukuuu zake wawili, Al-Hasan na Al-Husayn, watoto wa Fatma bint Muhammd na Aliyy bin Abi Twalib, aliwachinjia kondoo mmoja mmoja, kila mmoja. Ila kuna Hadithi nyengine, inasimulia kuwa Mtume ﷺ aliwachinjia wajukuu zake hao wa kiume, kila mmoja kondoo wawili. Tusome hadihi hiyo hapa chini:

    *وقد ورَد في حَديثٍ آخَرَ، أنَّ النَّبيَّ صلَّى الله عليه وسلَّم عقَّ عَنهُما: "كَبشَينِ، كَبشَينِ"، أي: ذبَحَ عن كلِّ واحدٍ مِنهُما كبشَينِ؛ وقيل: تُرجَّحُ روايةُ الكَبشَينِ بأمرَينِ؛ أحَدُهما: تضَمُّنُها زِيادةَ ثِقَةٍ مقبولةً، والثَّاني: مُوافَقتُها للأحاديثِ الأخرى التي نصَّ النَّبيُّ صلَّى اللهُ تَعالى عليهِ وسلَّم فيها على شاتَينِ، حيثُ يقولُ: "عَن الغلامِ شاتَانِ مُكافِئَتانِ"، أو لعلَّه ذبَحَ في يومِ وِلادَتِهما كبشًا وفي السَّابعِ كبشًا عن كلِّ واحدٍ مِنهُما، أو ذبَح النَّبيُّ صلَّى اللهُ علَيْه وسلَّم كبشًا مِن مالِه. وأمَر علِيًّا بكَبشٍ آخَرَ، فنُسِب إلى النَّبيِّ صلَّى اللهُ علَيْه وسلَّم لأمرِه له بذَلك*
    
    Hadithi nyengine inasema kuwa Mtume ﷺ aliwachinjiua wajukuu wake hao wawili wa kiume, kondoo wawili wawili kila mmoja, na wanazuoni wa Hadithi wamesema kuwa Riwaya ya kuchinjwa kondoo wawili wawili kwa kila mjukuu mmoja, ina nguvu zaidi kutokana na sababu mbili. Kwanza, Riwaya hii ya pili ina nyongeza kutoka kwa msimulizi muaminifu. Na pili, ni kuwa Riwaya hii inaendana na Riwaya nyingi nyengine zisemazo: Mtume ﷺ aliwachinjia wavulana wawili, kila mmoja mbuzi wawili. Hivyo, ama ina maana kuwa Mtume ﷺ aliwachinjia mbuzi mmoja mmoja kila mmoja, siku ya kuzaliwa, na kisha baada ya kutimia siku saba toke kuzaliwa, akawachinjia tena mbuzi mmoja mmoja kila mmoja; jumla mbuzi wawili kwa kila mvulana mmoja. Au alichinja kondoo kutoka na mali zake mwenywe, na baadae akamuamrisha Aliyy bin Abi Twalib, kama mzazi wa Al-Hasan na Al-Husyn, achinje kondoo wengine, na hivyo uchinjaji wote ukanasibishwa kwa Mtume ﷺ.

    روايةُ أخرى تقول “كبشًا كبشًا” للدَّلالةِ على مَشروعيَّةِ الاقْتِصارِ على ذَبْحِ كبشٍ واحدٍ عن الذَّكَرِ، وروايةُ “كَبشَين” للدَّلالةِ على أنَّ الأفضلَ والأتمَّ ذَبْحُ كبشَينِ؛ فإنَّ العدَدَ ليسَ شَرْطًا، بَلْ هو مُستَحَبٌّ

    Riwaya inayosema kuwa walichinjiwa kondoo mmoja mmoja kwa kila mtoto mmoja, ni dalili kuwa inajuzu kumchinjia mtoto mchanga mvulana, kondoo mmoja. Vile Riwaya inayozungumzia kuwa mtoto mchanga, mvulana, amechinjiwa kondoo wawili kila mvulana, ni dalili kuwa kwa mtoto wa kiume ni bora kumchinjia kondoo au mbuzi wawili, na mtoto wa kike, kumchinujia kondoo au mbulzi mmoja. Hivyo, idadi siyo sharti wala siyo wajibu, bali ni jambo linalo pendekezwa tu.

    ومِنَ سُنَنِ العَقيقَةِ: التَّفرِقةُ بينَ الغُلامِ والجاريةِ، بحَيثُ يُعَقَّ عن الغُلامِ بشَاتَينِ، وعن الجاريةِ بشاةٍ واحدةٍ؛ لصِحَّةِ الأحاديثِ بذلك

    Miongoni mwa Sunna za mnayma wa Aqiqa ni kutofautisha baina ya mtoto wa kiume na mtoto wa kike; ambapo mtoto wa kiume achinjiwe mbuzi au kondoo wawili, vile mtoto wa kike achinjiwe mbuzi au kondoo mmoja, kwa sabu kuna Hadithi nyingi sahihi zenye kusema hivyo.
    
    Na iwapo mtoto hakuchinjiwa na wazee wake, udogoni, mnyama wa Aqiqa na wazee wake, kutokana ukosefu wa hali na mali, au kuwa kusahau, au kutokana na kutokujua, basi mtoto mhusika, mwenywe, anaweza kujichinjia mnyama wa Aqiqa, hata ukubwani. Hakuna junaha.  Wanazuoni wa Fiqhi na Hadithi wamezidi kutufafanulia suala hili kama ifuatavyo:

    العقيقة مستحبة تذبح يوم السابع عن الذكر ثنتان وعن الأنثى واحدة، وإذا لم تذبح فلا شيء عليك، وإن ذبحت ولو بعد الكبر فذلك أفضل، والسنة أن تأكل منها أنت وأهل بيتك وتطعم من ترى من جيرانك والفقراء، وإن فرقتها بين الفقراء كلها أو بعضها فلا بأس، وإن أكلتها كلها أنت وأهل بيتك فلا بأس، ولكن الأفضل أن تطعم وتتصدق وتأكل
    Kuchinja mnyama wa Aqiqa ni Sunna iliyo pendekezwa kuifanya siku ya saba tokea kuzaliwa mtoto; Mtoto wa kiume achinjiwe wanyama wawili na mtoto wa kike achinjiwe mnyama mmoja. Na kama hajachinijiwa basi hakuna dhambi yoyote. Na akichinjiwa, hata baada ya mtoto husika kuwa mtu mzima, basi ni jambo jema. Na ni Sunna aliyejichinjia mnyama wa Aqiqa, awe miongoni mwa wataokula nyama hiyo, pamoja na watu wake wa nyumbani, na kuwatunukia majirani na kuwagawia mafakiri na masikini. Na wala hakuna junaha kuigwa nyama yote kwa mafakiri, au baadhi yake tu. Hali kadhalika, hakuna junaha iwapo utakula wewe mwenyewe, na watu wa nyumbani kwako tu. Lakini utaratibuu bora ni kuwagawia watu wengine, na wewe mwenywe kula kutokana na nyma hiyo hiyo.
    Na anayetakiwa kuchinja mnyama wa Aqiqa kwa mtoto au watoto wake, ni Baba mtu; ila hakuna junaha kwa Mama mzazi kufanya Ibada hiyo, anapokosekana Baba mzazi, au anapokuwa Baba mzazi hana uwezo wa mali. Mtume ﷺ amewausia wafuasi wa Umma wake wachinje wanyama wa Aqiqa, kama inavyosema Hadithi ya Amr bin Shu’ayb:

