Author: axb

  • TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*

    TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*

    مختصر صحيح البخاري للزبيدي
    رتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقات
    السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسيني
    خادم السنة النبوية
    *MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.
    *Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *
    Sayyid Abdulqadir Shareef
    MTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME
    *Leo Siku ya Jumatano, tarehe 30, Saffar, 1446, H., sawa na tarehe 04, Septemba, 2024. *
    (9)
    كِتَاب مَوَاقِيتِ الصَّلاَةِ
    KITABU CHA NYAKATI ZA SWALA

    363- وعَنْهَا رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: رَكْعَتَانِ، لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَدَعُهُمَا، سِرًّا وَلاَ عَلاَنِيَةً: رَكْعَتَانِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَرَكْعَتَانِ بَعْدَ الْعَصْرِ. [رواه البخاري: 592].

    1. Imepokewa kutoka kwa Aisha رضي الله عنها akisema: “Rakaa mbili Mtume ﷺ hakuwa anaziacha si kisiri siri wala waziwazi nazo ni rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri na rakaa mbili baada ya laasiri.” [Bukhari:592]

    UFAFANUZI

    Mtume ﷺ alikuwa anaswali rakaa mbili laasiri lakini hii ilikuwa khususwia yake, ndiyo maana alikuwa anaziswali peke yake nyumbani lakini zimekatwaza.

    25- بَاب: الأَذَانِ بَعْدَ ذَهَابِ الْوَقْتِ

    1. Mlango: Kuhusu kuadhini baada ya wakati wa swala husika kupita

    364- عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: سِرْنَا مَعَ النَّبِيِّ ﷺ لَيْلَةً، فَقَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ: لَوْ عَرَّسْتَ بِنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: «أَخَافُ أَنْ تَنَامُوا عَنْ الصَّلاَةِ». قَالَ بِلاَلٌ: أَنَا أُوقِظُكُمْ. فَاضْطَجَعُوا، وَأَسْنَدَ بِلاَلٌ ظَهْرَهُ إِلَى رَاحِلَتِهِ، فَغَلَبَتْهُ عَيْنَاهُ فَنَامَ، فَاسْتَيْقَظَ النَّبِيُّ ﷺ وَقَدْ طَلَعَ حَاجِبُ الشَّمْسِ، فَقَالَ: «يَا بِلاَلُ! أَيْنَ مَا قُلْتَ؟» قَالَ: مَا أُلْقِيَتْ عَلَيَّ نَوْمَةٌ مِثْلُهَا قَطُّ. قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ قَبَضَ أَرْوَاحَكُمْ حِينَ شَاءَ، وَرَدَّهَا عَلَيْكُمْ حِينَ شَاءَ، يَا بِلاَلُ، قُمْ فَأَذِّنْ بِالنَّاسِ بِالصَّلاَةِ» فَتَوَضَّأَ، فَلَمَّا ارْتَفَعَتْ الشَّمْسُ وَابْيَاضَّتْ،( ) قَامَ فَصَلَّى. [رواه البخاري: 595].

    1. Imepokewa kutoka kwa Abu Qataadah رضي الله عنه akisema: “Tulisafiri usiku mmoja na mtume ﷺ Tulivyofika njiani baadhi ya watu wakasema: “Lau tungesimama hapa njiani tukapiga kambi” Mtume ﷺ akawaambia: “Nachelea msije mkapitiwa na usingizi” Bilal alivyosikia maneno hayo akasema: “Mimi nit akuamsheni jionyoosheni tu” na Bilal akakaa na kuegemea masoji au mizingo ya mnyama wake lakini akapitiwa na usingizi. Mtu wa mwanzo kuzindukana alikuwa mtume ﷺ na wakati huo mwangaza wa jua ushachomoza, mtume ﷺ akasema: “Bilal yako wapi maneno yako uliyoyasema?” Bila akasema: “Sijapata kupitiwa na usingizi kama nilivyopitiwa jana usiku” Mtume ﷺ akasema: “Mwenyezi Mungu anazichukua roho zenu wkaati wowote anaotaka na anakurudishieni roho zenu wakati wowote anaotaka ewe Bilal, haya nasi simama uadhini” Bilal akaondoka akaenda akatawadha na jua lilikuwa limeshachomoza limeinuka juu kidogo ndiyo akaadhini na mtume ﷺ akasimama kuswali.” [Bukhari:595]

