Swala ya kuomba Mvua
Assallam alleykum warahmatullah wabarakatuh
TAFSIRI YA UFUPISHO WA KITABU CHA SWAHIHIL-BUKHARI*
مختصر صحيح البخاري للزبيدي
رتبه ثم فسره إلى السواحلية ووضع بعض تعليقات
السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم العلوي الحسيني
خادم السنة النبوية
*MUHTASAR WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY.
*Kimetayarishwa kisha Kufasiriwa kwa Kiswahili *
Sayyid Abdulqadir Shareef
MTUMISHI WA HADITHI ZA MTUME
*Leo Siku ya Jumanne, tarehe 03 Jumada Awwal, 1446, H., sawa na tarehe 05, Novemba, 2024. *
(15)
كِتاب الِاسْتِسْقَاءِ
KITABU CHA SWALA YA KUOMBA MVUA
3- بَاب: سُؤَالِ النَّاسِ الْإِمَامَ الِاسْتِسْقَاءَ إِذَا قَحَطُوا
3. Mlango: Watu kumuomba kiongozi aombe mvua wanapofikwa na janga la ukame
549- عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ: رُبَّمَا ذَكَرْتُ قَوْلَ الشَّاعِرِ، وَأَنَا أَنْظُرُ إِلَى وَجْهِ النَّبِيِّ ﷺ يَسْتَسْقِي، فَمَا يَنْزِلُ حَتَّى يَجِيشَ( ) كُلُّ مِيزَابٍ، وَهُوَ قَوْلُ أَبِي طَالِبٍ:
وَأَبْيَضَ يُسْتَسْقَى الْغَمَامُ بِوَجْهِهِ
[رواه البخاري: 1009]. ثِمَالُ الْيَتَامَى( ) عِصْمَةٌ لِلْأَرَامِلِ( )
549. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar رضي الله عنهما akisema: “Wakati mwengine hukumbuka maneno ya mshairi mmoja wakati mimi namuangalia Mtume ﷺ akiwa anatuombea mvua na hakuacha kuendelea kuomba mvua mpaka tunaona maji yanatirika katika kutoka katika kopo la kutiririka mani ya mvua. Na mshairi ninaye mkumbuka ni Abu Twaalib aliyesema: “Na mtu mmoja, mweupe ambaye hutokana na jaha yake na utukufu wake, watu huomba wateremshiwe mawingu ya kuleta mvua, chakula cha mayatima na ulinzi au ngao kwa wajawazito wenye watoto tumboni.” [Bukhari: 1009] Yaani Abu Twalib anamtaja Mtume ﷺ kuwa watau walikuwa wanapotaka kuomba mvua, walikuwa wakimuendea awaombee mvua, kutokana na jaha yake na utukufu wake.
550- عَنْ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رضي الله عنه أَنَّهُ كَانَ إِذَا قَحَطُوا اسْتَسْقَى بِالْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ رضي الله عنه فَقَالَ: اللَّهُمَّ إِنَّا كُنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِنَبِيِّنَا فَتَسْقِينَا، وَإِنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِعَمِّ نَبِيِّنَا فَاسْقِنَا، قَالَ: فَيُسْقَوْنَ. [رواه البخاري: 1010].
550. Imepokewa kutoka kwa Umar bin Khattwab رضي الله عنه akisema: “Walikuwa na kawaida pale wanapopatwa na ukame huenda kumchukua Abbas bin Abdul Muttwalib رضي الله عنه –Ammi wa mtume ﷺ – humtanguliza mbele kuomba mvua na husema: “Ewe Mola wetu tulikuwa tunatawasali kwako kwa Mtume ﷺ na unatuteremshia mvua leo tunatawasali kwako kwa ammi wa mtume wetu ﷺ basi tuteremshie mvua” anasema Al Abbas kwamba: “Na mvua huteremka.” [Bukhari: 1010]
4- بَاب: الِاسْتِسْقَاءِ فِي الْمَسْجِدِ الْجَامِعِ
4. Mlango: Kuomba mvua katika msikiti mkuu wa Ijumaa
551- حَدِيثُ أَنَسِ رضي الله عنه فِي الرَّجُلِ الَّذِي دَخَلَ الْمَسْجِدَ وَالنَّبِيُّ رضي الله عنه قَائِمٌ يَخْطُبُ فَسَأَلَهُ الدُّعاءَ بِالغَيْثِ، تَكَرَّرَ كَثِيرًا.( ) وَفِي الرِّوَايَةِ: فَمَا رَأَيْنَا الشَّمْسَ سِتًّا. ثُمَّ دَخَلَ رَجُلٌ مِنْ ذَلِكَ الْبَابِ فِي الْجُمُعَةِ المُقْبِلَةِ، وَرَسُولُ اللَّهِ رضي الله عنه قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَهُ قائمًا، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلَكَتْ الْأَمْوَالُ، وَانْقَطَعَتْ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُمْسِكْهَا عَنَّا. قَالَ: فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ رضي الله عنه يَدَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلَا عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الْآكَامِ وَالجِبَالِ، وَالآجَامِ وَالظِّرَابِ،( ) وَبُطُونِ الْأَوْدِيَةِ وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ» قَالَ: فَانْقَطَعَتْ، وَخَرَجْنَا نَمْشِي فِي الشَّمْسِ. [رواه البخاري: 1013].
551. Hadithi ya Anas رضي الله عنه kuhusu mtu aliyeingia msikitini na mtume ﷺ anakhutubia siku ya Ijumaa akamuomba aombee watu mvua, Hadithi hiyo imepokewa mara nyingi sana. Katika riwaya hii hapa anasema Anas رضي الله عنه : “Hatujapata kuona jua kwa muda wa siku sita baada ya Mtume ﷺ kuomba mvua, baadae akaja mtu yuleyule akaingia msikitini mlango ule ule akamuelekea mtume ﷺ ambaye wakati huo anakhutubu akasimama kumwambia: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu mali zetu zote zimeangamia, njia zote zimefungika tunakuomba umuombe Mwenyezi Mungu aizuie mvua” mtume ﷺ akainua mikono yake mbinguni na akaomba: اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلَا عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الْآكَامِ وَالجِبَالِ، وَالآجَامِ وَالظِّرَابِ،( ) وَبُطُونِ الْأَوْدِيَةِ وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ [Ewe Mwenyezi Mungu teremsha mvua hii kando kando yetu na si juu yetu, Ewe Mwenyezi Mungu iteremshe mvua hii kwenye vilima na majabali kwenye vichuguu vya mawe na vichuguu vya udongo na kwenye mabonde ya maji na katika maeneo ya kuota miti]” anasema: basi mvua ikakatika na tukatoka tunatembea chini ya jua kali.” [Bukhari: 1013]
KUTOKA *UFUPISHO WA SWAHIHIL-BUKHARI, YA AZ-ZABIIDY *
*HIFADHI NDANI YA SIMU YAKO ILI UWEZE KUMTUMIA MWENZAKO! *
من السيد عبد القادر شريف آل الشيخ أبى بكر بن سالم
خادم السنة النبوية
Leave a Reply