    عن عمرو بن شعيب، عن أبيه، عن جدِّه، أنَّ النَّبي -صلى الله عليه وسلم- قال: “من أحبَّ منكم أنْ ينسك عن ولده، فليفعل: عن الغلام شاتان، وعن الجارية شاة”. أخرجه مالك، وأحمد، وأبو داود، والنسائي
    Imepokwa kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa Baba yake kutoka kwa Baru yake, akisema: “Amesema Mtume ﷺ: “Atayapenda miongoni mwenu kumchinijia mtoto wake mnyama wa Aqiqa, afanye hivyo: Mvulana amchinjie mbuzi wawili, na msichana amchinjie mbuzi mmoja.” Ameipoke Malik, Ahmad, Abu Daud na Nasai.
    Ns haitakikani kufanya ada yoyote ya Kijahiliyya, kama kumpaka mtoto, kipajani kwake, damu ya mnyama waliyechinjiwa; Mtume ﷺ hakufanya mila hizo, bali alifanya kinyume na mila hizo potofu. Hadithi ya Aisha ifuatayo inafafanua zaidi:
    عن عائشة رضي الله عنها:”أنَّه عقَّ عنهما يوم السَّابع وسمَّاهما، وأماط عنهما الأذى، وجعل بدله خلوقًا”، مخالفًا بذلك عادة الجاهلية الَّذين يضعون على رأس المولود قطنة فيها دم من دم العقيقة
    Imepokewa kutoka kwa Aisha akisema: “Mtume ﷺ aliwachinjia wanyama wa Aqiqa, wajukuu zake wawili, siku ya saba tangu kuzaliwa, akawapa majina, na kuwanyoa na kisha akawapaka kichwni uturu (mafuta mazuri), kinyume na mila na ada za Kijahiliyya, ambapo walikuwa wakichovya kipande cha pamba, damu ya mnyama wa Aqiqa, na kumpaka damu hiyo mtoto kichwani mwake.”

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Kuchinja mbuzi wa Aqiqa ni miongoni mwa Ibada za kuchinja wanyama kwa lengo la kujisogeza mbele zaidi na Mola wako, na kutoa sadaka kwa kushukuru neema ya kupewa mtoto halali katika ndoa.
    2. Aqiqa ni Sunna ya Mtume ﷺ tokea Sunna ya Kauli hadi ya Vitendo, na hivyo ni miongoni mwa ibada kubwa sana katika Uwislamu.
    3. Kiwango cha chini cha Aqiqa ni mbuzi au kondoo mmoja moja kwa mtoto wa kiume na mtoto wa kike.
    4. Kiwango cha juu ni kuchinja kondoo au mbuzi wawili kwa mtoto moja wa kiume na kondoo au mbuzi mmoja kwa mtoto wa kike.
    5. Sunna ya kumchinjia mtoto mchanga, siku ya saba, baada ya kuzaliwa, na kunyoa nywele alizozaliwa nazo kichwani, ili ziote nywele nyengine, mpya,
    6. Ni Sunna vile vile, baada ya kumchinjia mnyama wa Aqiqa, kumpa Jina na kumuombea dua yoyote nzuri.
    7. Wajibu wa kuepuka mila na ada za kishirikina katika uchinjaji wa mnyama wa Aqiqa.
    8. Aliyeosa kuchinjiwa mnyma wa Aqiqa anaweza kujichinia, mwenyewe, ukubwani.
    9. Nyama ya Aqiqa inapendekeza kugawiwa kwa Mafakiri na Masikini, Majirani, ndugu na Jamaa wa fuko la uzazi.
    10. Inajuzu, bali ni Sunna watu wa nyumbani kula nyama ya Aqiqa.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA USIMTUMIEA MTOA DARSA

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARIمختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*TAFSIRI YA UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME

    Leo Siku ya Jumatatu, tarehe 11, Shaaban 1446, H., sawa na tarehe 10 Februari, 2025.

    16- بَاب: التَّحْمِيدِ وَالتَّسْبِيحِ وَالتَّكْبِيرِ، قَبْلَ الْإِهْلَالِ، عِنْدَ الرُّكُوبِ عَلَى الدَّابَّةِ

    1. Mlango: Kuhusu Kupiga Alhamdulillah, Tasbihi na Takbiri kabla ya kuhiramia na pale mtu anapopanda mnyama wake

    785- عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ ﷺ وَنَحْنُ مَعَهُ بِالْمَدِينَةِ، الظُّهْرَ أربعًا، وَالْعَصْرَ بِذِي الْحُلَيْفَةِ رَكْعَتَيْنِ، ثُمَّ بَاتَ بِهَا حَتَّى أَصْبَحَ، ثُمَّ رَكِبَ حَتَّى اسْتَوَتْ بِهِ عَلَى الْبَيْدَاءِ، حَمِدَ اللَّهَ وَسَبَّحَ وَكَبَّرَ، ثُمَّ أَهَلَّ بِحَجٍّ وَعُمْرَةٍ، وَأَهَلَّ النَّاسُ بِهِمَا، فَلَمَّا قَدِمْنَا، أَمَرَ النَّاسَ فَحَلُّوا، حَتَّى كَانَ يَوْمُ التَّرْوِيَةِ أَهَلُّوا بِالْحَجِّ. قَالَ: وَنَحَرَ النَّبِيُّ ﷺ بَدَنَاتٍ بِيَدِهِ قِيَامًا، وَذَبَحَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ بِالْمَدِينَةِ كَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ. [رواه البخاري: 1551].

    1. Imepokewa kutoka kwa Anas رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ alituswalisha sote ukiwa tupo Madina swala ya adhuhuri rakaa nne na laasiri akatuswalisha Dhul Hulayfa rakaa mbili kisha tukapiga kambi hapo hapo mpaka asubuhi tena, ilipoingia asubuhi akapanda mnyama wake alipokuwa amesimama sawasawa katika eneo la Bayda’a Mtume ﷺ alimshukuru Mwenyezi Mungu, akapiga Tasbihi, akapiga na takbiri kisha akapiga tahlili ya kuingia katika Hajji na Umra, na watu wakafanya hivyo hivyo, lakini tulipofika Makka aliwaamrisha watu wavue Ihram zao baada ya kufanya Umra na wasubiri mpaka siku ya tarehe nane kutoka Makka kwenda ‘Arafa ndiyo watie niya upya ya kufanya Hijja na anasema Anas: “Na Mtume ﷺ alichinja wanyama wa Udh-hiya wa Hijja kwa mkono wake, wanyama hao wote wakiwa wamesimama wima na Mtume ﷺ alichinja Madina aliporudi kondoo wawili wenye rangi nyeupe na nyeusi wakiwa na pembe.” [Bukhari: 1551]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *Mrumiahi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • DARSA YA BM.14.4\10 MLANGO WA AQIQA

    Hadithi ya Leo, Jumatatu, tarehe 11, Shaabani, 1446, sawa na tarehe 10, JANUARI, 2025

    KUHUSU KUCHINJA MNYAMA WA AQIQA

    SEHEMU YA KWANZA

    بَابُ اَلْعَقِيقَةِ
    10.Mlango kuhusu Mbuzi wa Aqiqa
    مقدمة
    UTANGULIZI

    Neno *عقيقة* maana yake, kwa upande wa Lugha, ni nywele anazo zaliwa nazo kichwani, mtoto mchanga.