    26- بَاب: مَنْ صَلَّى بِالنَّاسِ جَمَاعَةً بَعْدَ ذَهَابِ الْوَقْتِ

    1. Mlango: Kuswalisha jamaa baada ya kupita wakati wa swala husika

    365- عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رضي الله عنه جَاءَ يَوْمَ الْخَنْدَقِ بَعْدَ مَا غَرَبَتْ الشَّمْسُ، فَجَعَلَ يَسُبُّ كُفَّارَ قُرَيْشٍ، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! مَا كِدْتُ أُصَلِّي الْعَصْرَ حَتَّى كَادَتْ الشَّمْسُ تَغْرُبُ، قَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «وَاللَّهِ مَا صَلَّيْتُهَا» فَقُمْنَا إِلَى بُطْحَانَ فَتَوَضَّأَ لِلصَّلاَةِ، وَتَوَضَّأْنَا لَهَا، فَصَلَّى الْعَصْرَ بَعْدَ مَا غَرَبَتْ الشَّمْسُ، ثُمَّ صَلَّى بَعْدَهَا الْمَغْرِبَ. [رواه البخاري: 596].

    1. Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdullah رضي الله عنهما akisema: “Umar bin Khattwab رضي الله عنه alifika kwenye vita vya Khandaq baada ya jua kuchwa, akawa anawashambulia na kuwatukana makafiri wa Kiqureshi akisema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu sijapata wasaa wa kuswali laasiri mpaka jua limekuchwa” Mtume ﷺ akasema: “Hata mimi sijaiswali” kwa hiyo wote tukasimama kwenda katika bonde la maji Mtume ﷺ akatawadha na sisi pia tukatawadha akatuswalisha swala ya laasiri baada ya kuwa jua limeshakuchwa kisha akaswali magharibi baada yake.” [Bukhari:596]

    KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية
    Imetayarishwa na Sayyid Abdulqadir Shareef*

  • Je, majini wataingia peponi?

    Je, majini wataingia peponi?

    Nimeulizwa NANUKUU:-

    Al Habib Assalamu alaykum Mimi Nina swali dogo shareef Allah katuumba sisi na majini ili tumuabudu na akatuahidi sisi wanaadamu malipo ya pepo siku ya kiyama lakini pia Allah s,w kasema atawajaza motoni majini na watu lakini kuhusu peponi haijaelezwa je majini tutaingia nao peponi pamoja?

    JIBU

    BISMILLAH

    Kwa ufupi, kote kuwili kutajazwa wastahikifu wake tu, kutoka katika viumbve hivyo viwili; majini na wanaadamu. Acha nifafanue: Neno HAQQ maana yake USTAHIKIFU, au kwa maneno mengine, USTAHIKI, USTAHILI, USTAHILIVU na kadhalika. Kwa mfano, mtu akifanya jambo baya, akapatwa na madhara, huambiwa Astahili yako! Na mtu akifanya jambo jema akatunzwa huambiwa: Hongera unastahiki zawadi.

    Hibyo, pale watu wa Peponi watapomaliza kungia Peponi, na watu wa Motoni wakamaliza kuingia Motoni, basi majaaliwa hayo ndiyo USTAHILIVU wa kila kundi la viumbe vya Mwenyezi Mungu kutokana na AMALI ZAO walizozintanguliza kabla ya kufa na kuhesabiwa. Huko ndii kukamilisha USTAHILIVU wa kila mmoja, Wema kwa Wema na Uovu kwa Uovu. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema kwenye Kitabu Chake:

    وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ. إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ

    Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana, Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja.

    قال الشوكاني في تفسير هذه الآية: وإنما قضى عليهم بهذا لأنه سبحانه قد علم أنهم من أهل الشقاوة، وأنهم ممن يختار الضلالة على الهدى. اهـ.

    Mwenyezi Mungu amepitisha uamuzi Wake wa kuwahukumu watu hawa, kwa sababu AMEJUA kuwa ni miongoni mwa waja Wake waliojichagulia wenyewe UPOTOVU kwa vitendo vyao, wataishia wapi, baada ya kujichagulia Uongofu.