    الأصل في العقيقة: الشعر الَّذي على رأس المولود، فسميت الذبيحة عند حلق ذلك الشعر: عقيقة، فاشتهر حتَّى صار من الأسماء العرفية، بحيث لا يفهم من العقيقة عند الإطلاق إلاَّ الذبيحة
    Kwa upande wa Sharia, hata hivyo, العقيقة linatumiwa kumaanisha mnyama anaye chinjwa wakati wa kumnyoa nyewele mtoto mchanga. Hivyo, neno hilo limekuwa likituia kumaanisha mnayama wa kuchinjwa, wakati wa kumnyoa nywele mtoto mchanga kwa mara ya kwanza, tokea kuzaliwa; aghalazu siku ya saba tangu kuzaliwa.

    والعقيقة مستحبَّة بالسنَّة المطهرة

    Na Asasi ya Aqiqa ni Sunna inayo pendekezwa sana katika Uwislamu, kwa kauli na vitendo; Mtume ﷺ ameyafanya yote hayo mawili na kufuatiwa na Maswahaba wake.

    والعَقيقةُ هي ما يُذْبَحُ مِن بهيمةِ الأنعامِ يَومَ السَّابِعِ مِن وِلادةِ المولودِ مِن ذكَرٍ أو أُنْثى؛ شُكرًا للهِ تعالى على هذه النِّعمةِ العَظيمَة، ولها حِكمٌ ومقاصدُ جَليلَة

    Hivyo, Aqiqa ni mnyama miongoni mwa mifugo, anaye chinjwa siku ya saba tokea kuzaliwa mtoto, awe mwanamume au mwanamke, kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuruzukiwa neema hiyo kubwa. Na Asasi hiyo ina hekima zake na Malengo makubwa, kama tutavyo kuja kufafanua. 
    
    Hadithi ya mwanzo, katika Mlamgo huu, kama tutavokuja kuona, Mtume ﷺ aliwachinjia wajukuu wake wawili, Al-Hasan na Al-Husayn, watoto wa Aliyya bin Abi Twalib na Fatma binti Muhammad, kila mmoja kondoo mmoja mmoja. 
    
    Wanazuoni wengi wamesema:

    وذبحها أفضل من الصدقة بثمنها؛ لأنَّها سنَّة، ونسيكة مشروعة بسبب تجدد نعمة الله تعالى على الوالدين؛ ففيها معنى القربان، والشكران، والصدقة، والفداء، وإطعام الطعام عند السرور، فإذا شرع عند النكاح، فلأن يشرع عند الغاية المطلوبة منه، وهو وجود النسل، فيكون أولى، ولمَّا كانت النعمة بالذكر على الوالد أتم، والسرور والفرحة به أكمل، كان الشكران عليه أكثر بذبح شاتين له بدل شاة واحدة عن الأنثى، فإنَّه كما كانت النعمة أتمَّ، كان شكرها أكثر

    Na kuchinja mnyama wa Aqiqa, ni bora kuliko kutoa sadaka ya thamani ya mnyama wa Aqiqa, kwa sababu kuchinja mnyama wa Aqiqa ni Sunna kubwa sana, iliyotendwa na Mtume ﷺ na  kufuatwa na Maswahaba wake, kwa sababu ya kuzidishiwa neema za Mwenyezi Mungu kwa wazee wawili. Hivyo, katika kuchinja mnyama wa Aqiqa kuna Ibada ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, kwa upande mmoja, na kwa kutoa Sadaka ya kujitolea, na kulisha chakula wakati wa furaha. Ndiyo maana mtu anapofunga ndoa tu, huwa na malengo maalumu moyoni mwake, miongoni mwake ni kupata kizazi kilicho bora. Na hivyo, mzee kushukuru kwa neema uliyopewa ya mtoto, ndio kukamilisha lengo hilo, na kufurahi kwa kupata kizazi kipya ndio ukamilifu wa shukrani,  kwa kuchinja wanyama wawili kwa mtoto wa kiume ataye kuja kuendeleza ukoo wa baba yake, na mnyama mmoja kwa mtoto wa kike, atayekuja kuendeleza kizazi cha upande wa mumewe, siku za usoni. 

    وقد ورَد في حَديثٍ آخَرَ، أنَّ النَّبيَّ صلَّى الله عليه وسلَّم عقَّ عَنهُما: “كَبشَينِ، كَبشَينِ”، أي: ذبَحَ عن كلِّ واحدٍ مِنهُما كبشَينِ؛ وقيل: تُرجَّحُ روايةُ الكَبشَينِ بأمرَينِ؛ أحَدُهما: تضَمُّنُها زِيادةَ ثِقَةٍ مقبولةً، والثَّاني: مُوافَقتُها للأحاديثِ الأخرى التي نصَّ النَّبيُّ صلَّى اللهُ تَعالى عليهِ وسلَّم فيها على شاتَينِ، حيثُ يقولُ: “عَن الغلامِ شاتَانِ مُكافِئَتانِ”، أو لعلَّه ذبَحَ في يومِ وِلادَتِهما كبشًا وفي السَّابعِ كبشًا عن كلِّ واحدٍ مِنهُما، أو ذبَح النَّبيُّ صلَّى اللهُ علَيْه وسلَّم كبشًا مِن مالِه. وأمَر علِيًّا بكَبشٍ آخَرَ، فنُسِب إلى النَّبيِّ صلَّى اللهُ علَيْه وسلَّم لأمرِه له بذَلك

    Hali kadhalika kumepokewa Hadithi nyengine ambayo inasema kuwa Mtume ﷺ aliwachinjiua wajukuu wake hao wawili wa kiume, kondoo wawili wwili kila mmoja, na wanazuoni wa Hadithi wamesema kuwa Riwaya ya kuchinwa kondoo wawili wawili kwa kila mjukuu mmoja, ina nguvu zaidi kutokana na sababu mbili. Kwanza, Riwaya hii ya pili ina nyongeza kutoka kwa msimulizi muaminifu. Na pili, ni kuwa Riwaya hii inaendana na Riwaya nyingi nyengine zisemazo: Mtume ﷺ aliwachinjia wavulana wawili, kila mmoja mbuzi wawili. Hivyo, ama ina maana kuwa Mtume ﷺ aliwachinjia mbuzi mmoja mmoja kila mmoja, siku ya kuzaliwa, na kisha baada ya kutimia siku saba toke kuzaliwa, akawachinjia tena mbuzi mmoja mmoja kila mmoja; jumla mbuzi wawili kwa kila mvulana mmoja. Au alichina kondoo kutoka na mali zake mwenywe, na baadae akamuamrisha Aliyy bin Abi Twalib, kama mzazi wa Al-Hasan na Al-Husyn, achinje kondoo wengine, na hivyo uchinjaji wote ukanasibishwa kwa Mtume ﷺ.

    وقيل: روايةُ “كبشًا كبشًا” للدَّلالةِ على مَشروعيَّةِ الاقْتِصارِ على ذَبْحِ كبشٍ واحدٍ عن الذَّكَرِ، وروايةُ “كَبشَين” للدَّلالةِ على أنَّ الأفضلَ والأتمَّ ذَبْحُ كبشَينِ؛ فإنَّ العدَدَ ليسَ شَرْطًا، بَلْ هو مُستَحَبّ

    Riwaya inayosema kuwa walichinjiwa kondoo mmoja mmoja kwa kila moto mmoja, ni dalili kuwa inajuzu kumchinjia mtoto mchanga mvulana, kondoo moja. Vile Riwaya inayozungumzia kuwa mtoto mchanga, mvulana, amechinjiwa kondoo wawili kila mvulana, ni dalili kuwa kwa mtoto wa kiume ni bora kumchinjia kondoo au mbuzi wawili, na mtoto wa kike, kumchinujia kondoo au mbulzi mmoja. Hivyo, idadi siyo sharti wla siyo wajibu, bali ni jambo linalopendekezwa tu.

    ومِنَ سُنَنِ العَقيقَةِ: التَّفرِقةُ بينَ الغُلامِ والجاريةِ، بحَيثُ يُعَقَّ عن الغُلامِ بشَاتَينِ، وعن الجاريةِ بشاةٍ واحدةٍ؛ لصِحَّةِ الأحاديثِ بذلك

    Hivyo, miongoni mwa Sunna za mnayma wa Aqiqa ni kiutofautisha baina ya mtoto wa kiume na mtoto wa kike; ambapo mtoto wa kiume achinjiwe mbuzi au kondoo wawili, vile mtoto wa kike achinjiwe mbuzi au kondoo mmoja, kwa sabu kuna Hadithi nyingi sahihi zenhe kusema hivyo.
    
    Baada ya Utangulizi huo, sasa tusome Hadithi alizotuwekea Imam Ibn Hajar katika Mlamgo huu wa Aqiqa.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    IMETAYARISHWA na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

    KUTOKA KITABU CHA بلوغ المرام من أدلة الأحكام UFIKIAJI WA MALENGO KUPITIA HADITHI ZA FIQHI YA MILANGO*

    JIUNGE NA KUMBI ZA DARSA ZA SAYYID ABDULQADIR SHAREEF, KWA KUTUMA MAOMBI YAKO, MOJA KWA MOJA, KWENDA NAMBA +255786887887, KUPITIA WHATSAP
    LAZIMA UTAJE MAJINA YAKO HALISI MATATU NA MAHALI ULIPO! SHARIA ZA MITANDAO TANZANIA

    UKIWA NA SUALA LOLOTE, LINALOKUHUSU WEWE MWENYEWE, NA SI KUMHUSU MTU MWENGINE, USIMTUMIE MWENYE KUTOA DARSA, BALI MTUMIE ADMIN WA UKUMBI WAKO, AKUPATIE JIBU, KAMA LIPO JIBU LAKE, KUTOKANA NA MAJIBU ZAIDI YA 3000, AU ALIWEKE SUALA LAKO KUMBINI, LISUBIRI KUJIBIWA! USIMTUMIEA MTOA DARSA.

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARIمختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*TAFSIRI YA UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME

    Leo Siku ya Jumapili, tarehe 10, Shaaban 1446, H., sawa na tarehe 09 Februari, 2025.

    15- بَاب: التَّلْبِيَةِ

    1. Mlango: Kuhusu At-Talbiya (yaani Labbayka Allahuma Labbayk)

    784- عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ تَلْبِيَةَ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ: «لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ». [رواه البخاري: 1549].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar رضي الله عنهما akisema: “Talbiya ya Mtume ﷺ ilikuwa kama ifuatavyo: “لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ.” [Labbayk ewe Mola wangu Labbayka, Labbayka Ewe Mola wangu hakuna mshirika kwako Wewe Labbayka, hakika sifa zote na neema zote ni Zako pamoja na ufalme, hakika huna mshiriki yeyote].” [Bukhari: 1549]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *Mrumiahi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIA ZA MTUME ﷺLeo Jumapili, tarehe 10 SHAABANI, 1446, H., sawa na tarehe 09, JANUARI, 2025.WASIA WA 55مئتا وصية من وصايا الرسول ﷺجمعها ورتبها ثم فسرها إلى السواحليةالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIA ZA MTUME *ﷺ.Zimekusanywa na Kufasiriwa kwa Kiswahili naSayyid Abdulqadir ShareefMTIMISHI WA HADITHI ZA MTUME

    الوصية الخامسة والخمسون
    سَلُوا اللَّه العافيةَ في الدُّنْيا والآخِرةِ
    55. Muombe Mwenyezi Mungu usalama na uzima Duniani na Akhera

    • وَعَن أَبي الفَضلِ العبَّاسِ بنِ عَبْدِ المُطَّلِبِ رضِي اللَّه عنْهُ ، قال: قُلْتُ يارسول اللَّهِ: عَلِّمْني شَيْئاً أَسْأَلُهُ اللَّه تَعَالى ، قَالَ: « سَلُوا اللَّه العافِيةَ ». فَمكَثْتُ أَيَّاماً، ثُمَّ جِئتُ فَقُلْتُ : يا رسولَ اللَّه : علِّمْني شَيْئاً أَسْأَلُهُ اللَّه تعالى ، قَالَ لي : « يَا عبَّاسُ يا عمَّ رَسولِ اللَّهِ ، سَلُوا اللَّه العافيةَ في الدُّنْيا والآخِرةِ » .رَواهُ الترمذيُّ وقَالَ : حديثٌ حسنٌ صَحيحٌ .* Imepokewa kutoka Kwa Abul-Fadhil al-‘Abbas bin ‘Abdulmutwalib رضي الله عنه akisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nifundishe kitu cha kumuomba Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالي! Akaniambia: “Muombe Mwenyezi Mungu usalama na uzima!” Nikakaa siku kadhaa, kisha nikamwendea tena Na kusema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Nifundishe kitu cha kumuomba Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالي!” Akaniambia: Ewe ‘Abbas! Ewe Baba mdogo wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Muombeni Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالي* * usalama Na uzima, duniani na Akhera!” Ameipokea Tirmidhi na kusema: Hadithun Hasanun Swahih

    KUTOKA NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIYA YA MTUME ﷺ
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO!
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu!
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *Mrumiahi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • KCWW 68\1 UMAKINI KATIKA KUMCHA MWENYEZI MUNGU

    Hadithi za Marudio, Jumapili, tarehe 10, Shaaban, 1446, sawa na 09 ‎Februari,, ‎‎2025.‎

    KUHUSU UMAKINI KATIKA KUMWOGOPA MWENYEZI MUNGU ‎

    SEHEMU YA KWANZA.‎

    ‎68- Mlango wa Umakini wa Kumcha Mwenyezi Mungu na kujiepusha na ‎venye wasiwasi na udhanifu.