    Na kwa maana hiyo, mwenye kutenda mema atalipwa mema, na mwenye kutenda maovu atalipwa uovu. Na Mwenyezi Mungu ametubainishia wazi wazi kuwa Hakuna Usawa wa malipo, baina ya makundi mawili yenye kutofautiana: kundi la Mafasiki V Muumini. Hakuna malipo sawa kwa makundi hayo mawili tofauti. Amesema katika Sura mbali mbali, nani ya Qur’ani, kama ifuatavyo:

    وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ

    Na Mola wako, lau angelitaka, angeli wafanya watu wote wakawa umma mmoja; lakii hawaachi kutofautiana na kuhitalafiana. I_sipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja. (Huud, 11:118-9)

    Na Amesema:

    أَفَمَنْ كَانَ مُؤْمِنًا كَمَنْ كَانَ فَاسِقًا ۚ لَا يَسْتَوُونَ! أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ؟

    Je. aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa! Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu? (Swaad 38:28)

    أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ؟ مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ؟

    Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? Mna nini? Mnahukumu vipi? (Al-Qalam, 68:35-36)

    وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَلَا الْمُسِيءُ ۚ قَلِيلًا مَا تَتَذَكَّرُونَ

    Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na walio amini na watendao mema hawalingani na muovu. Ni machache mnayo yakumbuka. (Ghafir, 48:58)

    Katika Aya zote hizo, Mwenyezi Mungu ametubainishia wazi wazi, kuwa viumbe Vyake vimegawika katika makundi mawili makuu, Kundi la Wapotofu ambao majaaliwa yao ni kuishia kuingizwa Motoni, na Kundi la Watiifu, ambao majaaliwa yao ni kuishia kuingizwa Peponi. Ndiyo maana Akasema kuwaambia watu wa kila kundi husika: ndani ya Aya hiyo hiyo

    فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ ۖ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ

    Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. (As-Sajdah, 32: 14)

    فعلم من هذا أن امتلاء جهنم بهؤلاء لاستحقاقهم العذاب؛ وإلا فإن الله تعالى غني عن أن يعذب عباده، فقد صرح سبحانه أنه لا ينفعه ذلك، ولا يريده شرعا لكن الناس أنفسهم يظلمون؛ كما قال تعالى: ما يفعل الله بعذابكم إن شكرتم وآمنتم {النساء: 147}.

    Ndiyo maana ikatangazwa na kujulikana kuwa Kujazwa kwa Moto kwa watu waovu ni kutokana na USTAHIKIFU wao wa kuwepo huko; pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu hana haja ya kuwaadhibu Waja Wake, wala hapati manufaa yoyote kwa kuwaadhibu; bali wao wenyewe ndio waliotenda uovu, wakastahiki kuingizwa Wote Motoni kutokana na vitendo vyao wenyewe viovu. Mwenyezi Mungu hana haja ya kuwaadhibu waje Wake, kama alivyofafanua hivyo Mwenyewe, ila ni Viumbe Vyake venyewe, ndivyo vinavyo jiamulia waende wapi kutokana na dhuluma zao. Ndio maana Mwenyezi Mungu Akasema: Hafanyi kitu Mola wenu kwa kukuadhibisheni; ila mkinishuruku nitakuzidishieni malipo mema, na mkinikufuru basi juweni kuwa Adhabu Zangu ni kali mno (An-Nisaa,4:147) na Akasema:

    وقال: إن تكفروا فإن الله غني عنكم ولا يرضى لعباده الكفر وإن تشكروا يرضه لكم ولا تزر وازرة وزر أخرى ثم إلى ربكم مرجعكم فينبئكم بما كنتم تعملون إنه عليم بذات الصدور {الزمر: 7}.

    Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani._ (Az-Zumar, 39:7)

    Na Mwenyezi Mungu amekariri USTAHIKIFU huo wa kila kundi mahali mbali mbali ndani ya Kitabu Chake Kitukufu. Tunukuu Aua chache kuhusu Maudhui hiyo:

    كقوله عز وجل: لقد حق القول على أكثرهم فهم لا يؤمنون {يس: 7}.

    Bila ya Shaka, Kauli (ya Ustahikifu) imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo haaamini. (Yasin,36:7)

    قال السعدي: إنما حق عليهم القول بعد أن عرض عليهم الحق فرفضوه، فحينئذ عوقبوا بالطبع على قلوبهم. اهـ.

    Amesema As-Sa’diy akifasiri Aya hiyo: Kauli au Ahadi ya Mwenyezi Mungu imewastahiki, baada ya kuwaeleza wajibu wao, lakini wakakataa maelzo hayo, hivyo basi wakaadhibiwa kutokana na tabia ya ukaidi na ukanushi ndani ya nyoyo zao.