    ‎68- * Mlango wa Umakini wa Kumcha Mungu ‎na kujiepusha na venye wasiwas*i

    Amesema Mwenyezi Mungu ‎سبحانه وتعالي ‏‎ :-‎

    ‎1.‎ Na mlidhani ni jambo dogo, kumbe, kwa Mwenyezi Mungu ni kubwa mno ‎‎(An-Nur: 15)‎
    ‎2.‎ Na hakika Mola wako Mlezi Yupo kwenye mavizio Anawavizia (Al-Fajr: ‎‎14)‎

    ‎593. Imepokewa kutoka kwa al-Nu’maan bin Bashiirرضي الله عنهما ‏‎ akisema: ‎Nimemsikia Mtume ‎ﷺ ‏‎ akisema: ‎

    ‎“Hakika halali iko wazi na haramu iko wazi. Na baina yake kuna mambo mengi ‎yenye kutia wasiwasi, ambayo watu wengi hawayajui. Hivyo, mwenye kujikinga na ‎venye kutia wasiwasi huwa ameitakasa Dini yake na heshima yake, na mwenye ‎kujiingiza katika vyenye kutia wasiwasi amejiingiza kwenye haramu; kama alivyo ‎mchungaji anayechunga mifugo yake kando kando ya ngome; anajiponza kwa ‎uwezekano wa mifugo yake kuingia kwenye ngome. ‎

    Jihadharini! Kila mfalme ana ngome yake, na ngome ya Mwenyezi Munguسبحانه ‏وتعالي ‏‎ na makatazo Yake. ‎

    Jihadharini! Ndani ya kila mwili mna donge la nyama, ambalo likitengemaa ‎unatengemaa mwili mzima, na likifisidika unafisidika mwili mzima; Zindukaneni; ‎Donge hilo ni moyo.” Muttafaq ‘ alayhi.‎

    ‎594. Imepokewa kutoka kwa Anas ‎رضي الله عنه‎ akisema: Aliona Mtume ‎ﷺ‎ ‎kokwa ya tende barabarani, akasema: “Lau kama sichelei kuwa huenda ikawa ‎imetokana na tende ya sadaka, ningeila” Muttafaq ‘ alayhi. ‎

    ‎595. Imepokewa kutoka kwa al-Nawaas bin Sam’aan ‎رضي الله عنه‎ akisema: ‎Amesema Mtume ‎‏ ﷺ‎: “Wema ni kuwa na tabia nzuri, na dhambi ni kile ‎kinachokutia wasiwasi moyoni mwako, na ukachelea watu kukijua.” Ameipokea ‎Muslim. ‎

    UFAFANUZI

    Kumcha Mwenyezi Mungu maana yake kumtii kikamilifu, kadiri ya uwezo wako, ‎kwa kutenda aliyokuamrisha uyatende, au kukupa ruhusa uyatendo, na hayo ndiyo ‎mambo ya wajibu na halali, na kujiepusha kutenda aliyokukataza kuyatenda, na ‎hayo ndiyo mambo ya haramu; marufuku kuyatenda. Hivyo basi mambo ya halali ‎ni yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu, pekee. Na mambo ya haramu ni yale ‎aliyoharamisha Mwenyezi Mungu pekee. Ndiyo maana kwamba, halali iko wazi na ‎haramu iko wazi. Ila kuna mambo, vile vile, ambayo hayako wazi wazi uhalali ‎wake au uharamu wake, ambayo Mwenyezi Mungu ameyanyamazia, si kwa ‎kusahau, la; bali iwe rehema kwa waja Wake. Hivyo, ni muhimu sana kwa kila mja ‎kutoanza kuyapekua pekua au kuyadadisi dadisi, au kuyavamia kiusouso tu. Ni ‎wajibu kwake ayapime na kuyazingatia kwa makini, moyoni mwake. Haya ni ‎mambo ambayo yanaitwa SHUBHA: yaani hayako wazi! Yanaweza kuwa na sifa za ‎uhalali na wakati huo huo kuweza kuwa na sifa za uharamu. Ikifikia hali kama ‎hiyo, ni bora kuyaacha kuyatenda kuliko kuyatenda. Mwenye kujiepusha nayo hana ‎akosalo, zaidi ya kuitakasa Imani yake, na kuichunga dini yake na heshima yake. ‎Na mwenye kujitumbukiza kuyatenda, kuna uwezekano wa kuishia kutenda yaliyo ‎katazwa. Kwani mwenye kusogelea jambo, tu, akiamini kuwa ni haramu, basi ‎mwishowe anaweza kutumbukia kulitenda, na hapo atabebeshwa jukumu la ‎kitendo chake hicho. ‎

    Na Mtume ‎ﷺ‎ amebainisha wazi, shubha ni nini na vipi kuiepuka, aliposema: Wema ‎ni tabia njema\jambo jema, na dhambi ni jambo linalokutia wasi wasi na wayowayo ‎moyoni mwake, kiasi kwamba uchukie kuonekana unalitenda. Na muamuzi ni ‎wewe mwenyewe, kupitia moyo wako; kwani moyo ukitengemaa basi kila kitu ‎chengine kitatengemaa na moyo wako ukipotoka basi kila kitu chako kitapotoka ‎vile vile. ‎

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    ‎1.‎ Wajibu wa kutenda yaliyo halali na kujiepusha na yaliyo haramu.‎
    ‎2.‎ Halali ni alicho halalisha Mwenyezi Mungu, pekee, na Haramu ni alicho ‎haramisha au kukataza Mwenyezi Mungu, pekee.‎
    ‎3.‎ Uchamungu wa kweli ni kujiepusha na shubha, pasi na kuvuka mipaka ‎‎[usiharamishe kutoka nje, kwa mfano, eti unaweza kuona haramu!].‎
    ‎4.‎ Kila jambo jema lina thawabu na kila jambo ovu lina dhambi.‎
    ‎5.‎ Wema ni tabia njema, machoni mwako na mchoni mwa watu.‎
    ‎6.‎ Ouvo ni kila usilopenda watu wakuone unalitenda.‎
    ‎7.‎ Kila mja ana kiungo cha kumuongoza katika halali au haramu: ni moyo.‎
    ‎8.‎ Shughulika na kuuchunga moyo wako, usishughulike na yaliyomo kwenye ‎nyoyo za wengine; si kazi yako.‎
    ‎9.‎ Kpuuza maovu madogo madogo, katika maisha au dini, kunaweza ‎kutumbukiza katika mambo makubwa makubwa ya haramu.‎
    ‎10.‎ Mwislamu mchamungu ni yule mwenye kushikanama na yaliyothibiti kwa ‎nass na dalili, na kujiepusha na maneno au maoni ya watu.‎
    ‎11.‎ Umakini wa Mtume ‎ﷺ‎ katika kumcha Mola wake, kuepuka kula kokwa ya ‎tende aliyo iokota njiani, kwa kushuku kuwa yawezekana imetokana na ‎sadaka, na Mtume ‎ﷺ‎ haruhusiwi kula sadaka.‎
    ‎12.‎ Kujuzu kuokota kitu njiani na kunufaika nacho iwapo ni cha thamani ndogo, ‎na ambacho, kwa kawaida, watu hukipuuza.‎
    ‎13.‎ Kujuzu kula kilicho dondoka chini, iwapo kinasafishika.‎
    ‎14.‎ Ukitilia shaka jambo usilitende, na ukiwa na uhakika na jambo litende!‎
    ‎15.‎ Uwislamu ni tabia na mwenendo mwema.‎
    ‎16.‎ Dalili za dhambi ni mbili: Wasiwasi na waupwaup moyoni kuutenda, na ‎Kutopenda watu wakuone unautenda, au wajuwe unautenda.‎
    ‎17.‎ Kila nafsi imeumbwa na hisia za kujua jema na baya.‎
    ‎18.‎ Hakuna kupatilizwa kwa hisia za moyoni tu, ilimradi hisio hizo ‎hazitekelezwei kwa kitendo chenyewe, kiovu.‎
    ‎19.‎ Makatazo ya Mwenyezi Mungu ndio ngome Yake, usiyasogelee!‎

    INAENDELEA… ‎

    والله أعلم
    ‏ ‏
    وبالله التوفيق‎ ‎

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم.‏

    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    Kutoka Kitabu cha: Kitalu cha Waja Wema: Maneno ya Muokozi ‎wa ‎Umma, ‎ambacho ni tafsiri kamili ya ‎رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين للإ ‏مام ‏النووي ‏‎ ‎kilicho tungwa na Imam An-Nawawi na kufasiriwa kwa ‎Kiswahili na ‎Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aal Shaykh Abi Bakr bin Salim ‎آل الشيخ ابى بكر بن سالم‎.‎

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza, na ‎kuweka ‎kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye Makundi ya ‎Mitandao ya ‎Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na kuelimisha ‎Dini. Changia ‎kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARIمختصر صحيح البخاري للزبيديرتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقاتالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*TAFSIRI YA UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *Sayyid Abdulqadir ShareefMTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME

    Leo Siku ya Jumamosi, tarehe 09, Shaaban 1446, H., sawa na tarehe 08 Februari, 2025.

    14- بَاب: مَا يَلْبَسُ الْمُحْرِمُ مِنْ الثِّيَابِ وَالْأَرْدِيَةِ وَالْأُزُرِ

    1. Mlango: Mavazi gani anavaa mwenye kuhiramia na mitandio au shuka za aina gani

    783- وَعَنْهُ رضي الله عنه قَالَ: انْطَلَقَ النَّبِيُّ ﷺ مِنْ الْمَدِينَةِ، بَعْدَمَا تَرَجَّلَ وَادَّهَنَ، وَلَبِسَ إِزَارَهُ وَرِدَاءَهُ، هُوَ وَأَصْحَابُهُ، فَلَمْ يَنْهَ عَنْ شَيْءٍ مِنْ الْأَرْدِيَةِ وَالْأُزُرِ تُلْبَسُ، إِلَّا الْمُزَعْفَرَةَ الَّتِي تَرْدَعُ( ) عَلَى الْجِلْدِ، فَأَصْبَحَ بِذِي الْحُلَيْفَةِ، رَكِبَ رَاحِلَتَهُ، حَتَّى اسْتَوَى عَلَى الْبَيْدَاءِ( ) أَهَلَّ هُوَ وَأَصْحَابُهُ، وَقَلَّدَ بَدَنَتَهُ، وَذَلِكَ لِخَمْسٍ بَقِينَ مِنْ ذِي الْقَعْدَةِ، فَقَدِمَ مَكَّةَ لِأَرْبَعِ لَيَالٍ خَلَوْنَ مِنْ ذِي الْحَجَّةِ، فَطَافَ بِالْبَيْتِ وَسَعَى بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، وَلَمْ يَحِلَّ مِنْ أَجْلِ بُدْنِهِ؛ لِأَنَّهُ قَلَّدَهَا، ثُمَّ نَزَلَ بِأَعْلَى مَكَّةَ عِنْدَ الْحَجُونِ( ) وَهُوَ مُهِلٌّ بِالْحَجِّ، وَلَمْ يَقْرَبْ الْكَعْبَةَ بَعْدَ طَوَافِهِ بِهَا حَتَّى رَجَعَ مِنْ عَرَفَةَ، وَأَمَرَ أَصْحَابَهُ أَنْ يَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ وَبَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، ثُمَّ يُقَصِّرُوا مِنْ رُءُوسِهِمْ، ثُمَّ يَحِلُّوا، وَذَلِكَ لِمَنْ لَمْ يَكُنْ مَعَهُ بَدَنَةٌ قَلَّدَهَا، وَمَنْ كَانَتْ مَعَهُ امْرَأَتُهُ فَهِيَ لَهُ حَلَالٌ، وَالطِّيبُ وَالثِّيَابُ. [رواه البخاري: 1545].

    1. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas رضي الله عنهما akisema: “Mtume ﷺ alitoka Madina baada ya kutia mafuta na kuchana nywele zake, akavaa shuka yake pamoja na shuka ya kujitanda juu, yeye na maswahaba wake na hakumkataza mtu yeyote kujitanda shali lolote au kuvaa shuka ya aina yoyote isipokuwa shuka iliyotiwa rangi ya Zaafarani ambayo kwa kawaida yake zafarani iliyotiwa katika nguo ile anapoivaa mtu, rangi huingia katika ngozu ya mwili wake kwa hivyo ilipoingia asubuhi Mtume ﷺ alifika Dhul Hulayfa, akampanda mnyama wake, yule mnyama alipokaa sawasawa katika eneo la Bayda’a akapiga Tahlil yeye na maswahaba wake ya kuingia katika Hijja, na akawavisha kamba mahasusi ngamia wake aliowaswaga kwa ajili ya Hijja, na tarehe hiyo ilikuwa tarehe tano Dhul Qa’ada, tukaingia Makka baada ya siku kumi na nne ambazo zimabakia kwa kuingia mfungo tatu, akatufu Al Ka’aba, akaenda Swafa na Marwa lakini hajavua ihram yake kwa sababu aliswaga wanyama wake wa Udh-Hiya na alikuwa wanyama hao ameshawatia alama kwamba ni wanyama wa Udh-hiya, kwa hivyo akawa ana Ihram zake zilezile amevaa na akateremka sehemu za juu Makka inaitwa Al Hajuun akiwa yumo katika amali ya Hija na wakati wote huo hakuisogelea Al ka’ba, baada ya kutufu mara ya kwanza mpaka aliporudi kuyoka ‘Arafa lakini aliwaamrisha maswahaba wake waende wakatufu Al Ka’aba, waende Swafa na Marwa kisha wakate au kunyoa nywele zao kisha awavue Ihram. Na amri hii ilikuwa kwa mtu yeyote ambaye amekuja Makka pasi na kuswaga mnyama wake wala Udh-hiya wala kumtia alama mnyama wake na hivyo akaamrisha mtu yeyote ana mwanandoa wake mkewe basi ni halali kwake sasa akishamaliza kutufu na kufanya Swafa na Marwa kwa ajili ya Umra na inamjuzia kupaka mafuta na kuvaa nguo za kawaida.” [Bukhari: 1545]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY
    *HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ *
    *JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO! *
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu! ‎
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *Mrumiahi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.
    kcwajawema@gmail.com