    وقوله تعالى: وتمت كلمت ربك صدقا وعدلا لا مبدل لكلماته وهو السميع العليم {الأنعام: 115}

    Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. (Al-An’am 6:116)

    Ndiyo maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu, yasemayo:

    إِلَّا مَنْ رَحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ

    Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja (HUUD,11:119)

    قال ابن كثير: يخبر تعالى أنه قد سبق في قضائه وقدره، لعلمه التام وحكمته النافذة، أن ممن خلقه من يستحق الجنة، ومنهم من يستحق النار، وأنه لا بد أن يملأ جهنم من هذين الثقلين الجن والإنس، وله الحجة البالغة والحكمة التامة. اهـ.

    Ibn Kathiir akifasiri Aya hizi, amesema: “Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba: Kutokana na Ujuzi wke wa Utangu, Ameshaamua kupitia Hukumu Zake na Maaaliwa yake, kupitia Ujuzi wake kamilikfu, uliotimia na kutokana na Hekima zake, kuwa wapo waja Wake ambao Wanastahiki kuingia Peponi, na wapo Wanaostahiki kuingia Motoni. Na kwamba ni uhakika kuwa Moto wa Jahannam utajazwa na Viumbe Vyake hivyo, viwili: Majini na Wanaadamu; na hivyo Mweniezi Mungu Ana Hoja kamili na timilifu, na Hekima iliyokamilika.”

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

    HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO!‎ ‎
    Limejibiwa na Sayyid Abdulqadir Shareef
    *Mtumishi wa Sunna za Mtume ﷺ *

    من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
    خادم السنة النبوية

  • Ufafanuzi wa Aya Zenye Msamaha na Adhabu

    Ufafanuzi wa Aya Zenye Msamaha na Adhabu

    NIMEULIZWA NANUKUU:-

    Swali langu Al Habib Allah Katika quran katupa nafasi ya kuomba msamaha tunapokosea turejee kwake, na pia katuambia anasamehe madhambi yote, Aya nyengine anasema Allah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo duni ya hayo kwa amtakaye Na aya nyengine anasema mwenye kumuua muumini kwa kukusudia malipo yake jahanam milele na laana ya Allah juu yake. Sasa suala langu msingi nataka kujua hizi aya ipi mansuh

    JIBU
    BISMILLAH

    Umeshapata MAJIBU katika Aya hizo zote. Hakuna zaidi.

    Acha nifafanue!

    1.Atayekufa bila ya kutubu hatia ya ushirikina HANA MSAMAHA.

    2.HAKI YOYOTE ILIYOPO BAINA YA MJA NA MOLA WAKE, INAWEZA KUSAMEHEWA NA MOLA WAKE, AKITUBU TOBA YA KWELI NA KURUDI KWA MOLA WAKE, KABLA YA KUFA KWAKE.

    3.HAKI YOYOTE ILIYOPO BAINA YA MWANADAMU NA MWANADAMU MWENZIWE, HAIWEZI KUSAMEHEWA ISIPOKUWA ALIYE DHULUMIWA ASAMEHE, VENGINEVYO ITALIPISHWA KWENYE MAHAKAMA YA MBINGUNI.

    4.HUKUMU YA KUMUUA MWISLAMU, PASI NA HAKI, NI KUUAWA ALIYEMUUA. AKIKIMBIA KUULIWA DUNIANI, AKAFA BILA YA KUTUBU, ATAISHIA KUINGIZWA MOTONI MILELE.

    FULL STOP.

    والله أعلم

    وبالله التوفيق

  • BM.14.11.\3.6 MLANGO KUHUSU ADHABU YA WIZI

    BM.14.11.\3.6 MLANGO KUHUSU ADHABU YA WIZI

    Hadithi ya Leo, Jumaane, tarehe 29, Mfungo Tano, 1446, H. sawa na tarehe 03, Ogasti, 2024

    SEHEMU YA SITA

    KUHUSU ADHABU YA WIZI

    1236* وَعَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ؛ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ  قَالَ: لَا يَغْرَمُ السَّارِقُ إِذَا أُقِيمَ عَلَيْهِ الْحَدُّ. رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَبَيَّنَ أَنَّهُ مُنْقَطِعٌ. وَقَالَ أَبُو حَاتِمٍ: هُوَ مُنْكَرٌ*.

    1. Imepokewa kutoka kwa Abdulrahman bin Awf **رضي الله عنه akisema: “Amesema Mtume : “Halipishwi mwizi fidia ya kitu alichokiiba, baada ya kupitishiwa hukumu ya kukatwa mkono.” Ameipokea Nasai ila amebainisha kuwa Riwaya yake haikufika kwa Mtume . Abu Hakim anasema: Riwaya hii ni Munkari.