  • KCWW 67 UHARAMU WA KUTAMANI KUFA

    Hadithi za Marudio, Jumamosi, tarehe 09 Shaaban, 1446, sawa na 08 Februari, ‎‎2025.‎

    KUHUSU UBAYA WA KUTAMANI MAUTI

    ‎67- Mlango wa ubaya ya kutamani mauti kutokana na janga liliomfika mja ‎isipokuwa atapochelea kufitinishwa katika Dini yake.‎

    ‎590. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayraرضي الله عنه ‏‎ akisema: Amesema ‎Mtume‏ ﷺ ‏‎: “Asitamani mmoja wenu kufa; kwani kama ni mja mwema basi ana ‎fursa ya kuzidisha wema wake, na kama ni mja muovu basi ana fursa ya kujirudi ‎na kutubu.” Muttafaq ‘alaylhi. ‎

    Riwaya nyengine ya Muslim inasema: “Asitamani mmoja wenu kufa, wala ‎kuomba afe kabla ya kujiwa na ajali yake; kwani anapokufa mtu basi na kuweza ‎kunufaika na amali zake nako pia kunakatika (kunasita); na kwa mtu mwenye ‎kuamini, umri wake humzidishia kheri.”‎

    ‎591. Imepokewa kutoka kwa Anas ‎رضي الله عنه ‏‎ akisema: Amesema ‎Mtume ‎‏ ﷺ‎: “Asitamani mmoja wenu kufa kwa sababu ya kufikwa na tatizo la ‎kidunia, na kama hana budi, basi na aseme kuomba: “Ewe Mola wangu! Niache ‎niishi, iwapo kuishi ni kheri kwangu. Na nifishe, iwapo mauti ni kheri kwangu.” ‎Muttafaq ‘alayhi. ‎

    ‎592. Imepokewa kutoka kwa Qays bin Abi Haazim akisema: ‎Tulimtembelea Khabbaab bin al-Aratt‏ رضي الله عنه ‏nyumbani kwake, alipokuwa ‎mgonjwa, na tukamkuta ametibiwa kwa kupigwa msumari wa moto mwahali ‎saba, mwilini. Akasema: “Ndugu zetu waliotutangulia wamekwenda mbele ya ‎Haki bila ya kupoteza chochote katika dunia hii. Sisi, hii leo, tunamiliki vitu ‎ambavyo hatuna usalama navyo, iwipokuwa kuvizika ardhini. Na lau kama ‎sikumsikia Mtume ‎ﷺ ‏‎ anatukataza kuomba kufa, basi ningeliomba nife.” ‎Baadaye tukamtembelea tena na kumkuta anakarabati ukuta wake. Akasema: ‎‎“Mwislamu anapata thawabu kwa kila kitu anachotoa, isipokuwa kwa kile ‎anachokisitiri chini ya ardhi.” Muttafaq ‘alayhi.‎

    UFAFANUZI ‎

    Mlango huu unazungumzia uharamu wa kutamani kufa kwa sababu tu ya shida ‎na matatizo ya kimaisha. Kwani kutamani kufa ni sawa na kujijasirisha na ‎Mwenyezi Mungu, ha kutoridhika na alichokuamulia Mola wako; ni sawa na ‎kusema na liwe liwalo lakini sitaki kuishi tena! Ni kujiponza na Mwenyezi ‎Mungu. Hivyo, kama umefikwa na shida kubwa, na kuhemewa usijue la ‎kufanya, basi muombe Mola wako akuondoshee au kukupunguzia shida hiyo, ‎na kama ni lazima basi omba kwa kusema: “Ewe Mola wangu! Niache niishi, ‎iwapo kuishi ni kheri kwangu. Na nifishe, iwapo mauti ni kheri kwangu.” Lakini ‎usijiponze na Mwenyezi Mungu; kwani kujiponza Naye ni kuonesha ‎kutumuogopa! Ni kinyume, kabisa, na uchamungu. Zaidi, ni kwamba uhai ‎unakupa fursa siyo tu ya kutubu na kurudi kwa Mola wako, bali pia kuongeza ‎amali njema na hivyo kuzidisha thawabu zako. Na kifo ni kukatisha fursa za ‎kutubu au kutenda mema; utaenda na ulichokichuma tu, pamoja na dhambi za ‎kujijasirisha na Mwenyezi Mungu. ‎

    Hata hivyo, inajuzu kuchagua au kutamani kifo unapochelea kufitinishwa katika ‎Dini yako, kwamba ukiendelea kuishi basi utakufurishwa. Hapo unaweza ‎kumuomba Mola wako aichukue roho yako –kama alivyo usia Mtume ‎ﷺ‎ jinsi ya ‎kuomba- , ili uondokane na janga la kukufurishwa. Ni kumuomba Mola wako ‎akufishe, si kujiua! Na Mwenyezi Mungu ana hiari Yake, kuitikia ombi lako, au ‎kukuondolewa mtihani uliokukabili.‎

    YALIYOMO YA YATOKANAYO

    ‎1.‎ Haramu kutamani kufa, kabla ya wakati wako, kwa sababu ya shida au ‎misukosuko ya kidunia, kama maradhi na umasikini.‎
    ‎2.‎ Kutamani kufa ni kujijasirisha na Mwenyezi Mungu; dhambi!‎
    ‎3.‎ Hakuna shida inayodumu, wala raha isiyoisha; ni mitihani ya muda tu.‎
    ‎4.‎ Dawa ya mitihani yote duniani ni uvumilivu na dua kwa Mola wako.‎
    ‎5.‎ Fursa za kuchuma mema zimo katika uhai, na ukosefu wa fursa upo ‎kwenye mauti.‎
    ‎6.‎ Mbora wa bahati ni yule ambaye amejaaliwa kuishi maisha marefu na ‎akatenda yaliyo mema: ‎خير الناس من طال عمره وحسن عمله (رواه الترمذي)‏‎ .‎
    ‎7.‎ Kujijasirisha na Mwenyezi Mungu ni kutoridhika na maamuzi Yake.‎
    ‎8.‎ Sunna, kwa mwenye kukata tamaa na maisha, aombe dua ‎aliyofundishwa na Mtume ‎ﷺ‎ hapo juu.‎
    ‎9.‎ Fadhila za Sayyidina Khabbab bin Al-Aratt ‎رضي الله عنه‎ ambaye pamoja ‎na kushikwa na maradhi makali hakutamani kufa kwa sababu ‎wamekatazwa na Mtume ‎ﷺ‎ kuomba kufa.‎
    ‎10.‎ Kutokata tamaa kwa Sayyidina Khabbab na Mola wake, kumempa faraja.‎
    ‎11.‎ Mwislamu analipwa wema kwa kila jema alifanyalo, hata jambo la ‎manufaa yake mwenyewe.‎

    والله أعلم
    ‏ ‏
    وبالله التوفيق‎ ‎

    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم.‏

    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef

    Kutoka Kitabu cha: Kitalu cha Waja Wema: Maneno ya Muokozi ‎wa ‎Umma, ‎ambacho ni tafsiri kamili ya ‎رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين للإ ‏مام ‏النووي ‏‎ ‎kilicho tungwa na Imam An-Nawawi na kufasiriwa kwa ‎Kiswahili na ‎Sayyid ‎Abdulqadir Shareef Aal Shaykh Abi Bakr bin Salim ‎آل الشيخ ابى بكر بن سالم‎.‎

    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako au kwenye ‎WhatsApp na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu.‎

    kcwajawema@gmail.com

  • NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIA ZA MTUME ﷺLeo Jumamosi, tarehe 09 SHAABANI, 1446, H., sawa na tarehe 08, JANUARY, 2025WASIA WA 53مئتا وصية من وصايا الرسول ﷺجمعها ورتبها ثم فسرها إلى السواحليةالسيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسينيخادم السنة النبوية*NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIA ZA MTUME *ﷺ.Zimekusanywa na Kufasiriwa kwa Kiswahili naSayyid Abdulqadir ShareefMTIMISHI WA HADITHI ZA MTUME

    الوصية الثالثة والخمسون
    هجر المعاصي والتمسك بطاعة الله وذكره
    53: Kuhama maaswi na kushikamana na utiifu wa Mwenyezi Mungu na kumkumbuka

    وَعَنْ أُمِّ أَنُسِ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا أَنَّهَا قَالَتْ : يا رَسُولَ اللهِ أَوْصِنِي ، قَالَ :« اُهْجُرِي الْمَعَاصِي فَإِنَّهَا أفْضَلُ الْهِجْرَةِ ، وَحافِظِي عَلَى الْفَرَائِضِ ، فَإِنَّه أفْضَلُ الْجِهَادِ ، وَأَكْثِرِي مِنْ ذِكْرِ ِاللهِ ، فَإِنَّكِ لَا تَأْتِينَ لله بِشَيْءِ أَحَبُّ إِلَيه مِنْ كَثْرَةِ ذِكْرِهِ ».[ رَوَاهُ الطَّبَرانِيُّ بِإِسْنادِ جَيِّدٍ ]

    Imepokewa kutoka kwa Ummu Anas رضي الله عنها akisema: “Nilisema kumwambia Mtume ﷺ: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Niusie.” Mtume ﷺ akamwambia: “Yahame maaswi, kwani ndiyo Hijra iliyo bora sana. Na jichunge kutekeleza Swala za faradhi, kwani ndiyo Jihadi iliyo bora sana (Kwa mwanamke). Na kithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu, kwani hutaweza hata kidogo kwenda mbele ya Mwenyezi Mungu kwa jambo lolote Alipendalo zaidi ya kukithirisha kumtaja.” Ameipokea Tabarani kwa Isnadi nzuri.

    وإتمامًا للفائدة نروي هذين الحديثين الواردين في فضل الذكر: الأول: عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله ﷺ: «يقول الله عز وجل: أنا عند ظن عبدي بي، وأنا معه حين يذكرني، فإن ذكرني في نفسه ذكرته في نفسي، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منه، وإن تقرب إلي شبرًا تقربت إليه ذراعًا، وإن تقرب إلي ذراعًا تقربت إليه باعًا، وإن أتاني يمشي أتيته هرولة».[رواه البخاري ومسلم والترمذي]

    Riwaya nyingine kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume ﷺ: “Mwenyezi Mungu Anasema: “Mimi nipo na Mja Wangu kadiri anavyonidhania Mimi. Na Mimi Ninakuwa naye pale anaponikumbuka, akinitaja kisirisiri ndani ya nafsi yake basi Nitamtaja Mimi ndani ya Nafsi Yangu. Na akinitaja mbele ya watu Nitamtaja mbele za watu bora kuliko hao wake yeye. Akijisogeza Kwangu Mimi kwa shubiri moja, Nitajisogeza kwake kwa dhiraa moja. Akijisogeza Kwangu kwa dhiraa moja, Nitajisogeza kwake kwa pima. Akinijia anatembea, Nitamwendea Ninakimbia kwa kasi.” Ameipokea Bukhari na Muslim.

    عن معاوية رضي الله عنه أن رسول الله ﷺ خرج على حلقة من أصحابه، فقال: «ما أجلسكم؟» قالوا: جلسنا نذكر الله ونحمده على ما هدانا للإسلام، ومن به علينا، قال «آلله ما أجلسكم إلا ذلك؟» قالوا: والله ما أجلسنا إلا ذاك، قال «أما إني لم أستحلفكم تهمةً لكم، ولكنه أتاني جبريل فأخبرني أن الله عز وجل يباهي بكم الملائكة». [رواه الثلاثة ومسلم والترمذي]

    Riwaya nyingine kutoka kwa Muawiya رضي الله عنه akisema: “Mtume ﷺ alitoka akakuta watu wamekaa mduara akawauliza: “Nini kimekufanyeni mkae hivi?” Wakajibu: “Tumekaa tunamtaja Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa kutuongoza katika Uislamu, na kwa Neema Zake Alizotuteremshia.” Mtume ﷺ akauliza: “Ni kweli? Hayo tu ndiyo yamekufanyeni mkae hivyo?” Wakajibu: “Naam, hakuna chochote kingine.” Mtume ﷺ akasema: “Mimi sijakulisheni kiapo na kukutuhumuni kuwa hamfanyi ila nakutuhumuni kuwa hakuna lililokuwekeni hapo jingine. Na amenijia Jibril na kuniambia kwamba Mwenyezi Mungu Anajivunia nyinyi mbele ya Malaika Wake.” Wameipokea Maimamu watatu, Muslim na Tirmidhi.

    KUTOKA NYASIA 200 MIONGONI MWA NYASIYA YA MTUME ﷺ
    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO
    JIUNGE NA DARSA HIZI KWA KUTUMA MAJINA YAKO HALISI MATATU, TAJA MAHALI ULIPO NA WEKA NAMBA YA SIMU ULIOSAJILIWA JINA LAKO
    TUMA MOJA KWA MOJA KWENDA +255786887887 –Kupitia Whatsap tu
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*
    *Mrumiahi wa Hadithi za Mtume ﷺ *
    NI RUHUSA KUNUKUU, kama ilivyo, pasi na kubadilisha au kuongeza chochote, ‎na ‎kuweka kwenye FB yako, ‎WhatsApp, na kwenye Makundi ‎ya ‎Mitandao ya Kijamii za Kiislamu, ‎kwa lengo la kusambaza na ‎kuelimisha ‎Dini. Changia kusambaza ‎Dini, ujipatie thawabu
    kcwajawema@gmail.com