    UFAFANUZI

    Haidithi hii, pamoja na kwamba maana yake ni sahihi kuwa mwizi akithibitika kuwa ameiba na akakatwa mkono wake, haijuzu kumtaka alipe fidia ya kitu alichoiba, ila Isnadi yake ni pungufu, haijakamilika, maana mpokezi mmoja aitwaye Al-Miswar bin Ibrahim bin Abdurrahman bin Awf, hajakutana na Babu yake Abdurrahman bin Awf, lakini katika Hadithi amesema kuwa ameipokea kutoka kwa Abdurrahman bin Awf, ambaye ni babu yake. Hata Abu Hatim ameipokea hivyo hivyo, na kuishia kusema kuwa Hadithi hiyo ni Munkari; yaani haiwezi kukubaliwa kuwa ni maneno yametoka kwa Mtume ﷺ ; maana mtu yeyote akithibitika kutenda hatia na akatiwa adhabu ya Mwenyezi Mungu, hawezi kutakiwa alipe fidia ya kitu alichokiiba, wala kutakiwa arudishe alichokiiba, baada ya kutiwa adabu ya Mwenyezi Mungu. Hivyo, mafunzo yake ni kweli, lakini matamshi yake kunasibishwa kwa Mtume ﷺ siyo kweli.

    YALIYOMO NA YATOKANAYO

    1. Mwizi aliyeiba kitu cha mtu mwengine, ana haki mbili:
      a) Haki mahasusi, nayo ni kitu alichokiiba iwapo kipo; au kutozwa fidia iwapo alichokiiba hakipo, au kutozwa thamani ya alichokiiba, iwapo alichokiiba kimepotea au kimeharibika.
      b) Haki ya Jamii ya Waislamu, juu yake, na hiyo ndiyo Haki ya Mwenyezi Mungu, ya kukatwa mkono baada ya kukamilika masharti na nguzo za kukatwa mkono, au kuaziriwa iwapo hayajakamilika masharti ya kukatwa mkono.
    2. Iwapo kitu alichokiiba kipo salama, kama kilivyokuwa kabla ya kuibiwa, basi wanazuoni wa Kiislamu wameafikiana kuwa ni wajibu kurudishwa kwa mmiliki wa kitu hicho, na hakuna adhabu ya mwizi aliyekiiba kukatwa mkono, bali atatiwa adhabu ya kuaziriwa na kufedheheshwa hadharani.
    3. Haki ya Mwenyezi Mungu, ikithibitika hatia, lazima ipitishwe, ambayo ama ni Adhabu kubwa iliyowekwa juu ya aliyetenda Hatia, au adhabu ndogo, nayo ni kufedheheshwa hadharani, ili ajulikane kuwa ni mtu aliyewahi kuvuka mpaka ya Mwenyezi Mungu, makusudi.
    4. Adhabu za Mwenyezi Mungu kwa Hatia mbali mbali, hazikuwekwa kuwa ni ndiyo lengo lenuyewe, bali ni Onyo na Tahadhari kwa wengine, wasitende hatia husika; hivyo ni wajibu wa kukamilisha lengo hilo la kuzuwia wengine wasitende hatia hiyo.
    5. Haki ya Mwenyezi Mungu haiepukikji baada ya kufikishwa aliyetenda Hatia ya Adhabu, akishafikishwa mbele ya Mwenye mamlaka rasmi ya kupitisha Sharia za Mwenyezi Mungu.
    6. Hakuna junaha kwa aliyetenda hatia ya Adhabu ya Mwenyezi Mungu, kutopitishwa Adhabu ya Mwenuyezi Mungu, KABLA ya kufikishwa mbele ya Mwenye Mamlaka ya kusimamia Sharia, kwa kusamehewa na aliyedhulumiwa au aliye dhuriwa na mtenda hatia.
    7. Inajuzu kwa mtu aliyedhulumiwa au kudhuriwa, kumsamehe aliyemdhulumu au kumdhuru, kama alivyosema Mtume ﷺ : “لا يحل مال امرىء مسلم، إلاَّ بطيبة من نفسه” Haimjuzii mtu kujihalalishia mali ya mtu Mwislamu mwengine, isipokuwa akiridhia kumhalalishia.”

    والله أعلم

    وبالله التوفيق